A
Anonymous
Guest
Mwalimu MWALUKASA wa Shule ya Sekondari JM KIKWETE, Halmshauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe anayefanyabiashara ya kuuza karanga shuleni analalamikiwa na Wanafunzi kuwalazimisha kununua karanga na kuwachapa viboko wanaoshindwa kufanya hivyo.
Inadaiwa Mwalimu huyo anayefundisha Somo la Kiswahili katika shule hiyo amekuwa akitumia makosa ya Wanafunzi kama mtaji wa Biashara yake.
Inadaiwq kuwa Siku ya Aprili 23, 2024 aliingia katika madarasa ya Kidato cha Kwanza na kuanza kuwaadhibu Wanafunzi wote akidai wamefeli Somo la Kiswahili huku akiwataka kununua karanga ili wapunguziwe adhabu.
Wanafunzi walionunua karanga kuanzia za Sh 300 walisamehewa adhabu na wale walioshindwa walichapwa fimbo kuanzia 10 na kuendelea.
Wakati akitoa adhabu ya viboko kwa ambao walishindwa kununua karanga waliadhibiwa viboko zaidi ya 10 kwani aliwaalika Walimu wenzie wawili akiwemo Mwalimu OBOTE na MALIVA na kutoa adhabu kama ifuatavyo katika madarasa ya Kidato cha Kwanza A na B.
Mwalimu Mwalukasa aliwachapa viboko 7.
Sir Obote 4.
Maliva 3.
Je, ni Sawa Waalimu kufanya biashara Shuleni?
Je, ni sawa Mwanafunzi kuadhibiwa viboko zaidi ya vitatu kwa kosa anauliza Mdau?