Waziri wa kilimo amesema watu wauze mazao yao ndani na nje ya nchi hakuna kuzuia wasiuze nje ya nchi

wale wote wanaolalamika bei ya vyakula na nafaka imependa bei waziri ameamua kutoa kauli ya mwisho kuwa hakuna kufunga mipaka kwasababu ya bidhaa za nafaka kuuzwa nje ya nchi amesema niwakati wa mkulima kunufaika na mazao yake swala la budget ya chakula ni wewe na familia yako utapanga mwenyewe, hata hivyo amesema mfumuko wa bei siyo wa wizara ya kilimo ameshauri wanauchumi wanakila sababu ya kushauri serkali namna bora ya kuweza kukabiliana na mfumuko wa bei za vyakula na bidhaa ngingine kwa ujumla.

Ndugu zangu kama umelima na ukavuna uza lakini tunza chakula hali imekuwa tete siyo vyakula wala bei ya bidhaa nyingine kila kitu kipo juu.

maneno ya waziri amemaanisha kila mtu atumie akili yake kukabiliana na janga hilo. ukipenda uza popote upendapo lakini njaa ipo.
Wazara ya kilimo imepata msimamizi imara. Naunga mkono mawazo ya waziri 100%. Mungu akubariki Santa Bashe na fikra zako zidumu.
 
kila mtu apambane na hali yake
Hivi nikodi au ninunue kipande cha ardhi,na wakati mwingine nimechukuwa mkopo,niweke gharama za kulimia,mbolea,mbegu, mulching, kuotesha/kupanda, kupalilia,kulinda wanyama waharibifu,irrigation kuvuna,biocide,packing,kuhifadhi kwenye maghala,transportation n.k
Harafu nisiwe na uhuru wa kutafuta bei ya soko la mazao yangu ndani au nje ya nchi?

Ongezeko kubwa la bei ya mazao ya chakula ni wake up call kwa wananchi walio wengi kuchukua hatua stahiki kwa kuongeza nguvu katika kilimo cha mazao ya chakula.
Ardhi ipo,nguvu kazi ipo.Hizo nguvu za machinga,na majobless kibao waliojazana mjini wakisubiri kula bila kunawa japo kila mmoja wao alime robo eka ya mazao ya chakula.

Jambo baya zaidi miaka ya hivi karibuni kumezuka kundi hatarishi hao middlemen maarufu kama madalali,mkulima atauza gunia la mahindi sh 10,000 lakini likifika kwa mlaji hasa mijini ni sh 70,000 bei mara saba,700%!!!.
Ni kundi au makundi hatarishi kwa mlaji,yabomolewe haraka iwezekavyo.

Mwisho ili kujenga usalama wa kuzalisha mazao ya chakula cha kutosheleza mahitaji ya nchi,serikali ikaribishe wakulima wakubwa hasa wa kizungu toka Uholanzi,Israel, Ukraine,Australia, Marekani, Ugiriki,n.k wapewe ardhi zilizopangiwa kilimo lakini hazitumiki kikamilifu.
Ukulima wa mashamba makubwa unahitaji mitaji mikubwa.
 
naunga mkono hoja wakulima wananunua mbolea mfuko wa 50kg kwa sh 150,000 halafu leo apangiwe mahali pa kuuza mazao yao
 
naunga mkono hoja wakulima wananunua mbolea mfuko wa 50kg kwa sh 150,000 halafu leo apangiwe mahali pa kuuza mazao yao
Sawa kabisa waziri kufanya hivyo itapunguza wazururaji mijini nakuona kilimo kama mgodi. Vijana wanakimbilia mijini ni bora warudi kulima kwa faida. Kuhusu kujiwekea akiba ni mtu mwenyewe apige hesabu zake vema maana hata tusinge uza nje bado kama siyo wakuweka akiba utauza kwenye soko la ndani
 
Naunga mkono hoja,ukitaka bei rahisi kalime ila kujaza vitambi huko mjini na uzauza maji ya kandoro ni matumizi mabaya ya potential yako..

Ngoja njaa ikikuchapa utajua cha kufanya..
Hakuna mkulima anaye jua hata mpaka wa Namanga, au Silari, kule au Tunda, hao ni walanguzi na by the way kwa sasa wanao shindwa kumudu bei ya chakula ni hao wakulima,
 
Hakuna mkulima anaye jua hata mpaka wa Namanga, au Silari, kule au Tunda, hao ni walanguzi na by the way kwa sasa wanao shindwa kumudu bei ya chakula ni hao wakulima,
Na mimi nakuambia kwamba hakuna mkulima anamiliki touch na kuja kulalamika humu jf..

Mwisho ni kwamba wafanyabiashara wadogo wadogo yaani Wachuuzi ndio wanapenda Vijijini wanakuja na mahindi kuwauzia hao wanaopeleka Namanga kwa hiyo unaposema sijui wakulima hawamudu Bei sasa mahindi yanatoka kwa nani?

Hii Bei mnayoilalamikia haiko Kijijini iko Mijini so nunueni Kwa bei ya soko la sivyi tokeni mjini mkalime.
 
wale wote wanaolalamika bei ya vyakula na nafaka imependa bei waziri ameamua kutoa kauli ya mwisho kuwa hakuna kufunga mipaka kwasababu ya bidhaa za nafaka kuuzwa nje ya nchi amesema niwakati wa mkulima kunufaika na mazao yake swala la budget ya chakula ni wewe na familia yako utapanga mwenyewe, hata hivyo amesema mfumuko wa bei siyo wa wizara ya kilimo ameshauri wanauchumi wanakila sababu ya kushauri serkali namna bora ya kuweza kukabiliana na mfumuko wa bei za vyakula na bidhaa ngingine kwa ujumla.

Ndugu zangu kama umelima na ukavuna uza lakini tunza chakula hali imekuwa tete siyo vyakula wala bei ya bidhaa nyingine kila kitu kipo juu.

maneno ya waziri amemaanisha kila mtu atumie akili yake kukabiliana na janga hilo. ukipenda uza popote upendapo lakini njaa ipo.
Hii post hii imenichekesha sana na kunihuzunisha sana;

Naomba kuwa na orthodox thinking kwenye hili: kwa hakika ni JUKUMU LA SERIKALI KUDHITI MFUMUKO WA BEI LAKINI SII JUKUMU LA MKULIMA KUWATOLEA SADAKA WALIOJIAJIRI KWENYE SEKTA ZINGINE!!!

Hivi Kwa bei ya 70,000.00 bambopo msimu uliopita wakulima walinunua hadi 130,000.00 kwa mfuko wa mbolea ya kupandia peke yake, kilo ya mbegu mfano mahindi ni 15,000.00+ bado kuna gharama ya kupanda, palizi, uvinaji na gharama zingine, Je tunataka tumzuie mkulima huyu kuuliza nje ili TUNUNUE DEBE LA KILO 20 KWA 10,000.00?

Nafikiri kuna haja ya kuwa na Suluhu nzuri na sii vema kukimbilia kuwazuia wakulima kuuza nje!!! Kwa msimu huu serikali wanatoa ruzuku ya mbolea HIVYO WAKIDHIBITI KUUZA NJE NI SAWA. Lakini kwa mazao ya msimu uliopita kuwazuia ni kuwahujumu wananchi wenzetu!!!! Mbona mbolea, mafuta, ngano, saruji, Mabati yanapanda na hatulalamiliki kuwazuia au kuwalazimisha wauze kwa bei flani??? Kwa nini tumlazimishe Mkulima wa mahindi, mpunga na maharagwe????

Hatuoni kuwa tunakosea? Hatuoni tunawadhulumu wakulima hawa? Ambao wakati wanalima na familia zao hatukuwasaidia????

Sii jukumu lao kutulisha kwa wao kuingia HASARA bali ni jukumu la TAIFA KUTAFUTA NAMNA BORA YA KUDHIBITI HALI HILI IKIWEMO KUTOA RIZUKU ILI KUCHOCHEA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO!!
 
Back
Top Bottom