Zaidi Ya Watumishi Hewa 17,100 Wafukuzwa Serikalini

nkanga chief

JF-Expert Member
May 31, 2016
2,084
1,620
Amesema kuwa zoezi la uhakiki lililoanza march hadi september mwaka 2016 limebaini watumishi hewa 17100 limeisababishia hasara serikali kubwa pia waziri simbachawe amekili kuwa zoezi la uhakiki wa watumishi hewa limechelewesha ajira mpya kwa kiasi kikubwa

======

Serikali imewabaini na kuwafukuza zaidi ya watumishi hewa 17100 katika kipindi cha miezi sita huku watumishi hao wakitajwa kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo kupata mikopo kwa njia zisizo za halali na kulisababishia taifa hasara kubwa.

Waziri wa nchi ofisi ya rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe Angela Kairuki anatoa takwimu hizo za watumishi hewa katika hafla ya kuwaapisha wakurugenzi wapya wa halmashauri 13 walioteuliwa na rais John Magufuli hivi karibuni ambapo amesema kwa kipindi cha mwezi March hadi September idadi hiyo imebainika huku zoezi hilo likitajwa kuwa endelevu.

Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene amesema kubainika kuwepo kwa watumishi hewa kumechangia kwa kiasi kikubwa kuchelewesha ajira mpya huku akionya baadhi ya watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kupotosha umma kuhusu ajira waache mara moja kabla hawajachukuliwa hatua

Nao baadhi ya wakurugenzi hao wapya baada ya kula kiapo cha maadili ya viongozi wa umma wamesema wamepokea uteuzi huo na wako tayari kufanya kazi kwa kuzingatia maagizo ya rais katika maeneo yao.


Chanzo: ITV
 
Hivi watatumia hii hoja mwaka mzima wa fedha kutuzuga?Uhakiki gani huu usiofika mwisho?
Hapa dunia kuna serikali zenye akili na serikali njinga!! Sasa sijui hii ya kwetu inaangukia wapi? Sasa hivi wamekuja na uhakiki wa vyeti vya shule za msingi, utaje walimu watatu na masomo waliyokufundisha huko (kusoma na kuandika), wanafunzi watatu mliosoma nao huko, hivyo hivyo sekondari, chuo n.k. Sasa watuambie Mwigulu alisoma shule gani ya msingi kwa jina hilo la Kisukuma? Saidi Bagaile alimaliza shule ya msingi wapi na kwenda sekondari na jina hilo analolitumia sasa hivi? Nafikri hawa wahakiki watumishi hewa wangeanza na hao mawaziri wetu watukufu!!
 
AMESEMA KUWA ZOEZI LA UHAKIKI LILILOANZA MARCH HADI SEPTEMBER MWAKA 2016 LIMEBAINI WATUMISHI HEWA 71000 LIMEISABABISHIA HASARA SERIKALI KUBWA PIA WAZIRI SIMBACHAWE AMEKILI KUWA ZOEZI LA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA LIMECHELEWESHA AJIRA MPYA KWA KIASI KIKUBWA

SOURCE.ITV

ANGALIZO:

Mnapokuwa mnatizama News Bulletin zozote kama unajua huna uwezo wa kukariri au kushika kitu unachokisikia basi uwe una notebook yako pembeni na uwe unaandika kama kumbukumbu kwako la sivyo utakuwa unawapoteza Watanzania wote kwa uzushi. Siku nyingine try to be accurate Mkuu. Hajasema Watu 71000 kama ulivyotudanganya hapo katika bandiko lako bali kasema kwamba tokea mwezi March hadi September wamebaini Watumishi hewa 11,600 na ambao wameshawachukulia hatua za kuwafukuza Kazi ila zoezi la kuwabaini wengine bado linaendelea.

Halafu katika Kiswahili sanifu hakuna neno " amekili " bali kuna neno " amekiri ". Huwa sipendi kuona a very native Tanzanian anakosea ama kuzungumza au kuandika Kiswahili fasaha halafu Mimi " mgeni " tu tena kutoka nchini kwetu Rwanda nakijua vizuri mno hiki Kiswahili chenu na nakipenda sana kukizungumza na kukitumia katika kukiandika. Akhsante Mkuu na nimeona nikupe " makavu " yako " mubashara " kabisa.
 
Nimegundua ni wachache ndio wanafuatilia taarifa ya habari wengi hawafuatilii coz idadi ni watumish hewa 17100 sasa mleta mada amekosea hiyo idadi na wale wenzangu na mimi ndio kwanza kureply bila hata kuangalia wapi pamekosewa.
 
Ila watu aisee wana viwanda vya uongo na upotoshaji!! yule mama amesema watumishi hewa ni elf 17+ jamani huu uongo na upotoshaji utaisha lini!!!
 
Wanatafuta sababu za kutokuajiri vijana, kupandisha vyeo watumishi na kuongeza mishahara! Walete mbinu nyingine hii ya watumishi hewa tumeichoka sasa.
 
Back
Top Bottom