Ushauri; Tujipange kubadilika; Huenda miaka ijayo binadamu mzee zaidi ataishi mwaka mmoja tu na kuzeeka

Samico Tanzania

JF-Expert Member
Feb 6, 2022
296
811
Ulishawahi kuwaza zamani watu waliishije zama wayahudi? Walikuwa na maumbo gani?

Mfano ukiangalia umri wa maisha ya mfalme Suleimani alivyoishi miaka ile na wake zake?,vipi kuhusu kina yakoub, Daudi, ibrahim na wengine?

Naomba hili niliweke kimahesabu ili tuone mantiki!

Sitaki kujiuliza sana juu ya utaratibu wa mfalme selemani alivyoishi na wale wake zake na mahawala zake! Maana kama mwaka una siku 365, inamaana hata angelala na mke mmoja kila siku bado asingewamaliza!

Labda kama alikuwa analala na wake wawili kwa siku na hawala wawili hapo sawa lakini inje ya hapo selemani aliwatesa sana wale kina bibi kisaikolojia!!
(Anyway tuachane na maisha mitume)

Turudi kwenye umri wetu huu usiozidi miaka 120!

Umri huu wanasayansi wamebuni masomo meeengi, Sylabus nyiiingi sana tusome!

Miaka 7 ya kukua, 7 ya shule ya msingi, 6 ya sekondari, 4~6 ya chuo!
Jumla miaka 25 ya kuisaka elimu (hapo hujafeli kidogo )
Hapo bado miaka 5~10 ya kusubiri ajira!
Hapo kwa haraka haraka miaka 35 hadi 40 ndo unapokea tonge la kwanza la mshahara!

Hakika haya ni zaidi ya maigizo ya kuishi!

Kipi kifanyike?

Ingekuwa serikali (Wizara ya elimu) inasikiliza watu wa hali ya chini kabisa ngazi yetu mimi fundi umeme Samico , ningeshauri yafuatayo!
  • Miaka ya shule ya msingi iwe 4 tu!
  • Secondary iwe miaka 3
  • Chuo mwaka 1 (miezi 6 darasani na 6 site)
  • Baada ya kumaliza secondary IWE lazima kila mwafunzi akasome VETA mwaka 1,
  • Kutokea veta huko ndiko mchucho mkali wa mitihani ya kujiunga chuo iwepo, majeshi yachukulie vijana beta n.k
  • Ufaulu wa kuingia chuo kikuu kutokea veta uwe mwisho pointi 3 (AAA) tu
  • Hii inamaanisha vyuo vikuu viwe vichache lakini veta ziwe nyingi ili wanaofeli WAKAJIAJILI
  • Masomo yote yafundishwe kwa kingereza kuanzia chekechea hadi chuo! Ili Kupunguza kurudia rudia syllabus!
Hili litaleta mageuzi makubwa sana kwenye nchi yetu kwasababu!

  • Zamani watu walikuwa na vichwa vigumu sana kuliko sasa!
  • Hata kutumia kompyuta kwa mfano Mimi siku ya kwanza nilizungusha mouse hadi nyuma ya kioo (monitor)!
  • Kipindi cha zamani hata kutafta frequency za radio waliweza wachache sana.
  • Waliojaaliwa kuwa na luninga, mikanda ya video haikuwa kazi rahisi kuweka video hadi ioneshe! Kule kijijini kwetu mitambo ya sinema iliandaliwa kuanzia saa 10! Ili tuangalie kanda bongombani na yondo sister usiku! (haikuwa rahisi)
Lakini hivi Leo mtoto mdogo kabisa wa miaka mitatu anatumia laptop kama msomi;

Mtoto wa mwaka mmoja anajua kutoa keypads lock kwenye simu na kucheza gemu!

HILI NI FUMBO kubwa kwetu Mungu anatutaarifu umma kupitia uwezo wa kuelewa mambo kwa watu,

kauongeza uelewa wa mambo makusudi ili watu waelewe mambo mapema ili baadae waishi miaka michache!

Kuna uwezekano miaka ya kuishi inavyopungua hata maumbo ya miili yanapungua!

Miaka ijayo itafika kipindi watu tutakuwa na maumbo madogo kama chupa ya chai!

Tutaishi miaka michache na tutayafanya yote yanayostahili kufanywa!

Kama inzi anaishi siku saba sasa na anakamilisha yote yanayohitajika kufanywa hapa duniani! Basi na binadamu ataishi mwaka mmoja tu na kuzeeka!
Wanasayansi na wasomi wetu nashauri wakubali kubadili mitaala sasa! Hakuna kitakachoharibika!

(Kama unahoja mbadala karibu)

Haya ni mastory yangu tu Fundi umeme Samico; Tuinuane jamani kama unakazi yako ya kiufundi naomba nipigie kwa 0711756341 au instagram follow @samico_tanzania

Sinaga bei kabisa, nyumba yako ofisi yangu! Natindua na kufunga mifumo yote ya umeme
 
Hiyo selemani alikuwa na wake mia 7 lakini hakuwaoa ote siku moja! Hapo kwenye kupunguza masomo nimekuelewa kidogo
 
Back
Top Bottom