SoC03 Uwajibikaji kwenye kilimo Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Jiger

Member
Jun 8, 2023
26
12
Kilimo ni sekta muhimu yenye kuleta mapinduzi makubwa kwenye nchi yetu mapinduzi hayo kama VIWANDA, BIASHARA ZA NDANI NA NJEE, ELIMU BORA, UJUZI, NA AFYA KWA JAMII.

Uwajibikaji ungekuwa kama ifuatavyo elimu ya kilimo ingeanza kufundishwa kuanzia shule za msingi na sekondari na ingekuwa lazima kila mwanafunzi au kikundi cha wanafunzi wawe na sehemu yao ya eneo la shamba kwa ajili ya vitendo pamoja na kuzalisha mazao hii ingemtengeneza mwanafunzi kujua nini maana ya ujasiliamali pamaja na biashara kwakuwa anatakuwa anazalisha ubora wa bidhaa pamoja na biashara.

Pia serikali ingejipunguzia mzigo wa kuwalisha wanafunzi na kufanya kila shule ilzalishe mazao yao ya chakula pamoja na biashara apo vilevile kila shule inge ajili AFISA KILIMO, WAPISHI, WATUNZA STORE, WAHASIBU, AFISA MASOKO NA WALINZI kwa maana hiyo fupi shule nyingi zingeweza kuzalisha kwa ajili ya chakula na biashara na kuwalipa mishahara wafanya kazi wao walioajiliwa na shule bila serikali kutoa pesa serikali hapa ingekuwa kama mkaguzi na kufanya ushindani kwa kila shule kwenye bidhaa zao pia bidhaa hizo zitakazozalishwa na shule nyingi nchini zizingatie mazao makuu ya mkoa fulani mfano MBEYA wanazalisha sana mchele na SINGIDA wanazalisha sana alizeti yapewe kipao mbele kulingana na mkoa husika japo mazao mengine yatazalishwa.

Kama itafanyika hivi watanzania wengi wanaojua kilimo kwa ajili ya wazee kijiji, watu wa hali ya chini, watu wasio ajiliwa, wanaodhani kilimo ni adhabu itolewayo magereza, mashuleni basi watokwe na zana iyo ya upotoshaji kwenye kilimo.

Kilimo ni uwajibikaji wenye kuinua uchumi wenye kuzalisha marighafi nyingi na bidhaa zenye kuipatia nchi faida na kuinua uchumi. Kilimo ni uti wa mgongo wa TANZANIA basi tufanye mgongo wetu uzalishe na ubebe uchumi wetu.
 
Back
Top Bottom