SoC03 Somo la kilimo lifundishwe kama somo linalojitegemea na la lazima mashuleni. [kilimo cha mazao na mifugo]

Stories of Change - 2023 Competition
Sep 20, 2019
15
35
flyerdesign_07072023_220102.png

UTANGULIZI:
Elimu ni ujuzi, maarifa au utaalamu anaopata mtu kutoka kwa mtu, mashine au uzoefu kutoka katika mazingira aliyopitia.

Hata hivyo elimu inaweza kuwa Rasmi au isiyo rasmi. Elimu rasmi ni aina ya elimu inayohusisha usajili wa wanafunzi na kuwaweka darasani kwaajili ya kujifunza kwa kutumia mitaala ya kielimu. Elimu isiyo rasmi ni Elimu anayopata mtu kutoka kwa watu au mazingira yanayomzunguka bila kuhusisha usajili na kuingia darasani.

Hapa nitajikita kwenye "elimu rasmi" katika mfumo wetu wa Tanzania.
ELIMU RASMI KWA TANZANIA BADO HAIJAKIDHI MAHITAJI YA JAMII ZETU KIKAMILIFU.

Jamii zetu ni jamii za wakulima, wafugaji na wafanyabiasha na baada ya Elimu ndipo tunapata jamii ya Wafanyakazi.

Kwa mjibu wa takwimu za sensa ya mwaka kilimo, mifugo na uvuvi za 2019/20 inaonyesha kua Tanzania zaidi asilimia 65 ya kaya za Tanzania wanajihusisha na kilimo. Asilimia hii ni idadi kubwa ya watu.
Lakini kitu cha kushangaza mbali na asilimia ya watu wanaojihusisha na kilimo Tanzania ni kubwa, somo la kilimo halifundishwi mashuleni kama somo linalojitegemea na la lazima.​
Picha: Takwimu za sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/20


KWANINI KILIMO KIWE SOMO LINALO JITEGEMEA NA LA LAZIMA?

• Kwanza kabisa, Idadi ya watanzania wanaohitimu elimu na kuingia katika shuguli za kilimo ni kubwa. Wahitimu hawa wanaweza kufanya uzalishaji katika shughuli za kilimo na zikasaidia kukuza kipato chao na Taifa Kwa ujumla

• Pili, Kilimo Kama biashara; Kama kilimo kitafundishwa kama somo la lazima kuanzia kidato cha pili hadi cha nne kitamsaidia mhitimu kukifanya kilimo kama biashara kwa kufanya uzalishaji wa kilimo cha kisasa na kisha kuuza mazao yao.

Wakati nchi nyingi duniani zikilia kuhusu njaa; kama watanzania watajifunza kilimo cha biashara, hii itakua fursa kubwa kwao kuuza mazao yao na kupata faida. Tanzania imebarikiwa aridhi nzuri, kubwa na yenye rutuba, ni wakati sasa wa serikali kuangalia fursa hii na kuingiza somo la kilimo mashuleni.

• Tatu, Kilimo kama ajira; Hii ni sababu nyingine ambayo inaweza kufanya Somo la Kilimo liwe la lazima kwakua kilimo ni ajira kubwa kwa watanzania wengi. Wakati vijana wakihitimu elimu zao na kurudi mtaani kuhangaiga hii inaweza kuwa mbinu mbadala ya kukabiliana na tatizo la ajira

• Nne, Kukuza pato la Taifa; Kama somo la kilimo litaingizwa katika mtaala wa elimu kama somo linalojitemea na la lazima, vijana wataziona fursa zilizopo katika kilimo na kuingia kufanya kilimo cha biashara, katika biashara serikali itapata mapato kupitia kodi na ushuru na hiyo pato la nchi litapanda na kupunguza utegemezi.

NINI KIFANYIKE SASA?

Yafuatayo ni mapendekezo ya namna ya kufanya ili Somo la Kilimo lilete matokeo chanya:
Kwanza Somo la kilimo lifundishwe kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari, kidato cha nne kama somo la lazima.

Pili wanafunzi waondolewe dhana au saikolojia ya kusema kilimo ni mateso au ni kazi ya watu masikini wasio na elimu na badala yake waelekezwe kuwa kilimo ni fursa ya kibiashara na ajira.

Tatu Katika mtaala; Wanafunzi wajifunze kilimo cha kisasa na kilimo cha jembe la mkono.

Hapa ndipo kwenye kiini; Mwanafunzi aelekezwe kuhusu Mambo yafuatayo:
flyerdesign_07072023_222340.png
kilimo cha jembe la kukokotwa na wanyama kama vile punda na ng'ombe,
Kilimo cha kutumia mashine kama vile trekta
Kilimo cha umwagiliaji
Kilimo cha jembe la mkono​


Vilevile Katika kilimo Wanafunzi Wajifunze kuhusu ufugaji, Hapa katika ufugaji wajifunze ufugaji wa kisasa na wa kienyeji ilinkugusa mazingira ya wanafunzi wote na wa hali za kipato tofauti tofauti.
Ufundishaji katika ufugaji ukikite katika makundi mawili:​
Kwanza, Ufugaji wa wanyama kama vile Ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k
Pili ufugaji wa ndege kama vile: kuku, bata, njiwa, tausi n.k​


Katika Kilimo; Kilimo cha mazao na ufugaji wanafunzi waelezwe fursa zilizopo na namna ya kuzitumia.
Somo lieleze changamoto zilizopo katika kilimo na ufugaji na namna ya kuzitatua.

NINI WAJIBU WA SERIKALI KUHAKIKISHA WAHITIMU WANANUFAIKA NA SOMO LA KILIMO?

Baada ya somo la kilimo kuingizwa kwenye mtaala ni wajibu wa serikali sasa kuhakikisha wahitimu wanaohitaji mikopo wanaipata kwa urahisi ili kuendeleza shughuli za kilimo

Pili serikali ihakikishe pembejeo za kilimo zinapatikana kwa unafuu, hapa nasisitiza kuhusu utoaji wa Ruzuku za mbolea na viuatilifu vya kuua wadudu wahalibuo mazao na kushambulia mifugo.

HITIMISHO:
Kwakua kilimo ni uti wa mgongo wa taifa la Tanzania ni wakati sasa wa serikali kupitia wizara ya Elimu kuangalia namna ya kuingiza somo la kilimo katika shule zote na kufundisha somo hili kwa weredi ili kusaidia kukabiliana na umasiki ambao ni adui mkubwa na pia kupunguza Tatizo la ajira.​

Imeandaliwa na: Mapato Sigumwes
Simu: +255745922142
Email: officialmapatotz@gmail.com




 
Back
Top Bottom