Zaidi Ya Watumishi Hewa 17,100 Wafukuzwa Serikalini

kwenye vyombo vyetu vya ulinzi hakuna? basi huko safi sana wapo makini sana hongereni
Makao makuu ya vyeti kanjanja na watumishi hewa ni huku kwenye majeshi. Namshangaa waziri anazungumza kana kwamba ndyo tayari wamemaliza. Mbona bado kwenye majeshi yetu?
 
hewa inafukuzwa ua inagundulika kama iliwezekanika kumfukuza kwa nini hawakumkamata huyo hewa na kumpeleka polisi alipe alichojipatia kwa njia ya udanganyifu na huyo aliyekuwa analipa hizo hewa tatizo lake nini uelewa mdogo au naye ni mdanganyifu sasa wakisha wafukuza nani atalipa walicholipwa bila kustahili
 
Amesema kuwa zoezi la uhakiki lililoanza march hadi september mwaka 2016 limebaini watumishi hewa 17100 limeisababishia hasara serikali kubwa pia waziri simbachawe amekili kuwa zoezi la uhakiki wa watumishi hewa limechelewesha ajira mpya kwa kiasi kikubwa

======

Serikali imewabaini na kuwafukuza zaidi ya watumishi hewa 17100 katika kipindi cha miezi sita huku watumishi hao wakitajwa kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo kupata mikopo kwa njia zisizo za halali na kulisababishia taifa hasara kubwa.

Waziri wa nchi ofisi ya rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe Angela Kairuki anatoa takwimu hizo za watumishi hewa katika hafla ya kuwaapisha wakurugenzi wapya wa halmashauri 13 walioteuliwa na rais John Magufuli hivi karibuni ambapo amesema kwa kipindi cha mwezi March hadi September idadi hiyo imebainika huku zoezi hilo likitajwa kuwa endelevu.

Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene amesema kubainika kuwepo kwa watumishi hewa kumechangia kwa kiasi kikubwa kuchelewesha ajira mpya huku akionya baadhi ya watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kupotosha umma kuhusu ajira waache mara moja kabla hawajachukuliwa hatua

Nao baadhi ya wakurugenzi hao wapya baada ya kula kiapo cha maadili ya viongozi wa umma wamesema wamepokea uteuzi huo na wako tayari kufanya kazi kwa kuzingatia maagizo ya rais katika maeneo yao.


Chanzo: ITV
serikali iliyokosa dira!
 
Back
Top Bottom