Waziri Bashe apigilia Msumari marufuku ya kuuza Mazao nje ya Nchi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,470
8,321

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kilichozuiliwa na Serikali ni watu kufanya biashara ya mazao kinyume na utaraibu.

Bashe amesema hayo alipokuwa akizindua Ofisi ya kuleta mabadiliko ya sekta ya kilimo nchini jijini Dodoma leo jumatatu Juni 19, 2023 ambapo ameeleza kuwa Serikali haitaruhusu mtu yeyeyote kusafirisha mazao nnje ya nchi ikiwa hajasajili kampuni, hana Tin namba, Taarifa za ulipaji kodi pamoja na leseni ya biashara husika.
 
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametoa Kauli ya Serikali sakata la Kupiga Marufuku kuuza Mazao ya Nje.

Waziri Bashe amesema Mazao ya Kilimo ni kama biashara zingine hivyo Serikali imeamua kurasimisha biashara ya mazao ya Kilimo kwa kuwataka exporters na Wageni wote kusajili kampuni Kwa Kasi hiyo ndio waruhusiwe kwenda kununua mazao kwa wakulima maana Serikali inahitaji Mapato na kuona sekta ya Kilimo inachangia kwenye mapato ya Nchi.

My Take: Hapa Sasa mumeeleweka na naunga mkono hoja Kwa ubunifu huu.

====

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kilichozuiliwa na Serikali ni watu kufanya biashara ya mazao kinyume na utaratibu.

Bashe amesema havo alipokuwa akizindua Ofisi va kuleta mabadiliko ya sekta ya kilimo nchini jijini Dodoma leo jumatatu Juni 19, 2023 ambapo ameeleza kuwa Serikali haitaruhusu mtu yeyeyote kusafirisha mazao nnje ya nchi ikiwa hajasajili kampuni, hana Tin namba, Taarifa za ulipaji kodi pamoja na leseni ya biashara husika.

Chanzo: Mwananchi
 
Safi sana,hili jambo nilikuwa lilikuwa linanishangaza sana.Wakenya walikuwa wanakwenda kuchukua mahindi,Michele,parachihi na viazi mviringo kienyeji enyeji tu -huku wao wakipata faida Mara dufu.
Emu jaribu kufikia wewe Mtanzania utoke hapa uende Kenya kama unaweza nunua vitu kienyeji namna hiyo
 
Ploblem cannot be solved by the same lever of thinking that creates them... peter msigwa(as he then was)
 
Wengine tulipinga humu ule utaratibu wa hovyo na wa kienyeji uliotumika hapo awali! Badala ya kusikilizwa, tuliishia tu kutukanwa na kukejeliwa na watu wenye vichwa mninga.
 
Nilichosikia pale Himo ni kwamba marufuku kupeleka mahindi nje na wenye malori wakawa wanaelekezwa wakauzwe kwenye maghala ya Taifa.....

Sikusikia ukiukwaji wa Sheria katika Biashara hii.....Bashe alikuwa hajui kama kuna watu wanauza mahindi kinyume na Utaratibu mpaka Rais ametoa amri......na bado yuko ofisini???
 
Back
Top Bottom