Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,831
- 4,586
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali haijazuia kuuza mazao nje ya Nchi isipokuwa imezuia Watu kufanya biashaea bila kufuata utaratibu wa kisheria .
Bashe ametoa kauli hiyo June 21, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara aliyetaka kujua sababu za magari ya mazao kuzuiwa katika mpaka wa Silali baada ya zuio la Waziri kusitisha kuuza mazao nje ya Nchi.
Waziri Bashe amesema ‘’Haiwezekani Mtu unanunua mahindi Songea unapakia kwenye malori hauna leseni ya biashara, hauna TIN namba halafu unataka Nchi ikuruhusu Kwenda kuuza nje mazao hayo , malipo hayaonekani katika mfumo rasmi wa fedha, hatuzipati data , maelekezo ya Rais yako wazi Mtanzania yeyote anayetaka kufanya biashara ya mazao kwaajili ya kuuza nje au ndani akate leseni ya biashara”
‘’Nitumie Bunge lako tukufu kuwambia Wafanyabiasha wa mazao nendeni kwenye Hamashauri kateni leseni za biashara ili muuingie kwenye mfumo rasmi wa biasahara ya mazao ya kilimo, hatuwezi kuendelea katika mfumo huu unaondelea na nia ya Serikali ni kurasimisha shughuli za kilimo na shughuli za biashara za mazao”.
Pia Soma:
- Waziri Bashe apigilia Msumari marufuku ya kuuza Mazao nje ya Nchi