Siri ya maisha mazuri

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,936
12,217
Ni kuwa na nia ya kweli na ya dhati ya kufanikiwa kumshirikisha mungu katika mipango na vipaumbele kuelekea maisha mazuri..

Kuwa na bidii, maarifa na moyo wa kutokukata tamaa, pale unapokutana na magumu, mabonde na milima..

Na ukipita vizuri apo, huo unaweza kua mtaji lakini pia msingi muhimu sana wa maisha yako mazuri...

Kutokutilia maanani, kutokuzingatia wala kubabaishwa na lawama, mawazo au maoni ya kukuvunja moyo au kudhoofisha nia, jitihada na malengo yako yakupata maisha mazuri, mathalani kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki...

Degree ulizonazo zikusaidie tu katika kukuongezea usataarabu, utulivu, hekima uwezo wa haraka wa kutathimini madhara na faida za maamuzi utakayo chukua huko mbeleni dhidi ya mafanikio na maisha yako mazuri..

Lakini pia degree zako zikusaidie kubuni namna bora zaidi ya kumaintain stataus ya mafaniakio yako na maisha yako mazuri...

Hata hivyo,

Haya ni miongoni mambo machache sana ya kukupelekea, ndungu mwanafamilia wa jf kua na maisha mazuri,

Kutoka kwa wadau wa mafanikio na maisha mazuri,

Hebu sasa tupate mbinu, mikakati, mitindo na namna mbalimbali za kufanikisha kua na maisha maziri maishani...

Nawatakia yanga ushindi mnono dhidi ya mamelodi

Pasaka njema nyote
 
Back
Top Bottom