Vigezo na masharti ya kushiriki katika Stories of Change 2023

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,029
  1. Mshiriki lazima awe mwanachama wa JamiiForums, ambapo anaweza kujisajili kwa kiunganishi hiki; Register
  2. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’.
  3. Mshiriki atatakiwa kutaja jina halisi endapo ataibuka mshindi.
  4. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko ambalo linachochea mabadiliko kuhusu Uwajibikaji au Utawala bora katika nyanja mbalimbali. Andiko linaweza kuwa Habari, taarifa, maoni, uchambuzi au uchunguzi.
  5. Andiko liwe kwa lugha ya Kiswahili lenye maneno yasiyopungua 700 na yasiyozidi 1000.
  6. Andiko lisiwe limewahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote (Plagiarism). Aidha lisiwe tafsiri ya andiko lililochapishwa sehemu nyingine kwa lugha tofauti.
  7. Hakikisha unachapisha andiko lako kwenye Jukwaa la Stories of Change, ukichapisha katika majukwaa mengine halitazingatiwa.
  8. Usiweke andiko kama attachment (Word/pdf).
  9. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  10. Unaweza kuchapisha andiko Zaidi ya moja.
  11. Andiko lisiwe na sehemu ya mwendelezo, mathalani, Sehemu ya I, Sehemu ya II.
  12. Kichwa cha habari kisipungue maneno manne yanayoeleweka.
  13. Watendaji wa JamiiForums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.
Aidha

Soma SoC03 - Namna ya kuweka andiko lako ndani ya jukwaa la Stories of Change 2023

na SoC03 - Jinsi ya kujisajili kuwa mwanachama wa Jamiiforums.com
 
  1. Mshiriki lazima awe mwanachama wa JamiiForums, ambapo anaweza kujisajili kwa kiunga hiki; Register
  2. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’.
  3. Mshiriki atatakiwa kutaja jina halisi endapo ataibuka mshindi.
  4. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko ambalo linachochea mabadiliko kuhusu Uwajibikaji au Utawala bora katika nyanja mbalimbali. Andiko linaweza kuwa Habari, taarifa, maoni, uchambuzi au uchunguzi.
  5. Andiko liwe kwa lugha ya Kiswahili lenye maneno yasiyopungua 700 na yasiyozidi 1000.
  6. Andiko lisiwe limewahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote (Plagiarism). Aidha lisiwe tafsiri ya andiko lililochapishwa sehemu nyingine kwa lugha tofauti.
  7. Hakikisha unachapisha andiko lako kwenye Jukwaa la Stories of Change, ukichapisha katika majukwaa mengine halitazingatiwa.
  8. Usiweke andiko kama attachment (Word/pdf).
  9. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  10. Unaweza kuchapisha andiko Zaidi ya moja.
  11. Andiko lisiwe na sehemu ya mwendelezo, mathalani, Sehemu ya I, Sehemu ya II.
  12. Kichwa cha habari kisipungue maneno manne yanayoeleweka.
  13. Watendaji wa JamiiForums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.
Bahati njema kwa kila atakaye shiriki
 
habari nime register apo nimeambiwa nitapata ujumbe kwenye Email ndo nasubiri sijui saa ngapi
 
ok sawa
 
Mara zote mshindi mtarajiwa wa shindano la 'stories of change' huwa anafahamika.

Na mshindi huyo huwa habadiliki hata mara moja, labda kwa mtu asiye na macho ya rohoni. Sifa zake ni rahisi tu, anapaswa kukamilisha kazi ya shindano kama alivyoipokea. Na kufahamika kwa mshindi huyo ndio sababu ya kuwekezwa kwa pesa nyingi kwenye shindano hili maana hata waanzilishi wanajua faida ya shindano wao pia inawahusu.

Binafsi namfananisha mshindi huyu kama mshambuliaji hodari wa timu ya mpira. Nikiri kwamba hakuna mshindi halisi anayetangazwa kwenye shindano la 'stories of change'. Au hakuna mfungaji bora wa bao la ushindi anayepatikana kwenye michuano hii.
View attachment 2699379
Picha : mtandao

Wala sio kweli kwamba mwaka 2021, Mmari aliongoza kwa magoli! Mmari ni kiungo mkabaji tu, kufunga sio kazi yake! Alikaba vizuri na alifanikiwa kuzuia mashambulizi ya timu pinzani kama alivyoelekezwa na kocha. Mnasema mfungaji bora wa mwaka 2022 alikuwa Kulwa?! Na mnaamini kabisa?! Poleni sana! Kulwa ni golikipa tu! Kelele mlizosikia ni za yeye kuokoa penati na wala si tuzo ya mfungaji bora kama wanavyodai.

Anayefunga goli hasa ndiye mshindi. Lakini sijui kwa nini hajitangazi maana ni kawaida ya washindi kujigamba na kujigamba! Asimame mbele za kadamnasi, aseme si mnaniona?! Uwanja wote nimehaha. Mimi ni mshambuliaji bora sana. Nimefika hapa na pale na pale, lakini wapi!! Kimyaa! Kila mtu ametaharuki.
View attachment 2699381
Picha: mtandao

Tulia kwanza halafu nisikilize!

Kuna raha ya kuwa na mshambuliaji analijua goli bwana! Yeye mpe mpira halafu mengine muachie, hakuangushi. Mpira wa juu ataenda na kichwa-mchundo au 'tik-taka'. Mpira upo mita 30 ataachia kombora, kipa wao akidaka la kwanza na la pili basi la tatu lazima apishe au 'ajivunje' akapumzike nje. Wakati mwingine 'atawapunguza' mabeki mpaka utashangaa, huyu ni kijana wa mzee Nyerere huyuhuyu?! Kijana ana balaa! Baba yake angemuona, angefurahi sana.

Sio 'straika' pasi elekezi ameshapewa bado kuweka mpira kambani tu na bado anafeli. Anafeli wapi?! Amefeli au hajafeli, au hajasema kama amefaulu au amesahau au hajui! Akisema hajui itakuwa balaa maana atawavunja moyo mashabiki na wanachama wote, watasinzia wakiwa katikati ya mechi. Wakiambiwa "njoeni mtushangilie!" Wote watashangaa maana mchezo umekuwa wa saa ya ukutani yenye mishale iso-namba! Mshale ukisimama ni sawasawa na ukitembea! Mahali penye sita hakuna kitu na penye tisa pia hakuna chochote! Mchezo usio na faida au mchezo wa kutwanga maji 'kinuni'. Si ndioo?!

View attachment 2699399
Picha: mtandao

Labda nikuulize swali rafiki yangu mzuri, ni nani atakayegawa milioni 20 na asitarajie kuwa pesa hizo zitampatia manufaa?! Hakuna! Hata mapedeshee wakiwa baa watagawa pesa kwa wasanii ili watajwe wapate umashuhuri, yaani nitaje kwanza ndio ninyanyuke nikutuze. Wanasiasa watasogea na kamera nyingi wakati wa kutatua matatizo hata ya mwizi wa kuku tu, lakini wanajua wataongeza heshima yao kisiasa na kijamii. Kila mtu anafikiria faida wakati wa kufanya chochote! Naam, faida kwanza mambo mengine baadae.

Sisi sote, waanzilishi na washiriki wa 'stories of change' ni wananchi, wananchi wa kawaida kabisa. Waanzilishi ni kama kocha wa timu ya mpira wa miguu na washiriki ni mfano wa wachezaji 10 waliopo uwanjani isipokuwa 'straika' tu. Wote hawa umahiri wa kazi watakayofanya utapimwa na uhodari wa 'straika' wao kwenye kumalizia Majukumu anayopewa na kocha na wachezaji wenzake kwenye timu. 'Straika' ndiye mshindi hasa ambaye anaweza kutafsiri kazi ngumu za timu nzima kuwa matunda chanya na matamu! Hiyo ndiyo dhamana yake!

'Straika' wetu anafunga?!

Na kwasababu timu yetu ina mashabiki wengi basi kama angefunga goli hata la mkono na krosi zote alizopewa basi tungesikia makelele tu, watu mpira wanaupenda sana! Watu furaha ni kipaumbele chao, nani anapenda dhiki?!

Na kama hajafunga wakati huu, walau angefanya mahojiano na waandishi wa habari atueleze mipango yake kuhusu timu yetu au tuwahi kumchukua Kylian Mbappe kabla Real madrid hawajamnyakua.

Kocha wa timu yetu sio Pep Guardiola lakini mipango anaijua! Kila mkakati uliopangwa uko sawa na wachezaji wengine wote wako tayari kuufanyia kazi na wamefanya kazi kwa miaka miwili kwa moyo, mfungaji wetu walau atuambie maandalizi yake ya kuisaidia timu yetu yamefikia wapi. Watu wamechachamaa huko nje, watu wanataka ushindi. Msimu wa tatu huu makombe hatuyaoni! We 'straika' wewe!
View attachment 2699401
Pep Guardiola (picha mtandao)

Furaha ya timu yetu kila mmoja inamhusu, kuanzia mashabiki mpaka wanachama, na ndio maana wawekezaji wameweka takribani milioni 20 japo na wao hofu yao ni 'straika'. Mashabiki na wanachama wamejiandikisha vya kutosha kuisapoti timu yao na mwaka huu wanasema lazima watembee kifua mbele! Lakini na wao pia hofu yao ni nani atatupatia goli la ushindi?! Maana straika wetu ni kama ana kigugumizi miguuni! Wakati mwingine hata umpe penati nne kwenye mechi moja zote atapaisha!! Ilimradi tu atuue na presha!

Mshindi wa andiko lenye tija ni kama kiungo namba sita, kazi yake ngumu na nzuri ni lazima ikamilishwe vema na 'straika' mahiri. Mshindi yeyote wa andiko anayepatikana ni kama Khalid Aucho tu, kazi yake ngumu ni lazima ikamilishwe vizuri na Fiston Mayele.
View attachment 2699402
Fiston Mayele (picha-mtandao)

Shughuli-punda ya Muzamiru Yassin yafaa nini kama Jean Baleke hafungi?! Serikali ndiye hasa mshindi na 'straika' anayepangwa na mkamilishaji wa kazi ngumu na nzuri za vijana hawa, na hii ndio maana hai ya kuanzishwa kwa shindano hili.
View attachment 2699405
Jean Baleke (picha-mtandao)

Hivi 'straika' unajua kama kwenye mechi mbili za mwisho pasi umepewa nyingi? funga hata goli moja sasa! Pasi za chini umepewa za kutosha, krosi za kutosha, penati tulipata pia halafu ukapaisha sijui?! Mimi sijui na sina uhakika! Mpira wa kusikiliza kwenye redio si unaujua?! Au kama umefunga hata bao moja useme maana huku pia mtandao shida. Ukisikiliza redio mara usikie mara usisikie, ilimradi taabu tu. Na hata watu waliosikiliza kipindi cha michezo karibuni hakuna aliyesema kwamba straika wetu ana takwimu zozote. Eti wanasema hauna hata goli la kusingiziwa. Njoo uwaambie kama umefunga au utaanza kufunga mwaka huu.

Na pasi zote utakazopewa safari hii usizifanyie mzaha. Usifanye pasi ziwe sawasawa na hakuna, zikapatwa na vumbi kama mafaili ya miaka ya 2000 yaliyopo kwenye masijara za ofisi za umma. Hata kwa taabu na nafasi ndogo ndani ya boksi jitahidi uzifanyie kazi! Straika jikunje ufanye mambo!

Msimu huu ufanye kweli tuchukue kombe kabla ligi haijaisha! Kila la heri 'straika'.
Tupieni jicho hapa
 
Back
Top Bottom