Hivi ni kweli kuwa ukomo wa kurefuka na kunenepa kwa uume ni miaka 20?
Yaani mtu mwanaume mwenye umri wa miaka 25 au 30, kamwe hawezi ku experience ongezeko la ukubwa wa uume wake?
Kwa maana nyingine, ukubwa wa uume wa mwanaume akiwa na miaka 20, ndio atakaokuwa nao akifikisha miaka 35?
Yaani mtu mwanaume mwenye umri wa miaka 25 au 30, kamwe hawezi ku experience ongezeko la ukubwa wa uume wake?
Kwa maana nyingine, ukubwa wa uume wa mwanaume akiwa na miaka 20, ndio atakaokuwa nao akifikisha miaka 35?
- Tunachokijua
- Uume ni kiungo kinachofanya kazi kuu mbili, kutoa takamwili za mkojo pamoja na kushiriki tendo la ndoa. Muundo wake wa anatomia huruhusu kufanyika kwa kazi zote hizi mbili pasipo kuingiliana.
Kwa mujibu wa taasisi ya Weill Cornell Medicine, urefu wa uume hutofautiana miongoni mwa wanaume kulingana na asili yao. Vipimo vya kawaida huwa kama ifuatavyo;
- Urefu wa kawaida wa uume usiosimama ni wastani nchi 3.4-3.7 (8.6-9.3 cm)
- Urefu wa kawaida wa uume uliosimama ni wastani wa nchi 5.1-5.7 (12.9-14.5cm)
Ukuaji wa kasi wa uume hutokea wakati wa kubalehe kwenye wastani wa umri wa miaka 12 au mapema zaidi. Ukuaji huu huendelea hadi kufikia umri wa miaka ya mapema ya 20 ya mwanaume.
Kubalehe kwa kawaida huanza kati ya umri wa miaka 9 na 14 na hudumu hadi miaka mitano au zaidi, kulingana na umri ambao huanza. Katika umri huu, mambo yafuatayo hutokea kwa wavulana:
- Kuongezeka kwa ukubwa wa korodani
- Kuongezeka kwa ukubwa (urefu) wa uume
- Kuota nywele nywele sehemu za siri na kwapani
- Kumwaga shahawa
- Sauti kuwa nzito
Aidha, baada ya kuzungumza pia na wataalam wa afya ya binadamu, JamiiForums imebaini kwamba ukuaji wa uume husimama baada ya kumaliza umri wa balehe, ambao hutofautiana miongoni mwa vijana.
Kwa mujibu wa tafiti, balehe ya vijana wengi hukoma wakiwa na miaka 16 na wengine huendelea hadi wafikiapo umri wa miaka 20.
Mbinu mbadala za kukuza uume
Kumekuwepo na matangazo ya bidhaa nyingi zinazodai kuwa na uwezo wa kuongeza ukubwa (urefu) wa uume. Aidha, baadhi ya mazoezi hudaiwa pia kuwa na uwezo wa kuongeza ukubwa wa sehemu hizo.
Kwa mujibu wa Urology Care Foundation, mbinu hizi hazina ufanisi mkubwa. Hata hivyo, matumizi ya vifaa maalum yametajwa na baadhi ya tafiti kuwa na uwezo wa kuongeza urefu kwa kiasi fulani na sio unene.