SoC04 Tanzania inavyoweza kunufaika na Lugha ya Kiswahili kama raslimali nyingine

Tanzania Tuitakayo competition threads

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,560
2,270
Katika makala hii tutajadili jinsi ya kukufanya kiswahili kuwa bidhaa, jinsi ya kukufanya kuwa na mashiko kiuchumi, mbinu mpya ya kukiendeleza na kuwavutia zaidi wazungumzaji na jinsi tunavyoweza kunufaika na Lugha hii katika muktadha wa kiuchumi.

Ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili tunaweza kueleza kwa uchache kuwa nimchakato wa kuifanyia lugha kuwa bidhaa na kuiuza kwa wengine kwa njia ya mabadilidhano na fedha. Kama zilivyo raslimali nyingine nchi ya Tanzania ilibarikiwa kuwa na kiswahili sanifu kuliko nchi nyingine zinazozungumza kiswahili, hivyo nisahihi kusema kuwa Tanzania inazungumza kiswahili safi kuliko nchi nyingine zinazozungumza Kiswahili.

JINSI YA KUKIFANYA KISWAHILI KUWA BIDHAA
Ili kuanza kuifanya lugha ya kiswahili kuwa bidhaa nilazima tutengeneze kuhitajika kwa lugha ya kiswahili kwa wageni Kama vile kiakademia, kiutalii, kiburudani, na kiuchumi. Kuhitajika huko ndiko kutafanya tuweze kuiuza bidhaa hii kwa wageni. Mathalani tunaweza kutoa nafasi kwa wanafunzi wageni kusoma lugha ya kiswahili katika vyuo vyetu, au kutoa fursa ya wageni kuishi Tanzania ikiwa watajua kujifunza kiswahili. Hapa tutaweza kuuza vitabu vya kujifunza na kufundisha kiswahili kama bidhaa.

JINSI YA KUKIFANYA KISWAHILI KUWA NA MASHIKO KIUCHUMI
Nguvu ya kiuchumi katika lugha inayo nafasi kubwa sana katika kupendwa kwa lugha husika na kuenea kwake. Hii hutokana na ukweli kuwa nchi yenye nguvu kiuchumi huweza kueneza lugha yake kwa njia rahisi kwani watu wa mataifa mengine hulazimika kujifunza lugha hiyo kwa lengo la kunufaika na fursa zinazopatikana kwa wazungumzaji wa lugha hiyo. Kwa Sasa lugha ya Kiswahili inakosa mashiko makubwa kiuchumi kutokana na nchi yetu kutokuwa imara kiuchumi kulinganisha na nchi nyingine zenye hati miliki ya lugha kubwa duniani Kama vile, Kichina , kiingereza na kifaranza. Hivyo ili kukifanya kiswahili kiweze kukubalika zaidi duniani hatuna budi kukuza uchumi wetu ili kukifanya kiswahili kuwa na mashiko kiuchumi.

JINSI TUNAVYOWEZA KUNUFAIKA NA LUGHA YA KISWAHILI KIUCHUMI
Hapa tunalenga kupata faida itokanayo na mauzo ya lugha ya kiswahili Kama bidhaa inavyoweza kuuzwa sokoni na kujipatia kipato. Zifuatazo ninjia tunazoweza kukiuza kiswahili ili kutunufaisha kiuchumi

Moja, Kuuza vitabu vya kujifunza na kufunza kiswahili, Kama tulivyokwisha kuona hapo juu kuwa ikiwa tutakifanya kiswahili kizidi kukubalika kimataifa kitafanya wageni wengi wavutiwe kujifunza lugha hii hivyo kuwa na mahitaji makubwa ya kutafuta vitabu kwaajili ya kujifunza na kufundisha kiswahili hivyo kutuingizia kipato. Kwa mfano hai nilio nao nikuwa mwaka 2022 niliandika kijitabu Cha kurasa 20 cha kujifunza kiswahili na kukipakia katika mtandao wa Amazoni , baada ya muda nilikuta watu kutoka nchi mbalimbali wamenunua nakala, wawili kutoka marekani, mmoja Mexico, watatu kutoka India, na mmoja kutoka Misri. Idadi Yao sio kubwa Sana lakini ikiwa kiswahili kitazidi kuwavutia wageni basi tunaweza kuuza nakala nyingi zaidi kwa mataifa ya nje

Pili, Kuuza maudhui ya kiswahili mtandaoni : Hii ninjia nyingine ambayo tunaweza kutumia kukiuza kiswahili kitaifa na kimataifa, jambo hili linafanyika kitaifa kwa Sasa kwa watengeneza maudhui kurusha maudhui mbalimbali kwa lugha ya kiswahili katika majukwaa mbalimbali ya mtandaoni. Ikiwa kiswahili kitazidi kujua na kuenea watengeneza maudhui hao wanaweza kuwa na wafuatiliaji wengi katika mataifa ya nje hasa Ulaya na Marekani na hivyo kuongeza kipato

Tatu, Kufungua vituo vya kufundisha kiswahili katika mataifa ya nje; Kama wafanyavyo Taasisi ya Kichina ya confiscious, au shirika la kingereza, Taasisi Kama BAKITA ambayo ndiyo yenye jukumu la kukuza na kueneza kiswahili kisheria inaweza kuwezeshwa kwa kutenga bajeti kwaajili ya kuanzisha vituo vya kufunzia lugha katika nchi mbalimbali duniani pamoja na kuwashawishi wageni kujifunza lugha ya kiswahili kwa gharama fulani na kuingizia nchi kipato kupitia njia hiyo ya kufundisha kiswahili kwa wageni.

Nne, Kufanya lugha ya kiswahili kuwa ya lazima kwa wageni wanaotaka kunufaika na fursa za Tanzania ; Mathalani wale wageni wanaotaka Kuna kufanya kazi Tanzania au kuwekeza Tanzania kulazimika kujifunza kiswahili angalau kwa kiwango cha kwanza kabla ya kuruhusiwa kuishi Tanzania. Hii itawapa soko waalimu na wakufunzi wa lugha ya kiswahili kwani wageni hao watalalazimika kujifunza kiswahili ili wawezw kupata fursa hiyo. Jambo hili huweza kufanyika pia kwa vyuo vyetu kutoa fursa kwa wanafunzi wakigeni kuja kusoma bure iwapo wanamudu kuzungumza lugha ya kiswahili kwa kiwango fulani, hii itawavutia wanafunzi wengi wa kigeni kujifunza lugha ya kiswahili wakati huo sisi tukiiuza kwao.

Pamoja na hayo, Nilazima tufahamu ukweli kuwa ili lugha ya kiswahili uendelee kuwavutia wageni wengi nilazima kuwe na faida wanayoipata kutokana na kujua kwao lugha hii mbali na kuwasiliana, hivyo hatuana budi kujiimarisha kiuchumi ili kuwavutia wajifunzaji wengi zaidi nje ya wale wanaojifunza kwa malengo ya kielimu
 
Hongera Sana mkuu Uzi mzuri Sana huu kama njia hizi zitatumika hakika Tanzania tutanufaika na lugha yetu ya Kiswahili kama raslimali nyingine.
 
Nguvu ya kiuchumi katika lugha inayo nafasi kubwa sana katika kupendwa kwa lugha husika na kuenea kwake. Hii hutokana na ukweli kuwa nchi yenye nguvu kiuchumi huweza kueneza lugha yake kwa njia rahisi kwani watu wa mataifa mengine hulazimika kujifunza lugha hiyo kwa lengo la kunufaika na fursa zinazopatikana kwa wazungumzaji wa lugha hiyo. Kwa Sasa lugha ya Kiswahili inakosa mashiko makubwa kiuchumi kutokana na nchi yetu kutokuwa imara kiuchumi kulinganisha na nchi nyingine zenye hati miliki ya lugha kubwa duniani Kama vile, Kichina , kiingereza na kifaranza. Hivyo ili kukifanya kiswahili kiweze kukubalika zaidi duniani hatuna budi kukuza uchumi wetu ili kukifanya kiswahili kuwa na mashiko kiuchumi.
Kuna pointi ya msingi sana hapa.

Lazima tuwe na cha kuipa dunia, ili nayo ijali kuhusu mambo yetu kama lugha ya Kiswahili. Saaafi.

Pamoja na hayo, Nilazima tufahamu ukweli kuwa ili lugha ya kiswahili uendelee kuwavutia wageni wengi nilazima kuwe na faida wanayoipata kutokana na kujua kwao lugha hii mbali na kuwasiliana, hivyo hatuana budi kujiimarisha kiuchumi ili kuwavutia wajifunzaji wengi zaidi nje ya wale wanaojifunza kwa malengo ya kielimu
Umemalizia vema. Ndivyo ilivyo. Thamani ya nchi kuijumla wake. Ahsante sana
 
Kuna pointi ya msingi sana hapa.

Lazima tuwe na cha kuipa dunia, ili nayo ijali kuhusu mambo yetu kama lugha ya Kiswahili. Saaafi.

Umemalizia vema. Ndivyo ilivyo. Thamani ya nchi kuijumla wake. Ahsante sana
Nikweli mkuu
 
Asanteni Wadau wote mnaoendeleza kupiga kura bado kura 10 tu ushindi upatikane☺️
 
Back
Top Bottom