SoC02 Tawala Fikra zako Ili uweze kuboresha maisha yako

Stories of Change - 2022 Competition
Jul 13, 2021
19
35
Mwandishi mmoja aliwahi kusema “Hakuna sumu yenye kuidhuru akili yenye mawazo chanya na hakuna dawa yenye kutibu akili yenye mawazo hasi” bahati mbaya sana akili za watu wengi zimetawaliwa sana na mawazo hasi kuliko mawazo chanya pia nakubaliana na msemo wa Brian Tracy “Badili namna unavyofikiri ili ubadili maisha yako”.

Imani ya kuamini huwezi kufanikiwa kwa sababu ya watu fulani kukuambia huwezi kufanikiwa kwa mawazo yao au kwa kushindwa kwao kiasi Kukata tamaa kuona kama wao wameshindwa basi hata wewe utashindwa kwenye kitu unachofanya “Sijui ufunguo wa mafanikio lakini najua ufunguo wa kufeli ni kutaka kumridhisha kila mtu” alisema Boby Cosby mwigizaji maarufu wa filamu Marekani.

Kiasi kwamba maneno ya kukatishwa tamaa kuwa huwezi kwa sababu ya fulani alishindwa kwenye kitu unachofanya sasa wewe, umri ambao unao huwezi kabisa kufanikiwa kabisa sababu wewe ni mdogo sana au mkubwa sana na unatakata tamaa kupambania malengo yako na ndoto zako; Kumbuka kukata tamaa haifanyi maisha kuwa rahisi hata kidogo.

Tambua huwezi kuzuia watu kuongea kile wanachokiamini lakini unaweza sana kuthibiti nini kiingie kwenye akili yako kile ambacho wamezungumza, bahati mbaya sana unaamini sana maneno ya watu wengine kuwa ndio sahihi kuliko unavyoamini mawazo yako kuwa ni sahihi

Je unashindwa kuamini mawazo yako kwa sababu ya hofu na uoga Kutawala maisha yako?

Je unafikiria watakuonaje usipokubali mawazo yao?

Kumbuka maneno ambayo unaambiwa kuwa huwezi, utashindwa, hustahili, hutofanikiwa, wewe ni maskini tu, biashara hii unayofanya haikufai kabisa n.k yanatoka kwa watu wa karibu sana ambao unawaamini sana inawezekana wazazi wako, walezi wako, ndugu zako, mpenzi wako, mume/mke wako na marafiki zako.

Kiasi unaaogopa kufanya kitu fulani kwa kuhofia watakutazamaje ukifanya kitu hicho hivyo unashindwa kuanza kuchukua hatua ya kufanya ili uweze kuboresha maisha yako

Unaona aibu ya kufanya kazi fulani kwa sababu ya elimu ambao unao na hadhi ambayo unayo unaona ukifanya watakucheka kwa kuona kitu unachofanya ni cha kimaskini sana mfano unataka kutembeza bidhaa za biashara yako mtaani na ni muhitimu wa chuo kikuu unaona watu watakubeza hivyo unaacha kufanya kuishia kuwa pale pale huku unasubiri kazi kiuhalisia kazi serikali ambapo ajira ni chache kuliko idadi ambao wanatafuta ajira.

Upo kwenye mahusiano ambayo unaona kabisa sio sahihi lakini bado unang’ang’ania kwa sababu unaogopa kutoka kwenye mahusiano hayo kwa hofu utakuwa mpweke sana

Je unajua umezaliwa kuwa mtawala kwenye kila kitu na sio kutawaliwa?

Ndio umezaliwa kuwa mtawala hivyo kuwa mtawala wa maisha yako kwa kila kitu Ili uweze kufurahia maisha yako na kuyaboresha maisha yako

Ili uwe mtawala maisha yako ni kuanza kutumia muda mwingi kufikiria maisha yako na vitu ambayo unafanya kuliko kufikiria watu wengine wanafikiria nini kuhusu wewe

Huwezi kuthibiti nini watu wanafikiria kuhusu wewe kwa sababu ipo nje ya uwezo wako lakini unaweza kuthibiti fikra zako juu ya nini ufikiri kuhusu maisha yako na ipo ndani ya uwezo wako

Hivyo usijisumbue kuthibiti kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako

Tumia muda mwingi kufikiria maisha yako muhimu zaidi fikra zako ziwe ni fikra chanya na sio hasi sababu fikra chanya zinajenga na kuboresha maisha yako wakati fikra hasi mara zote zipo kubomoa na kuharibu maisha yako

Ili uwe na fikra chanya ni kuanza kufanya mambo yafuatayo;

✔️ Jenga tabia ya kujifunza kila siku kwa kuongeza maarifa, bahati nzuri tupo nyakati ambazo maarifa ni mengi ya bure na ya kulipia kwa kusoma vitabu, kuhudhuria semina, kusikiliza Podcast na audbooks n.k maarifa yanasaidia sana kuwa na mtazamo/fikra chanya, hivyo nakushauri tafuta Kitabu cha “The power of your subconscious mind” cha Dr Joseph Murphy kitakusaidia sana

✔️ Ambatana watu wenye mtazamo chanya, watu ambao unaambatana nao kwenye maisha yako hakikisha ni watu ambao wanakujenga na kuamini kila kitu kinawawezekana maishani, ambao waamini wao wanaweza, wapambanaji, wazingatiaji (wana focus) maisha yao, washindi, hawafuatili maisha ya watu wengine n.k, wewe ni wastani wa watu watano ambao unashinda nao muda mwingi.

✔️ Anza kujiambia maneno chanya, fikra chanya zinajengwa na kile ambacho unasikia au kuongea hivyo muda mwingi jiambie maneno chanya kila siku na baada ya muda itakuwa sehemu ya maisha kwa sababu maneno yanaumba mfano mimi ni mshindi, Mimi najiamini, Mimi naweza, Mimi ni mpambanaji, Mimi sio mvivu, Mimi ni wakipekee, Mimi nimezaliwa kufanikiwa n.k jiambie kila siku utaona jinsi gani maisha yako yanavyozidi kuwa bora zaidi

Kupitia mambo haya matatu inamaana kabisa “Mtazamo chanya ni kila kitu maishani” mtazamo chanya ndio chachu ya kuongeza kiwango cha kujitambua

Mtazamo/fikra chanya ndio msingi wa Kutawala maisha yako na kuweza kuboresha maisha yako

Ukiwa na mtazamo chanya utaweza kuchukua hatua kutimiza malengo yako na ndoto zako pasipo kuonea aibu watu wengine

Ukiwa na mtazamo chanya utakuwa mtu mwenye ufanisi mkubwa kwenye maisha yako na mambo ambayo unafanya kwa sababu utajua nini unataka kwenye maisha yako hivyo utafanya kwa ubora wa hali ya juu

Ukiwa na mtazamo chanya utakuwa mtu mwenye kujiamini sana sababu hofu na uoga sio sehemu ya maisha yako kwa maana tayari umeweza Kutawala hofu na uoga hivyo utaweza kuboresha maisha yako

Ukiweza Kutawala maisha yako pasipo watu wengine kuendesha maisha yako kwa namna yeyote utaweza kuyaongezea thamani maisha yako na kuweza kutimiza malengo yako na ndoto zako

Kumbuka umezaliwa kuwa mtawala wa maisha yako na sio kutawaliwa na maisha yako pamoja na maisha ya watu wengine, hivyo focus na maisha yako na kuboresha maisha yako zaidi

Mwisho kabisa unaweza kufanikiwa kuboresha maisha yako pasipo kujali kiwango cha elimu ambayo unayo, mtaji ambao unao, historia ya maisha yako muhimu ni kubadili fikra zako na kuwa na fikra chanya ili uweze kubadili maisha
_______
Imeandikwa na Innocent Ngaoh.

04C90A35-2524-4057-AB62-F901FE869BD2.jpeg
2FEA1E4E-A2F9-4743-BE5F-4B1629DAFA6A.jpeg
 
bandiko zako ni zakibabe hongera kwa kujitambua mapema na kuiona fursa yakuzindua wengine pia ili jamii iamasike kwa ukubwa kuleta maendeleo respect mkuu
 
Mwandishi mmoja aliwahi kusema “Hakuna sumu yenye kuidhuru akili yenye mawazo chanya na hakuna dawa yenye kutibu akili yenye mawazo hasi” bahati mbaya sana akili za watu wengi zimetawaliwa sana na mawazo hasi kuliko mawazo chanya pia nakubaliana na msemo wa Brian Tracy “Badili namna unavyofikiri ili ubadili maisha yako”.

Imani ya kuamini huwezi kufanikiwa kwa sababu ya watu fulani kukuambia huwezi kufanikiwa kwa mawazo yao au kwa kushindwa kwao kiasi Kukata tamaa kuona kama wao wameshindwa basi hata wewe utashindwa kwenye kitu unachofanya “Sijui ufunguo wa mafanikio lakini najua ufunguo wa kufeli ni kutaka kumridhisha kila mtu” alisema Boby Cosby mwigizaji maarufu wa filamu Marekani.

Kiasi kwamba maneno ya kukatishwa tamaa kuwa huwezi kwa sababu ya fulani alishindwa kwenye kitu unachofanya sasa wewe, umri ambao unao huwezi kabisa kufanikiwa kabisa sababu wewe ni mdogo sana au mkubwa sana na unatakata tamaa kupambania malengo yako na ndoto zako; Kumbuka kukata tamaa haifanyi maisha kuwa rahisi hata kidogo.

Tambua huwezi kuzuia watu kuongea kile wanachokiamini lakini unaweza sana kuthibiti nini kiingie kwenye akili yako kile ambacho wamezungumza, bahati mbaya sana unaamini sana maneno ya watu wengine kuwa ndio sahihi kuliko unavyoamini mawazo yako kuwa ni sahihi

Je unashindwa kuamini mawazo yako kwa sababu ya hofu na uoga Kutawala maisha yako?

Je unafikiria watakuonaje usipokubali mawazo yao?

Kumbuka maneno ambayo unaambiwa kuwa huwezi, utashindwa, hustahili, hutofanikiwa, wewe ni maskini tu, biashara hii unayofanya haikufai kabisa n.k yanatoka kwa watu wa karibu sana ambao unawaamini sana inawezekana wazazi wako, walezi wako, ndugu zako, mpenzi wako, mume/mke wako na marafiki zako.

Kiasi unaaogopa kufanya kitu fulani kwa kuhofia watakutazamaje ukifanya kitu hicho hivyo unashindwa kuanza kuchukua hatua ya kufanya ili uweze kuboresha maisha yako

Unaona aibu ya kufanya kazi fulani kwa sababu ya elimu ambao unao na hadhi ambayo unayo unaona ukifanya watakucheka kwa kuona kitu unachofanya ni cha kimaskini sana mfano unataka kutembeza bidhaa za biashara yako mtaani na ni muhitimu wa chuo kikuu unaona watu watakubeza hivyo unaacha kufanya kuishia kuwa pale pale huku unasubiri kazi kiuhalisia kazi serikali ambapo ajira ni chache kuliko idadi ambao wanatafuta ajira.

Upo kwenye mahusiano ambayo unaona kabisa sio sahihi lakini bado unang’ang’ania kwa sababu unaogopa kutoka kwenye mahusiano hayo kwa hofu utakuwa mpweke sana

Je unajua umezaliwa kuwa mtawala kwenye kila kitu na sio kutawaliwa?

Ndio umezaliwa kuwa mtawala hivyo kuwa mtawala wa maisha yako kwa kila kitu Ili uweze kufurahia maisha yako na kuyaboresha maisha yako

Ili uwe mtawala maisha yako ni kuanza kutumia muda mwingi kufikiria maisha yako na vitu ambayo unafanya kuliko kufikiria watu wengine wanafikiria nini kuhusu wewe

Huwezi kuthibiti nini watu wanafikiria kuhusu wewe kwa sababu ipo nje ya uwezo wako lakini unaweza kuthibiti fikra zako juu ya nini ufikiri kuhusu maisha yako na ipo ndani ya uwezo wako

Hivyo usijisumbue kuthibiti kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako

Tumia muda mwingi kufikiria maisha yako muhimu zaidi fikra zako ziwe ni fikra chanya na sio hasi sababu fikra chanya zinajenga na kuboresha maisha yako wakati fikra hasi mara zote zipo kubomoa na kuharibu maisha yako

Ili uwe na fikra chanya ni kuanza kufanya mambo yafuatayo;

Jenga tabia ya kujifunza kila siku kwa kuongeza maarifa, bahati nzuri tupo nyakati ambazo maarifa ni mengi ya bure na ya kulipia kwa kusoma vitabu, kuhudhuria semina, kusikiliza Podcast na audbooks n.k maarifa yanasaidia sana kuwa na mtazamo/fikra chanya, hivyo nakushauri tafuta Kitabu cha “The power of your subconscious mind” cha Dr Joseph Murphy kitakusaidia sana

Ambatana watu wenye mtazamo chanya, watu ambao unaambatana nao kwenye maisha yako hakikisha ni watu ambao wanakujenga na kuamini kila kitu kinawawezekana maishani, ambao waamini wao wanaweza, wapambanaji, wazingatiaji (wana focus) maisha yao, washindi, hawafuatili maisha ya watu wengine n.k, wewe ni wastani wa watu watano ambao unashinda nao muda mwingi.

Anza kujiambia maneno chanya, fikra chanya zinajengwa na kile ambacho unasikia au kuongea hivyo muda mwingi jiambie maneno chanya kila siku na baada ya muda itakuwa sehemu ya maisha kwa sababu maneno yanaumba mfano mimi ni mshindi, Mimi najiamini, Mimi naweza, Mimi ni mpambanaji, Mimi sio mvivu, Mimi ni wakipekee, Mimi nimezaliwa kufanikiwa n.k jiambie kila siku utaona jinsi gani maisha yako yanavyozidi kuwa bora zaidi

Kupitia mambo haya matatu inamaana kabisa “Mtazamo chanya ni kila kitu maishani” mtazamo chanya ndio chachu ya kuongeza kiwango cha kujitambua

Mtazamo/fikra chanya ndio msingi wa Kutawala maisha yako na kuweza kuboresha maisha yako

Ukiwa na mtazamo chanya utaweza kuchukua hatua kutimiza malengo yako na ndoto zako pasipo kuonea aibu watu wengine

Ukiwa na mtazamo chanya utakuwa mtu mwenye ufanisi mkubwa kwenye maisha yako na mambo ambayo unafanya kwa sababu utajua nini unataka kwenye maisha yako hivyo utafanya kwa ubora wa hali ya juu

Ukiwa na mtazamo chanya utakuwa mtu mwenye kujiamini sana sababu hofu na uoga sio sehemu ya maisha yako kwa maana tayari umeweza Kutawala hofu na uoga hivyo utaweza kuboresha maisha yako

Ukiweza Kutawala maisha yako pasipo watu wengine kuendesha maisha yako kwa namna yeyote utaweza kuyaongezea thamani maisha yako na kuweza kutimiza malengo yako na ndoto zako

Kumbuka umezaliwa kuwa mtawala wa maisha yako na sio kutawaliwa na maisha yako pamoja na maisha ya watu wengine, hivyo focus na maisha yako na kuboresha maisha yako zaidi

Mwisho kabisa unaweza kufanikiwa kuboresha maisha yako pasipo kujali kiwango cha elimu ambayo unayo, mtaji ambao unao, historia ya maisha yako muhimu ni kubadili fikra zako na kuwa na fikra chanya ili uweze kubadili maisha
_______
Imeandikwa na Innocent Ngaoh.

View attachment 2354909View attachment 2354910
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom