Mazda Axela anauliza: Kwanini Hamnioni?

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,270
50,732
Najua utakua umekutana mjini na Mazda nyingi tu, especially CX5. Lakini, unajua kama Mazda family haijaishia hapo kuna mengine mazuri tu na yanafanya vizuri sokoni? Mfano huyu Mazda Axela.

Mazda Axela kama inavyojulikana Japan na China au Mazda 3 inavyojulikana nchi za nyingine ni gari ndogo inayokuja kwenye shape mbili, sedan na hatchback. Hadi leo ina matoleo manne (4).

First Generation 2003 - 2007
2003-2006_Mazda_Axela_Sport_(cropped).jpg

Second Generation 2008 - 2012
2009_Mazda3_Sport_2.0_Front.jpg

Third Generation 2013 - 2018
2014_Mazda3_(BM)_SKYACTIV_hatchback_(2014-03-15)_01.jpg

Fourth Generation 2019 - Hadi sasa
2019_Mazda3_SE-L_2.0_Front.jpg


Ni vigumu kuziongelea zote, kwa uzoefu wangu nitaomba niongelee kidogo Third Generation (2013 - 2018).

Kama tulivyosema hapo mwanzo, Axela za hiki kipindi zinakuja na shape za aina mbili, hatchback kama hii hapa chini...
2015_Mazda3_Sport_GX_in_Snowflake_White_Pearl,_Rear_Right.jpg


Na pia sedan, kwa wale wapenzi wa sedan kama mimi.
2018_Mazda3_Touring,_Rear_Right.jpg


Yeah, najua sedan ya hii generation sio nzuri kaa muonekano, ila Hatchback yake ni kali, sio tu kwenye picha, ata live.

Baada ya shape, tuje kwenye engine tulizoletewa:

Hapa tunakutana na engine za SkyActiv technology za Petrol na Diesel kuanzia ukubwa wa 1.5L, 2.0L, 2.2L na 2.5L zote inline 4 (i4). Na Hybrid pia ipo ya 2.0L Petrol/Hybrid.

Utajiuliza kwanini nina recomend hii generation kuliko zilizotangulia ni kwasababu kuanzia huu mwaka, Mazda ndio alianza kutumia SkyActiv technology kwenye Axela na kuachana na platform ya C1 aliyokua anatumia ya kampuni ya Ford. Hii ilikua na matatizo kadhaa na ulaji wa mafuta haukua mzuri sana.

Kwanini nakushawishi uiangalie kwa jicho la pili next time unavyotafuta gari?

1. Kwanza reliability ya magari ya Mazda.
Screenshot_20240425-001837.png

Kwa muda wako ukigoogle "most reliable used car brands" najua top tano zitakuja gari za Japan. Najua na Mazda lazima itakuwepo.

Na kama haitoshi, ukisearch Most reliable Used Mazda Cars, hauwezi ikosa Mazda 3 (Axela) kwenye iyo list.

2. Style au muonekano kuanzia nje hadi ndani.
Mazda Axela alichukua "koddo design" kutoka kwa CX-5. Yeye alikua wa tatu kucopy iyo design baada ya Mazda 6.

Mazda3_BM_Hatchback_Sports-Line_2.2_SKYACTIV-D_150_Automatik_Cockpit_Innenraum_Interieur.JPG

Kwa nje gari ina muonekano mzuri, na ndani pia ina muonekano wa kisasa sana.

3. Bei yake na Ushuru.
Najua bei ni subjective, kwasababu kwanza kwakua tunanunua used bei haiwezi kua constant. Ila inaanzia low as $3500 CIF na kwenda juu na ushuru unaanzia Mil 6 na kuendelea kutegemea vigezo vya miaka, mafuta na ukubwa wa engine.

4. Ulaji wa mafuta na power.
Najua bila hapa siwezi kukushawishi. Ila Axela yenye SkyActiv 2.0L inatumia mafuta kidogo kuliko IST yenye 1.3L 2NZ FE engine, kutokana na data za EPA.
Pamoja na ulaji mdogo wa mafuta, bado Mazda atakupa power zaidi (120hp) wakati IST atakupa 86hp.

*Nimetumia IST kama reference tu, tungeweza kuweka gari yoyote.

5. Options nyingi za Engine na transmission.
Axela anakupa options nyingi za Engine kuanzia cc 1500 hadi cc 2500 na pia anakupa options ya Petrol, Diesel na Hybrid na kama haitoshi anakupa option ya Manual na Automatic transmission. Upewe nini.

6. Vipi kuhusu spea na "mafundi"?
Unaambiwa, ukishasikia fundi anajiita " Specialist " wa gari fulani, ilo gari " fulani " liogope kama wewe mwenzangu na mimi.

Ndio maana hujawahi sikia fundi specialist wa Toyota ila utasikia wa Benz, VW, BMW, Land Rover etc. Nadhani umenielewa.

Mazda brand inajulikana vizuri tu Tanzania na spare zake wala sio tatizo. Maduka kibao mjini zinapatikana, na uzuri siku hizi Dunia kijiji unaweza ukatumiwa spare kutoka Dar kufika mkoa wowote chini ga siku mbili.

Okay, my point, usiogope kuitizama hii gari kisa cha kuwazia spare na mafundi.

Kila kizuri hakikosi Kasoro. Je huyu mwali ana kasoro gani?

1. Haka kadude kapo chini sana.
Hii haipingiki, ground clearance ya ili gari ni ndogo. Kwa barabara zetu haitapitika kila mahala lakini sio mbaya hadi ikukatishe tamaa kabisa.

Tuchukulie mfano unaijua gari ya Toyota Runx au Allex. Basi naweza kukufananishia na hapo kwa kuangalia huu mchoro:

Screenshot_20240425-005014.png


Huo mchoro umezilishanisha gari mbili tajwa, mistari myeusi ni Mazda Axela na iyo rangi ya orange ni Toyota Runx/Alex.

Unaweza kuzingatia ukubwa wa gari na ground clearance for reference.

2. Seat za nyuma sio kubwa sana. Ila zinatosha kabisa. Pia buti lake sio kubwa saaaaana. Huko nyuma (seat) pia hakuna AC vents kwahiyo kwa mikoa yenye joto, watu wa nyuma kidogo wataumia kama joto ni kali sana (ila magari mengi madogo hayana).

3. Ina rangi nyepesi kidogo. Ni rahisi kuchubuka na kuacha mikwaruzo (ugonjwa wa Mazda).

4. Hybrid engine walikurupuka. Kama unaweza kuepuka achana nayo. Au kama lazima hybrid tafuta kwingine.

5. Kama unapiga mziki kwa Bluetooth inatabia ya kukata bila sababu. Sasa hii sijui kama inaweza kukushawishi usinunue Ila unaweza badirisha redio ukaweka aftermarket kali zaidi.

Je, mbadala wake?

Kama umezielewa Mazda, unaweza angalia mbadala wale (cheaper zaidi) bwan Mazda Demio kama uyu hapa chini:
Mazda_Demio_XD_Touring_L_Package.jpg


Au Mazda CX3 huyu hapa:

1280px-2017_Mazda_CX-3_Sport_NAV_Automatic_2.0_Rear.jpg


Karibuni tujadili zaidi Mazda Axela.

Pamoja.
 
Baba mwenye nyumba wangu anayo CX 5 ,kuna siku nilipewa lift aisee ni mkwaju wa maana afu yule mzee anapenda mbio.

Ni hela tu hazijanitembelea ila kwa maisha ya sasa kua na chuma cha maana ni moja ya nyenzo ya kupata deals kubwa ,heshima na starehe.
 
Baba mwenye nyumba wangu anayo CX 5 ,kuna siku nilipewa lift aisee ni mkwaju wa maana afu yule mzee anapenda mbio.

Ni hela tu hazijanitembelea ila kwa maisha ya sasa kua na chuma cha maana ni moja ya nyenzo ya kupata deals kubwa ,heshima na starehe.
😁😁 Zikija kututembelea mzee tunajiweka kwenye CX5. Kali sana.
 
Back
Top Bottom