SoC04 Lugha ya kufundishia na kujifunzia katika mfumo wa Elimu Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

eddy2023

New Member
Oct 20, 2023
1
0
Mfumo wa elimu wa Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni umeonekana kulegalega mno. Hali inayosababisha kupoteza imani kwa mashirika ya ndani na nje katika kiwatumia wataalamu wetu. Ni ukweli usiopingika lugha inayotumika kufundishia inaweza kuwa sababu ya kujenga umahiri thabiti au uliolegalega.

Hali ilivyo sasa
Nchini Tanzania lugha mbili kiingeleza na kiswahili hutumika kwa pamoja katika mfumo wa elimu. Kiingeleza hutumika kama lugha ya kufundishia kwa ngazi ya sekondari mpka chuo kikuu, huku kiswahili kikiwa lugha ya kufundishia kwa ngazi ya msingi na awali.

Matokeo ya tafiti mbalimbali
tafiti mbalimbali za lugha kama za Noam Chomsky, na zile za wanasaikolojia wanaamini mtoto hujifunza vyema zaidi akitumia lugha yake ya kwanza. Lugha ambayo tayari ana ujuzi nayo. Pia katika nadharia ya "English modern linguistic theories" inaaminika matumizi ya lugha mbili katika mfumo wa elimu hupelekea "linguistic frustration" ikiimanisha kwamba uzao utakaopatikana katika mfumo huu, utakuwa njia panda katika lugha zote. Hatakuwa na stadi za kutosha katika lugha yoyote Moja wapo. Hii itapelekea zao katika mfumo huu kushindwa kumudu maarifa katika lugha Moja wapo au zote kwa pamoja. Utetezi huu upo katika nadharia ya balloon theory.

Matokeo katika mfumo wa Tanzania

wataalamu wanaozalishwa wameshindwa kabisa kumudu lugha mojawapo. Anayetumia kiswahili anahamia kwenye kiingeleza, anayetumia kiingeleza anaye hujikuta anahamia kwenye kiswahili. Hii imekuwa changamoto kubwa sana. Wataalamu wetu wameshindwa kuweza kuchanganua mambo kwa lugha yoyote kati ya kiswahili au kiingeleza. Hapa imekuwa tatizo.

Pia imepelekea kuwepo kwa mifumo ya shule ya mchepuo ya kiingeleza "English medium" na kiswahili medium inayopelekea matabaka katika fursa ya ajira na kukuza utofauti wa mwenye nacho na masikini.

Matokeo hasi ya mfumo uliyopo sasa
uwezo wa wataalamu wetu wameshindwa kishindana katika soko la dunia, na la ndani. Waliosoma nje wamesalia kuwa tegemeo huku wa ndani wakishindwa kushindana.

Pia, uwepo wa shule za mitaala ya kingeleza "English medium schools" na kiswahili medium" imepelekea kukuza janga la usawa katika nchi yetu. Siku hizi hakuna kiongozi anayesoma ktk shule za umma.

Pia, imepelekea kutengeneza walimu ambao hawawezi kumudu Kasi ya maendeleo ya karine ya 21. Mwalimu wa chemistry Tanzania anaweza kufundisha somo Hilo Urusi, USA nk??

Nini kifanyike?
Imezoeleka kisikia wazee wazamani wakisifika Kwa kistarabika na kielimika licha ya kuishia la nne ya mkoloni. Darasa la 12 la miaka ya 70 na Sasa haiendani ustarabu na mhitimu WA elimu ya ngazi ya shahada. Ktk kijitambua na kuchanganua mambo. Yafuatayo yanaweza kufanyika.

I. Kuchagua lugha Moja iwe ya kifundishia ngazi zote za elimu.

ii. Kutumia lugha ya kingeleza kama lugha ya kifindishalia maana inaonekana ndio mahitaji ya jamii kuliko kiswahili. Ni mahitaji Kwa sababu Ili kumudu mwingliano wa kimataifa lugha ya kingeleza inahitajika zaidi.

iii. Lugha ya kiswahili itumike kama lugha ya kufundishia Kwa ngazi zote. Kama ikiwa hivi basi lugha ya kingeleza ibaki kama somo na ipunguziwe majukumu ktk baadhi ya maeneo mahususi. Ili kiswahili kithaminisiwi. Maendeleo kama kwenye shughuli za mahakama, utoaji wa haki, habari.

iv. Kufuta uwepo wa shule za lugha ya kingeleza na za kiswahili. Maana zimelea na kukuza matabaka katika jamii yetu tofauti na zamani.
 

Attachments

  • tanzania_ur_education_sector_development_programme.pdf
    301 KB · Views: 2
, uwepo wa shule za mitaala ya kingeleza "English medium schools" na kiswahili medium" imepelekea kukuza janga la usawa katika nchi yetu
Usawa, ni ngumu kuwepo, japo lugha ni sehemu ndogo tu ya utofauti wao. Aliyepata elimu ya uhakika atatamba pote tu

Kufuta uwepo wa shule za lugha ya kingeleza na za kiswahili. Maana zimelea na kukuza matabaka katika jamii yetu tofauti na zamani
Kwa kuwa wapo watu ambao hutetea lugha mojawapo na kukataa nyingine: unaonaje tukiziacha zote ziendelee kuwepo. Za kiswahili na kingereza zote za binafsi na serikali ziwepo za kiswahili na kiingereza ili tuje tufanye utafiti mfumo utakaofaa zaidi??

Na hata baada ya hapo, kuendelea kuwepo kwa idadi ndogo ya shule mbadala ili wenye chaguo hilo waendelee kujifaidia.
 
Back
Top Bottom