KERO Walimu Sekondari JM Kikwete ya Tunduma waache kulazimisha Wanafunzi kununua karanga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kama unaweza fanya Kila namna mtoto wako asiwe mwl au polisi utakuwa umemsaidia ikibidi muelekeze kwenye biashara na maisha mengine hii kazi ajuae ni Mungu ila ni ngumu na Ina mitihani mizito sana
(By experience)It takes strong courage to live as a teacher
 
Wenyeji WA mkoa WA songwe Wana roho mbaya,wachawi na ni wabaguzi Kwa watumishi. Yawezekana mnamsagia kunguni huyo mwalimu .
 

Mwalimu MWALUKASA wa Shule ya Sekondari JM KIKWETE, Halmshauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe anayefanyabiashara ya kuuza karanga shuleni analalamikiwa na Wanafunzi kuwalazimisha kununua karanga na kuwachapa viboko wanaoshindwa kufanya hivyo.

Inadaiwa Mwalimu huyo anayefundisha Somo la Kiswahili katika shule hiyo amekuwa akitumia makosa ya Wanafunzi kama mtaji wa Biashara yake.

Inadaiwq kuwa Siku ya Aprili 23, 2024 aliingia katika madarasa ya Kidato cha Kwanza na kuanza kuwaadhibu Wanafunzi wote akidai wamefeli Somo la Kiswahili huku akiwataka kununua karanga ili wapunguziwe adhabu.

Wanafunzi walionunua karanga kuanzia za Sh 300 walisamehewa adhabu na wale walioshindwa walichapwa fimbo kuanzia 10 na kuendelea.

Wakati akitoa adhabu ya viboko kwa ambao walishindwa kununua karanga waliadhibiwa viboko zaidi ya 10 kwani aliwaalika Walimu wenzie wawili akiwemo Mwalimu OBOTE na MALIVA na kutoa adhabu kama ifuatavyo katika madarasa ya Kidato cha Kwanza A na B.

Mwalimu Mwalukasa aliwachapa viboko 7.
Sir Obote 4.
Maliva 3.

Je, ni Sawa Waalimu kufanya biashara Shuleni?
Je, ni sawa Mwanafunzi kuadhibiwa viboko zaidi ya vitatu kwa kosa anauliza Mdau?

Picha kwa msaada wa pronga69.blogspot
Hilo mbona tatizo dogo sana ambalo halikustahili kufika huku. Ungeanzia kwa mkuu wa shule, akishindwa kwa AEK, au mwenyekiti wa bodi ya shule.
Ungekuwa umemsaidia mwalimu na wanafunzi pia ila hapo moto lazima uwake.
 
Nimemkumbuka mwl. Haule
Tukiandikwa majina ya wapiga kelele anatuambia "ili nikusamehe nunua biscuit zangu moja 50"
Usiponunua unapigwa fimbo ukinunua unasamehewa kupiga kelele darasani.
Kwa hiyo ulikuwa unanunua biscuit? Pole saana
 
Sasa wewe ticha haujui yaliyomkuta mwenzio pale Mlowo alipokuwa anajaribu kuongeza mihela kupitia kipodozi ? Muache afanye hiyo biashara maana ni halali na sio ya magendo muache ajitafute maana alichukuliwa nyingi
 
Wazazi muwe mnawapa watoto japo hela za vikaranga vya ku-support hao walimu shuleni bhana, Nyie mmefanyiwa elimu bure mnashindwa kufanya hata hivyo vitu vidogovidogo jamani, Kwani mlilazimishwa kuzaa au mlifuata mikumbo?
 
Acha unoko wewe kwani hao madogo wakimuungisha huyo mwalimu kununua hizo karanga za 100 au 200 Kuna shida gani
 
Back
Top Bottom