UTANGULIZI
Ni ukweli usiopingika kwamba, siku hizi majanga ya kuporomoka kwa maadili katika jamii yanaongezeka tena kwa kasi sana. Miongoni mwa majanga haya ni pamoja na Ushoga, Usagaji, kuvunjika kwa ndoa na mengine mengi.
Majanga haya ni mambo mabaya sana mblele za Mwenyezi Mungu na hata katika jamii zetu. Pia tunaona kwamba majanga haya yanaongezeka kwa kasi sana na lengo kubwa ni kutengeneza kizazi cha ovyo kuanzia kwa Watoto wadogo ili waanze kujifunza mambo ya ovyo mapema na wakiwa watu wazima waone kuwa ni mambo ya kawaida.
Kwa mfano: Kwa utafiti mdogo niliofanya mimi mwenyewe, nilibaini kuwa, baadhi ya wanawake wanaona talaka ni jambo la kawaida sana na hawaoni shida kuingia kwenye ndoa na kutoka muda wowote. Wamesahau kuwa, kuvunja ndoa ni kitu kibaya na hatari kwa Familiya na Jamii kwa ujumla. Hii ikapelekea nikumbuke maneno haya....
"Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe."
Hakika mwanamke ana jukumu kubwa sana la kulinda na kujenga nyumba yake, kuanzia kwa watoto wake, mume wake na wote walio katika nyumba yake.
Siku hizi akina mama wengi wametoka katika MSINGI huu wa kujenga nyumba zao na kuanza kuzibomoa kwa tabia na mienendo yao mibovu. Wengi wamekuwa na dharau kwakuwa wana elimu, pesa au vyeo kuzidi waume wao. Wengine wamekuwa bize sana kuliko waume zao na kukosa kabisa muda hata kidogo wa kukaa na watoto ili kuwafundisha maadili mema.
MFANO:
Hata kama mke una mali nyingi kuzi mume, hata kama una fedha kuzidi mume, hata kama una elimu kuzidi mume, hata kama una vyeo kuzidi mume, tambua wewe ni mwanamke unapaswa kumpa mwanaume kile anacho stahili na kutoa muda wako katika kulea ndoa au familiya yako.
Pia, mwamke akumbuke kuwa ana jukumu kubwa la kuwa mlezi mkuu wa Familiya yake ili kuhakikisha anatengeneza kizazi bora.
Siku hizi baadhi ya wanawake hawapendi tena kazi hii ya kulea watoto badala yake hutumia muda mwingi sana katika kazi zinazowaweka nje ya nyumba zao kuanzia asubuhi hadi usiku.
Hali hii husababisha watoto wadogo kulelewa na wajakazi wa ndani pamoja na shule wanazosoma. Mbali zaidi.. baadhi wamethubutu kupeleka hadi watoto wenye mwaka mmoja wakae shuleni ili wao waendelee na kazi zao. Matokeo yake mtoto hapati tena malezi bora ya mama yake bali anapata malezi machafu na kujifunza tabia chafu pale anapolelewa na watu wenye nia mbaya.
HITIMISHO
Ingawa malezi ni jukumu la wazazi wote yaani baba na mama, ila akina mama mnajukumu kubwa la kuhakikisha watoto wenu wanapata malezi bora. Fanyeni kazi ila kumbukeni nyumba inajengwa na kubomolewa na akina mama.
Akina mama rudini katika misingi mizuri ya familiya ya kulea ndoa zenu na watoto wenu ili kupunguza mmomonyoko wa maadlili na talaka zisizo za lazima katika jamii.
NB: Akina baba pia tambueni ninyi ni vichwa vya familiya, hivyo wajibikeni kikamilifu katika kuhudumia familiya na kufatilia mienendo ya watoto wenu.
Asante msomaji kwa kusoma hadi mwisho wa chapisho hili. Tafadhari bonyeza Vote hapo chini kama umependa chapisho.

- Mwanamke hakumbuki siku aliyopika chakula cha Mume wake.
- Mwanamke hakumbuki lini kafua nguo za Mume wake hata mara moja kwa wiki.
- Baadhi hawakumbuki lini wametandika vitanda wanavyolala na waume zao
Hata kama mke una mali nyingi kuzi mume, hata kama una fedha kuzidi mume, hata kama una elimu kuzidi mume, hata kama una vyeo kuzidi mume, tambua wewe ni mwanamke unapaswa kumpa mwanaume kile anacho stahili na kutoa muda wako katika kulea ndoa au familiya yako.
Pia, mwamke akumbuke kuwa ana jukumu kubwa la kuwa mlezi mkuu wa Familiya yake ili kuhakikisha anatengeneza kizazi bora.
Siku hizi baadhi ya wanawake hawapendi tena kazi hii ya kulea watoto badala yake hutumia muda mwingi sana katika kazi zinazowaweka nje ya nyumba zao kuanzia asubuhi hadi usiku.
Hali hii husababisha watoto wadogo kulelewa na wajakazi wa ndani pamoja na shule wanazosoma. Mbali zaidi.. baadhi wamethubutu kupeleka hadi watoto wenye mwaka mmoja wakae shuleni ili wao waendelee na kazi zao. Matokeo yake mtoto hapati tena malezi bora ya mama yake bali anapata malezi machafu na kujifunza tabia chafu pale anapolelewa na watu wenye nia mbaya.
- Mtoto anamwona mama asubuhi hadi asubuhi inayofuata
- Mtoto hakumbuki lini amepewa mafundisho ya kidini na mama yake.
- Mama hakumbuki lini amesikiliza changamoto za mtoto wake.