Vijana kufanya kazi ya saidia Fundi mwisho mwaka mmoja tu zaidi ya hapo unatakiwa uwe fundi au uachane nayo

Ofcourse, mi mwenyewe nilishamshangaa sana dogo mmjoja amepiga saidia kwa zaidi ya miaka miwili na mpaka leo eti kazi yake ni kukoroga mchanga tu na kuwapelekea mafundi.
Tatizo kupata kazi ya ufundi
Mafundi wengi wanafahamika na jamii na ma engineer wa ujenzi
Wakiwa na kazi utasikia kampe fundi Fulani.Sasa huyo kibarua Hadi kuja kukubaliwa na kuaminiwa kuwa naye fundi apewe kazi ya ufundi sio Leo Wala kesho
 
Unakutana na kijana ana mwaka wa 4 anafanya saidia fundi

Unakaa unamshangaa , ina maana anafanya hii kazi pasipo malengo yoyote,

Kuna mawili , uachane na hiyo kazi au uwe tayali umejifunza ufundi..

Kinyume na kuendelea kuwa saidia fundi tu miaka na miaka ni kupoteza malengo..

Hakuna aliyepata mtaji kwa kazi ya saidia fundi kama wapo ni mmoja kwa kumi.
Uko sahihi kabisa , hapa nilipo kuna kijana mmoja amesaidia sana ndugu zake kwa kuwatumia kama SAIDIA FUNDI kwa muda na wao sasa ni mafundi na makundi yao.

Ujumbe huu uende mpaka kwa mafundi WAWASAIDIE wasaidizi hao ili wawe mafundi na kutanua wigo. Kila wakati nasikia kijana fulani kwa sasa amendable Dar KUEZEKA NYUMBA ,kachukuliwa na fulani.

Ww mbona hujaenda. Mimi fundi wangu ni fulani tunaondoka siku fulani kuelekea sehemu fulani kuna kazi pia. yaani mpaka inafurahisha ,vijana wameoa, wamejenga nyumba zao na usafiri wa pikipiki wanazo , kilimo wakati wa msimu wanalima INAPENDEZA, Mafundi wakuu hongereni.
 
Unafikiri kujifunza ni rahisi??Si rahisi kama unavyodhani na pia tuna vichwa tofauti katika kujifunza,,,Wapo wa haraka kujifunza na wale sloo Lena wanaojifunza Kwa taratibu mnoo na Si dhambi na ndio maisha yenyewe pia hatuwezi fanana kamwe,,wape Hongera kwa kazi vijana wako wa saiti,,waheshimu,,waombee na uwape matumaini pia,,###HakunaAlieKamili###
 
Ufundi Sasa hivi lazima uwe na vyeti labda ujenzi unaoongelea wewe ni uwe ule wa kujenga nyumba za uswahilini Lakini majengo yanayohitaji Contrator bila kuwa na vyeti kuajiriwa kama fundi hakupo mtu ataishia kuwa msaidizi wa fundi
Huo ufundi wa vyeti ni mpaka uwe na ada ulipe ili uupate.Uzi unaeleza kuhusu simple life ya uswazi.
 
Ufundi Sasa hivi lazima uwe na vyeti labda ujenzi unaoongelea wewe ni uwe ule wa kujenga nyumba za uswahilini Lakini majengo yanayohitaji Contrator bila kuwa na vyeti kuajiriwa kama fundi hakupo mtu ataishia kuwa msaidizi wa fundi
Mkuu hata hayo majengo yanayohitaji contractor,huyo huyo contractor anatumia mafundi ambao hawana vyetu ila Wana uzoefu na wanatoa kitu chenyewe. Contractor kazi yake inakuwa kusimamia tu huwa hawafanyi kazi yoyote.
 
Ni sawa na kutueleza kwamba barabara/reli zetu wamejenga Wachina/Bashing'waa!Wao ni waelekezaji tu.Tunajenga wenyewe.
 
Mkuu hata hayo majengo yanayohitaji contractor,huyo huyo contractor anatumia mafundi ambao hawana vyetu ila Wana uzoefu na wanatoa kitu chenyewe. Contractor kazi yake inakuwa kusimamia tu huwa hawafanyi kazi yoyote.
Hiyo ni Kwa local contractor asiye serious na kazi yake na ubora wa kazi

Ndio maana local contractors wengi kazi zao Huwa duni sababu ya kupenda cheap unprofessional labor ndio maana miradi mingi ya ujenzi hupewa wageni ambao huajiri mafundi professional waliopitia VETA sio kuokoteza wasaidizi wa mafundi barabarani
 
Back
Top Bottom