Waziri wa kilimo amesema watu wauze mazao yao ndani na nje ya nchi hakuna kuzuia wasiuze nje ya nchi

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,617
3,936
wale wote wanaolalamika bei ya vyakula na nafaka imependa bei waziri ameamua kutoa kauli ya mwisho kuwa hakuna kufunga mipaka kwasababu ya bidhaa za nafaka kuuzwa nje ya nchi amesema niwakati wa mkulima kunufaika na mazao yake swala la budget ya chakula ni wewe na familia yako utapanga mwenyewe, hata hivyo amesema mfumuko wa bei siyo wa wizara ya kilimo ameshauri wanauchumi wanakila sababu ya kushauri serkali namna bora ya kuweza kukabiliana na mfumuko wa bei za vyakula na bidhaa ngingine kwa ujumla.

Ndugu zangu kama umelima na ukavuna uza lakini tunza chakula hali imekuwa tete siyo vyakula wala bei ya bidhaa nyingine kila kitu kipo juu.

maneno ya waziri amemaanisha kila mtu atumie akili yake kukabiliana na janga hilo. ukipenda uza popote upendapo lakini njaa ipo.
 
Naunga mkono hoja,ukitaka bei rahisi kalime ila kujaza vitambi huko mjini na uzauza maji ya kandoro ni matumizi mabaya ya potential yako..

Ngoja njaa ikikuchapa utajua cha kufanya..
 
Ok wauze mahindi huko kwao Somalia kwenye njaa.

Wazalendo nchi hii ni wa kuwahesabu.
 
Kama ni sawa kuuza mazao kokote. Bas iwe sawa kuagiza bila utitiri wa kodi
 
Bashe akili nyingi sana.! Ni wakati sasa wa sisi tulioko mijini na tusio na ajira kwenda kujikita kwenye kilimo kwani mazao sasa ni biashara.!!
Eko Bashe,
Usiwastue waache waendelee kulalamika,hayo majitu ya Mijini kwanza siwezi kuyatetea kabisa..

Yamekataa tozo Kwa za kuhudumia Vijijini ila yanataka kula jasho la wakulima..

Serikali kamatieni hapo hapo hadi akili ziwakae sawa.
 
Mtoa mada unazungumzia hutuba aliyoitoa singida au ? Kama ni ile unapotosha umma
 
Wacheni wakulima wafaidi jasho lao. Watu hamtaki kulima mnakimbilia mjini mkitegemea wakulima wanyonge ndio wawalishe. Sasa ni hivi wakulima wauze wanakoona wanapata faida mzuri na kisha waweke akiba ya kuwatosha wao tuu.

Kama serikali itqkuwa serious na food insecurity next year, basi inunue vyakula kwa bei nzuri na kuvihofadhi ili wakulima wasiuze nje
 
Back
Top Bottom