Tasnia ya Habari na vifo vya mapema, nini kipo nyuma ya pazia?

kalisheshe

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
1,882
3,517
Wanahabari,

Isack Gamba, Ahmed Juma Baragaza, Fredwaa, Ephraim Kibonde, Agnes Almasy, Samadu Hassan, Gardner G Habash, Prince baina kamukulu na wengine wengi wameondoka wakiwa na umri mdogo.

Inaweza ikawa ni kawaida au isiwe kawaida hasa tukifanya ulinganifu na tasnia nyingine ambazo ni siasa, biashara, sanaa na michezo n.k.

Kama sio kawaida tatizo ni nini? Je? Ni lifestyle, kukosa mazoezi au kuondoana mapema? So much confusing.
 
Mkuu hata mtaani watu wanakufa Sana kwa umri huo below 50 yrs ni kwakuwa sio famous huwezi kuwajua

Pia MTU ukifikisha miaka 25 unabidi kuwa makini na AFYA yako

Kuanzia miaka 25 robo karne MTU anabidi kuishi Kama mzee kwa tahadhari Sana.

Kupunguza pombe au kuacha
Ngono kuwa na kiasi
Sigara ,bangi kuacha
Kamali kubeti n.k

Unfortunately watu wakifika huo umri wa 25 yrs wanajiona wanaweza kufanya kila aina ya Anasa na mwisho wanaingia 40 washaisha figo na maini vimeshachoka.

Kutoboa 50 inakuwa ngumu Sana kutokana na lifestyle waliyoishi nyuma
 
Wanahabari
Isack gamba, ahmed juma baragaza, fredwaa, ephraim kibonde, agnes almasy, samadu hassan, gardner g habash, prince baina kamukulu na wengine wengi wameondoka wakiwa na umri mdogo...
Unatakiwa ufanye research kabla ya kuandika hivi. Wanahabari ni watu wanaojulika na watu wengi , hivyo vifo vyao ni lazima vitajulikana na watu wengi.

Nikikuuliza ni madaktari au mahakimu wangapi wamefariki mwaka huu bila shaka utajua wale unaowajua ambao ni wachache.

Daktari anajulika na watu wachache, hata wilaya nzima haiwezi kumjua, hivyo akifariki ni watu wachache watajua kifo chake, lakini mtangazaji wa radio au TV anajulikana karibu nchi nzima hivyo hivyo kifo chake.
 
Mkuu hata mtaani watu wanakufa Sana kwa umri huo below 50 yrs ni kwakuwa sio famous huwezi kuwajua...

Kutoboa 50 inakuwa ngumu Sana kutokana na lifestyle waliyoishi nyuma
Hili ndio jibu sema wao wanajulikana maana tumezoea kuwaona kwenye tv ila kwenye tasnia zote watu wanakata moto daily life span ya mtz wanasema huwa ni 45 na zaidi kidogo
Ni muhimu kuwa na tahadhari ya afya zetu
 
Wanahabari
Isack gamba, ahmed juma baragaza, fredwaa, ephraim kibonde, agnes almasy, samadu hassan, gardner g habash, prince baina kamukulu na wengine wengi wameondoka wakiwa na umri mdogo...
Umri mdogo? Huo umri mdogo huanzia miaka mingapi hadi mingapi?Ni sawa na kutueleza kwamba watu wenye albinism huwa hawafi.

Au, kusema wazungu hapa Tanzania hawafi.Si kweli.Uchache wao hutufanya tufikiri hayo.Wanahabari ni wachache ukilinganisha na raia wengine.Wana maisha na hufa.

Tafakari kwa kutulia.Hakuna jipya ofisa!
 
Wanahabari,

Isack Gamba, Ahmed Juma Baragaza, Fredwaa, Ephraim Kibonde, Agnes Almasy, Samadu Hassan, Gardner G Habash, Prince baina kamukulu na wengine wengi wameondoka wakiwa na umri mdogo.

Inaweza ikawa ni kawaida au isiwe kawaida hasa tukifanya ulinganifu na tasnia nyingine ambazo ni siasa, biashara, sanaa na michezo n.k.

Kama sio kawaida tatizo ni nini? Je? Ni lifestyle, kukosa mazoezi au kuondoana mapema? So much confusing.
Babu yangu alinijuza kama utaweza kuficha sura yako na sauti...angalau utakuwa salama katika huu ulimwengu wa washirikina.
 
Back
Top Bottom