Uzinduzi wa awamu ya 3 wa Shindano la Stories of Change

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,025
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UZINDUZI WA AWAMU YA 3 YA SHINDANO LA “STORIES OF CHANGE”

Ndugu Wanahabari,

JamiiForums (JF) ni asasi ya Kiraia iliyosajiliwa kufanya uchechemuzi wa Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora. Vilevile, JF inaratibu jukwaa la JamiiForums.com ambalo ni maarufu duniani kwa maudhui ya Kiswahili na tovuti namba moja nchini yenye rekodi ya kufikia watu zaidi ya Milioni 3 kila siku.

Kwa muda mrefu, JamiiForums.com imechangia kuleta mabadiliko katika uchakataji taarifa nchini. Wananchi Jukwaani humo hushiriki kuripoti Matukio kwa haraka na kuanzisha mijadala yenye staha.

Katika mpango mkakati wake wa miaka 5 (2020-2024), JF ilidhamiria kuendesha shindano lenye lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki katika kuongeza ubora wa maudhui ya Kiswahili mtandaoni yenye kuchochea mabadiliko kwa kizazi cha sasa na cha baadae.

Awamu ya kwanza ya shindano hili ilifanyika kuanzia Julai hadi Oktoba 2021 ambapo jumla ya wananchi 1,509 walishiriki na kuandika jumla ya machapisho 1,536 huku 936 yakipitishwa kuingia kwenye shindano. Washindi watano wa kwanza walikabidhiwa zawadi mbalimbali katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Oktoba 2021.

Awamu ya pili ya shindano hili ilifanyika kuanzia Julai mpaka Septemba 2022 ambapo wananchi 1,820 walishiriki na kuandika jumla ya machapisho 2,073 huku 1,462 yakipitishwa kuingia kwenye shindano. Washindi bora kumi walikabidhiwa zawadi mbalimbali katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Novemba 2022.

Miongoni mwa maudhui yaliyowasilishwa yamechangia maboresho katika mifumo ya utoaji huduma Serikalini huku baadhi ya taasisi zikipokea mapendekezo na kuahidi kuyafanyia kazi.

Awamu ya Tatu (2023)
Baada ya kufanikiwa kufanya shindano la Stories of Change mwaka 2021 na 2022, JF imedhamiria kufanya shindano hili mwaka 2023, litakalofanyika kwa siku 90 kuanzia tarehe 01 mwezi Mei. Awamu hii, wananchi wataandika maudhui mbalimbali yanayolenga kuchochea mabadiliko chanya na kupelekea kuwepo kwa Uwajibikaji au Utawala Bora.

Katika shindano la mwaka huu, JF itashirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza (SAUT) na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kutambua mchango wao katika upashanaji Habari ikiwa ni Pamoja na kushiriki katika kuwandaa wananchi/vijana waliosomea taaluma ya habari, pia katika kufanya tafiti mbalimbali zinazoleta mabadiliko nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:
  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko na kwenye nyanja zote za Utawala Bora (ikiwemo Uwajibikaji).
  • Andiko liwe kwa lugha ya Kiswahili lenye maneno kati ya 700 na 1,000.
  • Matumizi ya picha, vielelezo na video yanaruhusiwa ili kuongezea uzito wa wasilisho. Ikiwa picha/video zilizotumika si za mshiriki, atatakiwa kutaja chanzo.
  • Machapisho yanatakiwa kuwa halisi yasizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Ubwakuzi (Plagiarism) hautaruhusiwa.
Jinsi ya Kushiriki
  • Maandiko yawasilishwe ndani ya siku 90 kuanzia Mei 01, 2023 kwenye jukwaa la “Stories of Change 2023".
  • Ili kushiriki, LAZIMA mtu awe mwanachama aliyejisajili JamiiForums.com ili kuchapisha maudhui yake kwenye jukwaa la shindano la Stories of Change. Ikiwa sio mwanachama, anapaswa kujiandikisha kwa kufuata kiungo hiki Register
  • Washiriki wanaweza kutumia Majina yao ya Kuigiza (pseudonyms) katika shindano hili, wakijua kuwa mshindi anapaswa kuwa tayari kutoa utambulisho wake halisi kwa madhumuni ya kukabidhiwa zawadi pale atakaposhinda.
Upatikanaji wa washindi

Jopo la majaji linaloundwa na wataalamu 5 wenye mchango mkubwa katika masuala ya uwajibikaji na utawala bora nchini, litaamua washindi kulingana na vigezo vilivyowekwa. Kura za majaji zitabeba 60% ya ushindi huku kura za wananchi jukwaani zikibeba 40% ya ushindi.

Washindi watapewa taarifa kuhusu ushindi na akaunti rasmi ya JamiiForums kupitia ujumbe wa faragha katika akaunti zao walizotumia kushiriki na kisha kutangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums "Stories of Change" na kurasa za JF katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.

JF inawaalika wananchi wote wenye miaka 18 na kuendelea kushiriki katika Shindano hili, ili kutimiza haki yao ya msingi ya kujieleza na kuhamasisha Serikali kutekeleza wajibu wake wa utoaji huduma bora kwa wananchi.
AA8A8778.jpg

Soma hapa vigezo na masharti SoC03 - Vigezo na masharti ya kushiriki katika Stories of Change 2023
 
Nilichofurahi ni kuona Chuo Kikuu changu Bora na Kilichonipika vyema Kiuweledi na Nikatukuka Kitaaluma na Kiakili cha Saint Augustine University of Tanzania ( SAUT Mwanza ) kwa Fani ya Mawasiliano ya Umma na Uandishi wa Habari kimehusishwa Kikamilifu.

Nakipenda Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza " We Build the City of God " hadi nataka hata Kukufuru. Kimenijenga hadi Watu wenye Masters na Doctorates zao Wananiogopa Kiakili na Kifikra wakati GENTAMYCINE ninamiliki Degree yangu tu ya mwaka 2009.

Popote mlipo Wakufunzi na Wahadhiri wangu wote wa SAUT Mwanza ( wale mlionifundisha kati ya mwaka 2006 - 2009 ) na mlioendelea Kufundisha na mnaofundisha hadi sasa GENTAMYCINE nasema Asanteni sana na mno kwa Taaluma yenu Tukuka Kwangu na nikiombea Mafanikio mema Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza na Wanafunzi wote walioko Waelimike vyema ili waje kuwa Faida ya Kimaendeleo kwa Taifa letu la Tanzania, Bara la Afrika na duniani kote.

Mbarikiwe SAUT Mwanza. Nawapenda.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UZINDUZI WA AWAMU YA 3 YA SHINDANO LA “STORIES OF CHANGE”

Ndugu Wanahabari,

JamiiForums (JF) ni asasi ya Kiraia iliyosajiliwa kufanya uchechemuzi wa Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora. Vilevile, JF inaratibu jukwaa la JamiiForums.com ambalo ni maarufu duniani kwa maudhui ya Kiswahili na tovuti namba moja nchini yenye rekodi ya kufikia watu zaidi ya Milioni 3 kila siku.

Kwa muda mrefu, JamiiForums.com imechangia kuleta mabadiliko katika uchakataji taarifa nchini. Wananchi Jukwaani humo hushiriki kuripoti Matukio kwa haraka na kuanzisha mijadala yenye staha.

Katika mpango mkakati wake wa miaka 5 (2020-2024), JF ilidhamiria kuendesha shindano lenye lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki katika kuongeza ubora wa maudhui ya Kiswahili mtandaoni yenye kuchochea mabadiliko kwa kizazi cha sasa na cha baadae.

Awamu ya kwanza ya shindano hili ilifanyika kuanzia Julai hadi Oktoba 2021 ambapo jumla ya wananchi 1,509 walishiriki na kuandika jumla ya machapisho 1,536 huku 936 yakipitishwa kuingia kwenye shindano. Washindi watano wa kwanza walikabidhiwa zawadi mbalimbali katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Oktoba 2021.

Awamu ya pili ya shindano hili ilifanyika kuanzia Julai mpaka Septemba 2022 ambapo wananchi 1,820 walishiriki na kuandika jumla ya machapisho 2,073 huku 1,462 yakipitishwa kuingia kwenye shindano. Washindi bora kumi walikabidhiwa zawadi mbalimbali katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Novemba 2022.

Miongoni mwa maudhui yaliyowasilishwa yamechangia maboresho katika mifumo ya utoaji huduma Serikalini huku baadhi ya taasisi zikipokea mapendekezo na kuahidi kuyafanyia kazi.

Awamu ya Tatu (2023)
Baada ya kufanikiwa kufanya shindano la Stories of Change mwaka 2021 na 2022, JF imedhamiria kufanya shindano hili mwaka 2023, litakalofanyika kwa siku 90 kuanzia tarehe 01 mwezi Mei. Awamu hii, wananchi wataandika maudhui mbalimbali yanayolenga kuchochea mabadiliko chanya na kupelekea kuwepo kwa Uwajibikaji au Utawala Bora.

Katika shindano la mwaka huu, JF itashirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza (SAUT) na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kutambua mchango wao katika upashanaji Habari ikiwa ni Pamoja na kushiriki katika kuwandaa wananchi/vijana waliosomea taaluma ya habari, pia katika kufanya tafiti mbalimbali zinazoleta mabadiliko nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:
  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko na kwenye nyanja zote za Utawala Bora (ikiwemo Uwajibikaji).
  • Andiko liwe kwa lugha ya Kiswahili lenye maneno kati ya 700 na 1,000.
  • Matumizi ya picha, vielelezo na video yanaruhusiwa ili kuongezea uzito wa wasilisho. Ikiwa picha/video zilizotumika si za mshiriki, atatakiwa kutaja chanzo.
  • Machapisho yanatakiwa kuwa halisi yasizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Ubwakuzi (Plagiarism) hautaruhusiwa.
Jinsi ya Kushiriki
  • Maandiko yawasilishwe ndani ya siku 90 kuanzia Mei 01, 2023 kwenye jukwaa la “Stories of Change 2023".
  • Ili kushiriki, LAZIMA mtu awe mwanachama aliyejisajili JamiiForums.com ili kuchapisha maudhui yake kwenye jukwaa la shindano la Stories of Change. Ikiwa sio mwanachama, anapaswa kujiandikisha kwa kufuata kiungo hiki https://jamii.app/Register
  • Washiriki wanaweza kutumia Majina yao ya Kuigiza (pseudonyms) katika shindano hili, wakijua kuwa mshindi anapaswa kuwa tayari kutoa utambulisho wake halisi kwa madhumuni ya kukabidhiwa zawadi pale atakaposhinda.
Upatikanaji wa washindi

Jopo la majaji linaloundwa na wataalamu 5 wenye mchango mkubwa katika masuala ya uwajibikaji na utawala bora nchini, litaamua washindi kulingana na vigezo vilivyowekwa. Kura za majaji zitabeba 60% ya ushindi huku kura za wananchi jukwaani zikibeba 40% ya ushindi.

Washindi watapewa taarifa kuhusu ushindi na akaunti rasmi ya JamiiForums kupitia ujumbe wa faragha katika akaunti zao walizotumia kushiriki na kisha kutangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums "Stories of Change" na kurasa za JF katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.

JF inawaalika wananchi wote wenye miaka 18 na kuendelea kushiriki katika Shindano hili, ili kutimiza haki yao ya msingi ya kujieleza na kuhamasisha Serikali kutekeleza wajibu wake wa utoaji huduma bora kwa wananchi.
View attachment 2598157

Soma hapa vigezo na masharti SoC03 - Vigezo na masharti ya kushiriki katika Stories of Change 2023
Mwaka huu idadi ya washindi na kiwango cha zawadi hakijawekwa wazi!
 
Back
Top Bottom