Consigliere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 12,037
- 24,596
Unamfukuzaje mfanyakazi hewa?
Ndio maana tukamwambia mleta uzi aandike vizuri, inaonekana alikosea figure.Hii idadi uliyoionyesha hapa mbona ni kubwa, au hawa viongozi wanaficha idadi halisi
Kwenye post ya awali kabisa, naona wamerekebisha. Ndio maana tunasema kable ya kuleta uzi watulie kwanza.Hizo number umetoa wapi?
Aisee, natafuta mwalimu wa kiswahili hapa shuleni kwangu,hebu nipm ule shavu.
Vijana msivunjinge moyo Ajira zenu zinakuja. Vuteni subira
Wadanganyika tunaendelea kudanganywa!Unamfukuzaje mfanyakazi hewa?
Aliyekojoa karibu na geti la kuingia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na yule aliyekojoa karibu na geti la kuingilia kambi yoyote ya Jeshi wote hawa wakikamatwa " adhabu " zao zinalingana? Nasubiri jibu kisha nilale zangu.
Jamani hata Kiswahili kumbe ni kigumu namna hii?Amesema kuwa zoezi la uhakiki lililoanza march hadi september mwaka 2016 limebaini watumishi hewa 17100 limeisababishia hasara serikali kubwa pia waziri simbachawe amekili kuwa zoezi la uhakiki wa watumishi hewa limechelewesha ajira mpya kwa kiasi kikubwa
======
Serikali imewabaini na kuwafukuza zaidi ya watumishi hewa 17100 katika kipindi cha miezi sita huku watumishi hao wakitajwa kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo kupata mikopo kwa njia zisizo za halali na kulisababishia taifa hasara kubwa.
Waziri wa nchi ofisi ya rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe Angela Kairuki anatoa takwimu hizo za watumishi hewa katika hafla ya kuwaapisha wakurugenzi wapya wa halmashauri 13 walioteuliwa na rais John Magufuli hivi karibuni ambapo amesema kwa kipindi cha mwezi March hadi September idadi hiyo imebainika huku zoezi hilo likitajwa kuwa endelevu.
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene amesema kubainika kuwepo kwa watumishi hewa kumechangia kwa kiasi kikubwa kuchelewesha ajira mpya huku akionya baadhi ya watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kupotosha umma kuhusu ajira waache mara moja kabla hawajachukuliwa hatua
Nao baadhi ya wakurugenzi hao wapya baada ya kula kiapo cha maadili ya viongozi wa umma wamesema wamepokea uteuzi huo na wako tayari kufanya kazi kwa kuzingatia maagizo ya rais katika maeneo yao.
Chanzo: ITV
Mmm mbona kwenye majeshi bado?Amesema kuwa zoezi la uhakiki lililoanza march hadi september mwaka 2016 limebaini watumishi hewa 17100 limeisababishia hasara serikali kubwa pia waziri simbachawe amekili kuwa zoezi la uhakiki wa watumishi hewa limechelewesha ajira mpya kwa kiasi kikubwa