KERO Walimu Sekondari JM Kikwete ya Tunduma waache kulazimisha Wanafunzi kununua karanga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
DSC01942.JPG

Mwalimu MWALUKASA wa Shule ya Sekondari JM KIKWETE, Halmshauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe anayefanyabiashara ya kuuza karanga shuleni analalamikiwa na Wanafunzi kuwalazimisha kununua karanga na kuwachapa viboko wanaoshindwa kufanya hivyo.

Inadaiwa Mwalimu huyo anayefundisha Somo la Kiswahili katika shule hiyo amekuwa akitumia makosa ya Wanafunzi kama mtaji wa Biashara yake.

Inadaiwq kuwa Siku ya Aprili 23, 2024 aliingia katika madarasa ya Kidato cha Kwanza na kuanza kuwaadhibu Wanafunzi wote akidai wamefeli Somo la Kiswahili huku akiwataka kununua karanga ili wapunguziwe adhabu.

Wanafunzi walionunua karanga kuanzia za Sh 300 walisamehewa adhabu na wale walioshindwa walichapwa fimbo kuanzia 10 na kuendelea.

Wakati akitoa adhabu ya viboko kwa ambao walishindwa kununua karanga waliadhibiwa viboko zaidi ya 10 kwani aliwaalika Walimu wenzie wawili akiwemo Mwalimu OBOTE na MALIVA na kutoa adhabu kama ifuatavyo katika madarasa ya Kidato cha Kwanza A na B.

Mwalimu Mwalukasa aliwachapa viboko 7.
Sir Obote 4.
Maliva 3.

Je, ni Sawa Waalimu kufanya biashara Shuleni?
Je, ni sawa Mwanafunzi kuadhibiwa viboko zaidi ya vitatu kwa kosa anauliza Mdau?
DSC01356.JPG

DSC01922.JPG
 
Inadaiwq kuwa Siku ya Aprili 23, 2024 aliingia katika madarasa ya Kidato cha Kwanza na kuanza kuwaadhibu Wanafunzi wote akidai wamefeli Somo la Kiswahili huku akiwataka kununua karanga ili wapunguziwe adhabu.
Sioni tatizo Lolote, Walimu Wana changamoto kubwa sana, graduate huyo Ujue, Hana overtime wala allowance yoyote ile wakati Serikali yake imetenga Billions kununua magari
 
Kwani Kuna Sheria inayomkataza mwalimu kujiongeza? Mlitaka akawauzie wafungwa magerezani? Keep it up mwalimu, tunajua mnayopitia.
Mwalimu anakaywa 2% ya mshahara kwenda CWT inakwenda kuliwa na walevi na wazinzi tu hawana MTU wa kuwatetea. Mwalimu anakaywa hela ndefu NHIF . Sasa hivi NHIF ime collapse mwalimu akifika hospitali anatakiwa achangie kutoka mfukoni kwani NHIF haiwezi kumlipia. (Waziri wa afya yupo anacheka cheka tu huku nhif unachungulia kaburi)
Mwalimu haruhusiwi kufundisha tuition ilhali wafanyakazi manispaa wanachukua mamilioni kwa kisingizio Cha safari ambazo hawaendi.
Mwalimu uza njugu hizo.
 
Hii inaitwa character assassination. Moderators mngefuta huu uzi wenye name calling.
 
Back
Top Bottom