Matatizo ya injini na gari ambayo hutakiwi kupuuzia, Jibu la shida ya Dualis

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
619
Unaweza usielewe kichwa cha habari lakini pindi utakaposoma mpaka mwisho utaelewa hivyo nakusihi usome mpaka mwisho.

Katika chombo chochote kinachoitwa cha moto injini ni Moyo wa chombo hicho, Hakika hakutakuwa na Gari, Pikipiki ama Jenereta kama hakuna Injini katika chombo husika. Binafi kama chombo hakina Injini kwangu naona hiyo ni Housing tu au kava na kama ni hivo basi yatakiwa kuwa makini sana na injini ya gari lako kwani ndiyo moyo wa chombo chako cha usafiri na ndiyo maana huwa tunapouliza gari swali la kwanza ni ukubwa, Uwezo na gharama zake za uendeshaji kama vile unywaji wa mafuta na hapa ndipo linapokuja swali la gari yako ina Cc ngapi? Leo nitaelezea matatizo ambayo hupaswi kuyapuuzia pindi unapohisi au kuyaona kwenye injini ya gari lako kwani kupuuzia utapelekea marekebisho au ununue injini mpya kabisa jambo ambalo ni gharama.

1. KIWANGO CHA JOTO KUZIDI KWENYE INJINI YA GARI LAKO

Kila gari lina geji maalum ya kupima joto kwenye injini ya gari kuonesha umuhimu wake kwani madhara huwa ni makubwa endapo joto la injini litazidi ubaya ni kwamba madereva wengi huwa wanajisahau sana kuangalia mwenendo wa joto la injini yeye akishaangalia mbele amemaliza na ndiyo unakuta mtu anaendesha gari hadi lianze kutoa moshi kwenye boneti ndiyo anaangalia kiwango cha joto hakika hii ni hatari sanahivo unatakiwa kuwa makini na kuangalia kiwango cha joto cha injini na kinapozidi tafuta sehemu nzuri egesha gari lako subiri lipoe ufungue uangalie mfumo wa kupooza injini yani rejeta kama ina maji na pia angalia kama feni ya kupooza rejeta endapo inafanya kazi yani kuzunguka.

2. INJINI KUZIMA KATIKATI YA MWENDO

Hapa namaanisha gari inazima wakati upo barabarani na saa ingine kwenye mwendo sasa katika hili kuna mtu unakuta anawasha anaendelea na safari anachukulia kawaida, Tatizo hili huenda linasababishwa na labda gari kumiss kutokana na plug kuchoka ama tatizo katika mfumo wa mafuta au filter ya mafuta ya gari lako au pia likawa linasababishwa na sababu ingineyo lakini si ya kupuuzia kwani inaweza kukusababishia ajali mfano inakuaje endapo gari inazima ukiwa unapita gari jingine au upo kwenye mteremko mkali? hakika waweza sababisha kukatokea ajali na ikawa na madhara kwako au watumiaji wengine wa barabara.

3. KELELE YOYOTE AMBAYO SI YA KAWAIDA KWENYE INJINI

Nimetangulia kusema kelele si ya kawaida kwasababu mfumo wenyewe wa injini ni wa kelele lakini kuna kelele ambazo si za kawaida ambazo zinaweza kujitokeza ambazo zinaweza kuwa ni kutokana na kuchoka kwa mikanda {Belt} zinazokuwa zimeungana na engine au labda stata ya gari lako lakini pia inaweza kuwa tatizo jingine ambalo ni kubwa zaidi.

4. MATATIZO YANAYOHUSIANA NA OIL YA INJINI

Sote tunajua kwamba oil ni kitu muhimu sana kwenye injini ya gari na katika kila gari pale mbele kuna taa ya oil ambayo inawaka kama kutakuwa na shida yoyote ile inayohusiana na oil pressure ya gari lako. Hutokea pale tunapoendesha magari yetu kugonga sample chini na kusababisha oil kumwagika taratibu na kupelekea kupungua hatimae kuisha kabisa lakini yote hayatatokea bila ya taa ya oil kuwaka kwenye dashboard ya gari lako hivo basi hutakiwi kupuuzia haraka sana egesha gari lako pembeni fuatilia sababu ya taa hiyo kuwaka kama oil iko chini ongeza alafu upeleke kwa mtaalamu.Kumbuka upungufu wa Oil kwenye Injini yako huweza kukugharimu kununua Injini mpya kwani huweza sababisha kunoki kwa Injini na sababu ikawa ni moja tu ulipuuzia dalili.


5. MAJI KWENYE INJINI YA GARI HASA KIPINDI HIKI CHA MVUA

Hapa nitaongelea kwa wale wenye mazoea ya kuendesha gari kupita kwenye maji mengi kama vile mabwawa yetu ya uswahilini au kwenye barabara zilizojaa maji bila kujua kina halisi cha pahala unapopita. Kiufupi injini ya gari lako haitakiwai kuingia maji kwa maana pindi maji yanapofika kwenye usawa wa injini huingia kupitia vitundu vya manifolda ambapo hakika hapa kuna plagi za mlipuko mwisho wa siku gari itazima na ikitokea yamekukuta basi zima gari na uisukume kwani kuendelea kuiwasha husababisha injini kunyonya maji. Hakikisha unajua kimo cha gari yako na wapi inaweza pita na wapi haiwezi pita lakini pia kama kuna dimbwi hakikisha unajua kina chake vinginevyo unaweza lala barabarani na ukashusha injini vilevile. Hivyo usiendeshe gari kwa mazoea ukaleta yale ya "I know my car" ukaona kila sehemu ni ya kupita ndugu gari sio Kifaru.

6. MOSHI WA AINA YOYOTE ILE.

Kwa kawaida gari ya petroli haitakiwi kutoa moshi wowote mwingi unaoonekana kwani ikitokea hivyo basi jua injini ya gari yako ina shida. Nimetanguliza kusema hivyo kwasababu bomba la moshi limeundwa ili kutoa hewa chafu kutoka kwenye injini lakini haitakiwi kuwa moshi mkubwa unaoonekana pale unapokuwa unaendesha gari kwani kwa kipindi unawasha gari ikitoa moshi na maji kidogo ni jambo la kawaida. Somo la aina za moshi kutokana na rangi yake ili kujua tatizo nitakuja kulileta hapa lakini kwa hii mada hutakiwi kupuuzia moshi wowote unaotoka kwenye gari ukiwa unaendesha au ukipiga resi {hasa kwa gari za Diesel}.


7. GARI KUTOKUWAKA KWA WAKATI

Gari kutokuwaka kwa wakati husababishwa na sababu nyingi sana wengi huwa tunaendesha magari kimazoea kwani mtu anapowasha gari zaidi ya mara tatu na ikaja kuwaka mara ya nne ni kawaida na kuendelea na safari huku ukipuuzia. Binafsi ilishawahi nitokea na shida ilikuwa ni betri ilipofika siku ya kufa nyani iligoma kabisa kuwaka hadi nilipokuja kubustiwa. Ukubwa wa tatizo huja pale ambapo una haraka au una dharura na gari ikagoma kabisa kuwaka mfano una mgonjwa au dharura nyingineyo hapo ndipo unapokuja kujuta kwanini ulipuuzia mwanzoni. Gari kushindwa kuwaka husababishwa na sababu nyingi sana ila kubwa ni matatizo ya betri ya gari yako au kuharibika kwa starter na uzuri huwa haziharibiki ghafla huwa zinaanza na dalili ambazo ni ugumu katika kuwaka na baadae hugoma kabisa kuwaka. Ni vema kujua tatizo pale dalili zinapojitokeza kwani huenda pia ni shida ndogo tu kama vile inaweza kuwa kutu kwenye vichwa vya betri ambavyo unatakiwa kusafisha tu alafu gari ikarudi kwenye hali yake ya kawaida.

UKWELI KUHUSU NISSAN DUALIS
Kikubwa ambacho mara nyingi huwa nawaambia watu ni kutoendesha au kuvihudumia hivi vyombo vyetu kwa mazoea. Hakika kila gari ina namna yake ya kuihudumia na pia spea na vilainishi vyake. Nimalize na mfano ambao pia una elimu juu yake Kuna watu wengi huwa wanaumiza kichwa la kwanini gari aina ya Dualis zimeshindwa kufanya vema nchini na pia zimelalamikiwa sana hakika mimi ni shahidi sababu nimeshawahi kuwa nayo. Hizi gari watu wanazilalamikia lakini kiukweli ni gari ambazo zimefanya vema sana sokoni Ulaya yani ni katika top 10 ya gari ambazo wazungu wengi walizinunua na wakazipenda.

Kwanini zinalalamikiwa sana Tanzania? Jibu ni Simple tu hizi gari watu wanazitumia kwa matumizi ambayo kinyume na gari inavyotaka. Huwezi nunua dualis na ukaitumia kwa matumizi ambayo watu wa Rav 4 Old wanaitumia kwakigezo tu kwamba gari iko juu na nyingi zina 4wheel hivyo unaweza itumia vyovyote na kupita popote hapana. Dualis ni mfano wa baunsa ambaye ni mtoto wa mama yani ukimwona ni mgumu anatisha lakini kumbe ni Mamaz boy kofi moja tu analia hata harudishi. Hii gari haihitaji shida kabisa yani kama wewe ni mtu wa rough road kwa mwaka zile mounting utabadili zaidi ya mara tatu. Pia tatizo la kulalamikiwa kuungua ni kwasababu ya mazoea tuliyonayo ya kupelekea gari kwa watu ambao si wataalamu akuwekee sijui Mziki ama akuon gezee mataa na vitu vingine vya umeme, Mkuu hii gari haitaki hayo kabisa kiufupi kama unamiliki hii gari amini kwamba unamiliki Benz au Classic cars zingine ambazo hazihitaji shortcut na pia hazitaki shida kwa maana kwamba Dualis iweke kwenye kundi hilo na ndiyo maana Europe zilifanya vema kwasababu wenzetu huwa hawana kona kona yani gari ikienda kurekebishwa inaenda kwa Mechanic haswaa na si mafundi wa mtaani na hata maswala yanayohusu umeme kama vile mziki na taa za nyongeza hufanywa kwa vipimo maalum na mashine maalum. Swali la kujiuliza kwa wale wanaosema Dualis ni gari mbaya je ni kwanini gari ambayo ni best selling car in UK 2022 japo imeundwa Sunderland lakini ni toleo la kwanza la Dualis alafu anatokea Mtanzania mmoja anasema zile gari hamna kitu, Hakika utajiuliza mara mbili kwanini. Nadhani point ya msingi imeshaeleweka na suala la Dualis ni swala ambalo linatokea kwenye magari mengi sana ambayo yanakuja Tanzania na kushindwa kufanya vema,Kiufupi ugonjwa wetu ni kuendesha au kumiliki gari kwa mazoea. Kabla hujamiliki unatakiwa ujue gari unayoenda kumiliki ina strength na weakness gani hakika tusifanye vitu kwa mazoea na kama unaona wewe ni mtu wa mazoea ushauri wangu mkuu baki kwenye Toyota tena zile ambazo ni common. Naomba nimalize na mfano wa mwisho tukibaki hapo hapo kwenye Nissan. Watu wengi huzilalamikia sana Nissan X Trail lakini kuna Muhindi ana X Trail yake namba B ukiiona ni mpya kabisa na namfahamu mpaka leo yuko nayo na kuna mwenye namba D ila imechoka hata Milion Nne hutoi, Nadhani Utakuwa umejifunza tukutane Makala nyingine.


Imeandikwa na Hamis Mgaya

0655513132
 
Back
Top Bottom