Unavyotafuta gari ya kununua, RANGI uwa unaipa kipaumbele au kanyaga twende?

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,903
52,551
Wakuu, kwema.

Kwa wale ambao wamewahi kununua gari, kwa kuagiza, kwa mtu au showroom, hivi rangi ya gari uwa unaiweka katika options zako za muhimu au?

Kwa upande wangu, rangi ya gari nilikua naichukulia poa. Nikakutana na Runx nyeusi, nikanunua fresh.

Shida ikaja, AC kuna kipindi ilizingua kidogo. Kwa joto ili la Dar, nilikua naiva. Yaani kukaa ndani ni kero, labda ukiwa kwenye motion hafu ukashusha vioo ila kwenye foleni kidogo tu joto ndani ova tanuli.

Pia rangi nyeusi (ilikua black metallic ) kuitunza kazi sana. Inavutia sana sana sana machoni dakika 15 tu tokea itoke kuoshwa au polish. Baada ya hapo, sio vumbi sio tope sekunde mbili tu vishanasa. Hii ilinitesa. Unless uwe na access ya kuosha kila siku au mara 3 kwa week.

Pia rangi nyeusi nyepesi kuonesha mikwaruzo na michubuko ata iwe midogo, ukipata rangi inaonekana na rangi yake gharama kidogo.

Nina bad experience na rangi nyeusi na sidhani kama nitakuja nunua tena gari jeusi. Sahivi ni pearl white nikishindwa nitatafuta silver au grey.

Sisemi kwamba nyeusi ni mbaya, ila mimi sina experience nayo nzuri, labda kwakua Runx ilizingua AC ndio maana.
 
Japo sina gari ila ndio nalitafuta, ila huwezi amini sijapay attention na rangi kwenye gari zote nimeletewa.
Mimi ni engine na body tu.
 
Rangi haina uzito sana kama gari ni nzuri na imetunzwa maana unaweza kuibadili ikishafika bongo.
 
Kwa mazingira ya DAR gari nyeusi sio rafiki sana, rangi nyeusi ukipita kwenye njia yenye majani utatamani upige tena rangi maana Ile mikwaruzo yake itakunyima Raha na roho huwa inauma mno..
Gari yangu rangi ya maroon lkn huwa najitahidi Sana kupaki sehemu zenye kivuli Hadi jioni.

Repainting Kwa gari nyeusi huwa inakaa Kwa mwaka mmoja baada ya hapo inaanza kuvimba na kubanduka tena rangi
 
Japo sina gari ila ndio nalitafuta, ila huwezi amini sijapay attention na rangi kwenye gari zote nimeletewa.
Mimi ni engine na body tu.
Okay kwakua upo kwenye kutafuta, basi vya muhimu sana sana:
1. Engine
Hapa kuna muonekano wa engine na mlio. Sasa ukienda kuitest gari, USIENDE WAKATI GARI IMETOKA KUTUMIKA (WARM ENGINE). Wanashauri nenda muda engine ilikua OFF angalau kwa masaa 10 zaidi, sana sana Asubuhi na mapema. Mfano imepark. Utafaidika kuona kama chini imeacha leakage na pia cold start inaonesha matatizo. Engine ikiwa warm kuiwasha haisuisui.

2. Endesha mwenyewe
Mbali na fundi kuikagua itabidi uiendeshe mwenyewe. Kuendesha usiendeshe eti dk 5 au 10. Endesha ata dk 30 if possible weka ata mafuta ya elfu 10 endesha.

Endesha kwenye lami, rough road, mlima mkali na highway.

Lami utaona jinsi gari linavyotulia kwenye smooth road.
Rough road tutaona suspension zinavyoitika kwenye kologesheni.
Highway utaangalia jinsi gari kinavyo handle above 60kph
Mlimani tutaona gari linavyobadirisha gear automatically, smooth au rough?

3. Legal Documents
Umiliki wa gari sio tu gari, Pamoja na documents zote za muhimu. Pia angalia chassis number ya kwenye kadi na gari.

4. Ajali & Modifications
Gari ukiona imefanyiwa modifications nyingi sana, piga chini. Na kama limefanyiwa ukarabati sana piga chini.
 
Kwa mazingira ya DAR gari nyeusi sio rafiki sana, rangi nyeusi ukipita kwenye njia yenye majani utatamani upige tena rangi maana Ile mikwaruzo yake itakunyima Raha na roho huwa inauma mno..
Gari yangu rangi ya maroon lkn huwa najitahidi Sana kupaki sehemu zenye kivuli Hadi jioni.

Repainting Kwa gari nyeusi huwa inakaa Kwa mwaka mmoja baada ya hapo inaanza kuvimba na kubanduka tena rangi
Aisee, story of my life.
 
Okay kwakua upo kwenye kutafuta, basi vya muhimu sana sana:
1. Engine
Hapa kuna muonekano wa engine na mlio. Sasa ukienda kuitest gari, USIENDE WAKATI GARI IMETOKA KUTUMIKA (WARM ENGINE). Wanashauri nenda muda engine ilikua OFF angalau kwa masaa 10 zaidi, sana sana Asubuhi na mapema. Mfano imepark. Utafaidika kuona kama chini imeacha leakage na pia cold start inaonesha matatizo. Engine ikiwa warm kuiwasha haisuisui.

2. Endesha mwenyewe
Mbali na fundi kuikagua itabidi uiendeshe mwenyewe. Kuendesha usiendeshe eti dk 5 au 10. Endesha ata dk 30 if possible weka ata mafuta ya elfu 10 endesha.

Endesha kwenye lami, rough road, mlima mkali na highway.

Lami utaona jinsi gari linavyotulia kwenye smooth road.
Rough road tutaona suspension zinavyoitika kwenye kologesheni.
Highway utaangalia jinsi gari kinavyo handle above 60kph
Mlimani tutaona gari linavyobadirisha gear automatically, smooth au rough?

3. Legal Documents
Umiliki wa gari sio tu gari, Pamoja na documents zote za muhimu. Pia angalia chassis number ya kwenye kadi na gari.

4. Ajali & Modifications
Gari ukiona imefanyiwa modifications nyingi sana, piga chini. Na kama limefanyiwa ukarabati sana piga chini.
Nimefaidika sana kwenye haya maelezo, Nitajatibu kua nayo hata at least siku nzima.
No. Ya chasis ya gari inawekwa kwenye chasis au?
 
Okay kwakua upo kwenye kutafuta, basi vya muhimu sana sana:
1. Engine
Hapa kuna muonekano wa engine na mlio. Sasa ukienda kuitest gari, USIENDE WAKATI GARI IMETOKA KUTUMIKA (WARM ENGINE). Wanashauri nenda muda engine ilikua OFF angalau kwa masaa 10 zaidi, sana sana Asubuhi na mapema. Mfano imepark. Utafaidika kuona kama chini imeacha leakage na pia cold start inaonesha matatizo. Engine ikiwa warm kuiwasha haisuisui.

2. Endesha mwenyewe
Mbali na fundi kuikagua itabidi uiendeshe mwenyewe. Kuendesha usiendeshe eti dk 5 au 10. Endesha ata dk 30 if possible weka ata mafuta ya elfu 10 endesha.

Endesha kwenye lami, rough road, mlima mkali na highway.

Lami utaona jinsi gari linavyotulia kwenye smooth road.
Rough road tutaona suspension zinavyoitika kwenye kologesheni.
Highway utaangalia jinsi gari kinavyo handle above 60kph
Mlimani tutaona gari linavyobadirisha gear automatically, smooth au rough?

3. Legal Documents
Umiliki wa gari sio tu gari, Pamoja na documents zote za muhimu. Pia angalia chassis number ya kwenye kadi na gari.

4. Ajali & Modifications
Gari ukiona imefanyiwa modifications nyingi sana, piga chini. Na kama limefanyiwa ukarabati sana piga chini.
Engine nzuri ukiachana na beams 200, 5A zingine ni zipi?
 
Back
Top Bottom