Tasnia ya Habari na vifo vya mapema, nini kipo nyuma ya pazia?

Pascal mayalla aliwahi kuelezea hii scenario ila aliizungumzia radio Tanzania ilivyopoteza watangazaji wengi,
 
Wanahabari,

Isack Gamba, Ahmed Juma Baragaza, Fredwaa, Ephraim Kibonde, Agnes Almasy, Samadu Hassan, Gardner G Habash, Prince baina kamukulu na wengine wengi wameondoka wakiwa na umri mdogo.

Inaweza ikawa ni kawaida au isiwe kawaida hasa tukifanya ulinganifu na tasnia nyingine ambazo ni siasa, biashara, sanaa na michezo n.k.

Kama sio kawaida tatizo ni nini? Je? Ni lifestyle, kukosa mazoezi au kuondoana mapema? So much confusing.
Embu angazia na tasnia ya wanamuziki pia.

Ukianza na wa kimataifa Bob Marley na wengineo, halafu uje na wa humu nchini kuanzia akina Chiriku Maneti na wengineo walivyokufa bado makinda.

Ndiyo tuje tuivaliuate kwa pamoja nini kipo nyuma ya siri ya vifo vyao vya mapema?
 
Umri mdogo? Huo umri mdogo huanzia miaka mingapi hadi mingapi?Ni sawa na kutueleza kwamba watu wenye albinism huwa hawafi.

Au, kusema wazungu hapa Tanzania hawafi.Si kweli.Uchache wao hutufanya tufikiri hayo.Wanahabari ni wachache ukilinganisha na raia wengine.Wana maisha na hufa.

Tafakari kwa kutulia.Hakuna jipya ofisa!
Umri mdogo wa kufa ni miaka chini ya 70 ambayo imeandikwa hata kwenye vitabu vitakatifu.

Ukifa 70+ haifikirishi sana.

Watu msibani watakuwa wanauliza... 'Hivi huyu mzee alikuwa anaumwa nini'...huku wakichati na kinamama kulia machozi ya kulazimisha ya msibani kuonesha naye kalia.
 
humo Kila mtu na lake !!.

Kikubwa

Tuchukue Tahadhari wakati wa kutumia vyombo vya moto barabarani.

Tulale kwenye vyandarua vyenye Kinga dhidi ya Malaria.

Tunywe Maji safi na Salama Kwa kiwango sahihi.

Tudhibiti au tuache kabisa Pombe.

Tudhibiti au tuache kabisa Sigara.

Tupunguze uzito .

Tupunguze mavyakula ya viwandani na ya mafuta .

Tufanye mazoezi

👉👉Matumizi ya Kondomu

👉Tuwe waaminifu Kwa Wapenzi /Wachumba au Ndoa zetu.

Tutembelee Mbuga za wanyama .

Tujitoe out tupunge upepo.


Tuongee na watu tuwapo na matatizo tunayopitia.

Tufanye uchunguzi wa mwili angalau Kwa mwaka Mara mbili

Wagonjwa wa Magonjwa yasoambikiza , wahudhurie Kliniki, watumie dawa waachane na waganga wa kienyeji.


👉👉👉👉TUMUOMBE MUNGU

Tuache majungu kazin.

Tufanye kazi Kwa weledi Kila Mmoja Kwa nafasi yake ili Tusionenae wivu maana ndo inafanya tunapeana simu na kulogana.



Mengine wataongezea
 
Nahisi mfumo wa maisha yao unawaweka hatarini.

Wanaishi maisha ya bata sana maana kazi yao haiwafanyi wawe busy.

Kazini huwa wanaingia muda wa vipindi vyao tu. Na vikimalizika wanaenda kula bata
Hivi wale watoto walio kufa Arusha kwa gari lao kutumbukia kwenye mto ni bata gani walikuwa wakila?
 
Sababu zpo nyingi tu kwa uliowataja.
Ugonjwa gadner na gamba
Ajali fredwaa dereva alikua amelewa.
Prince alifariki akiwa kwenye session ya maazoezi ya viungo akiwa kwake. Hii hata gym ya sinza pale mapambano vijana watatu washafariki wakiwa mazoezini.
Hivo kuna umri shughuli huwa nyingi. Ukitoboa wewe mwamba that's 30-50
 
humo Kila mtu na lake !!.

Kikubwa

Tuchukue Tahadhari wakati wa kutumia vyombo vya moto barabarani.

Tulale kwenye vyandarua vyenye Kinga dhidi ya Malaria.

Tunywe Maji safi na Salama Kwa kiwango sahihi.

Tudhibiti au tuache kabisa Pombe.

Tudhibiti au tuache kabisa Sigara.

Tupunguze uzito .

Tupunguze mavyakula ya viwandani na ya mafuta .

Tufanye mazoezi

Matumizi ya Kondomu

Tuwe waaminifu Kwa Wapenzi /Wachumba au Ndoa zetu.

Tutembelee Mbuga za wanyama .

Tujitoe out tupunge upepo.


Tuongee na watu tuwapo na matatizo tunayopitia.

Tufanye uchunguzi wa mwili angalau Kwa mwaka Mara mbili

Wagonjwa wa Magonjwa yasoambikiza , wahudhurie Kliniki, watumie dawa waachane na waganga wa kienyeji.


TUMUOMBE MUNGU

Tuache majungu kazin.

Tufanye kazi Kwa weledi Kila Mmoja Kwa nafasi yake ili Tusionenae wivu maana ndo inafanya tunapeana simu na kulogana.



Mengine wataongezea
Umenena Kwa kina
 
Back
Top Bottom