MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Nikiwa naendelea kumpa Miryam bembelezo kwa kusugua mkono na bega lake taratibu, mlango wa kuingilia hapo chumbani ukafunguka, nami nikatazama hapo na kumwona Ankia akiwa amesimama. Bila shaka ndiyo alikuwa amerudi, na inaonekana alikuja moja kwa moja mpaka humu chumbani kutuangalia mimi na Tesha, lakini akakuta niko na dada mtu.

Miryam akawa amemwona pia, naye akajitoa begani kwangu na kuanza kujifuta machozi kwa viganja vyake. Ankia alikuwa amesimama hapo mlangoni akitutazama kama vile anasubiri maelezo.

"Ndiyo umerudi?" nikamuuliza hivyo.

"Ee... ndiyo nimefika. Kila kitu kiko sawa jamani?" Ankia akauliza hivyo kwa kujali.

Miryam akasimama baada ya kujikausha machozi, nami nikasimama pia. Akasema, "Ndiyo, nimemwijia Tesha."

"Yuko wapi?" Ankia akamuuliza.

"Ameingia uani. Ngoja niende nikamsubiri hapo nje," Miryam akasema hivyo.

Nilikuwa namtazama tu kwa utulivu, naye akaanza kuelekea mlangoni lakini Ankia akamshika mkono kumzuia. Sote tukamtazama.

"Nime... nimeleta supu. Kaa basi tunywe pamoja na mdogo wako, eti?" Ankia akamwambia hivyo.

Miryam akasema, "Sitaweza Ankia. Naingia kazini, nataka nikajiandae. Ila Tesha anaweza kubaki, na...."

"Ankia umerudi?" Tesha akawa amefika na kusema hivyo.

"Eee. Namwambia dada yako tunywe supu, nimeleta nyingi, ila anataka kuwahi kazini..." Ankia akasema.

"Aaa, Mimi... kunywa tu hata bakuli moja. Sikumbuki mara ya mwisho tumekunywa supu pamoja..." Tesha akamwambia hivyo dada yake.

Ankia akatabasamu na kusema, "Ee bwana, hata bakuli moja tu. Ngoja nikaweke, sawa?"

Miryam akaonekana kutaka kumridhisha mdogo wake, hivyo akatikisa kichwa kukubali.

"Haya twendeni jamani. JC... njoo," Ankia akaniita.

Nikatikisa kichwa kukubali, nami nikafata nyuma yao wote mpaka hapo sebuleni.

Hakukuwa na ile hali changamfu sana iliyozoeleka kutokana na uwepo wa Tesha, kwa sababu wakati huu alikuwa chini ya mvurugo wa kihisia. Angalau Ankia angeongea kwa njia nyepesi ili kurudisha hali iliyosawazika zaidi kwa sehemu hiyo. Kulikuwa na hotpot mezani na mfuko wenye kitu kwa ndani, naye Ankia akawa ameleta sahani ya udongo na mabakuli manne pamoja na vijiko.

Kwenye ule mfuko akatoa chapati sita za kusukumwa na kuziweka kwenye sahani, akisema ndizo zilizofanya akakawia kiasi kwa sababu ya kuhitaji kusubiri. Akaweka na supu kwenye mabakuli, nyama zikiwa zile zifananazo na maini (wanaita mapupu), naye akatusogezea kila mtu sehemu yake na kumsisitizia Miryam anywe na kula chapati.

Nilikuwa namwangalia mwanamke huyo na kuona namna alivyojitahidi kusitiri hisia zake. Kuna kitu kilichokuwa kinaisumbua nafsi yangu kutokana na kushindwa kumwambia maneno yenye kufariji alipokuwa anajilaumu kwa sababu ya matatizo yaliyokuwa yanatokea kwenye familia yake.

Hii ndiyo iliyokuwa mara ya pili kwangu kuweka ukaribu wa namna hiyo kwa huyu mwanamke, yaani vile nilivyombembeleza kidogo akiwa amenilalia begani, nikiwa nakumbukia mara ya kwanza aliponikumbatia kwa kutoa shukrani ya moyoni nilipomsaidia mdogo wake. Nilihisi kama ningeweza kujiweka karibu naye zaidi ili tushirikishane katika mambo yenye kujenga zaidi, lakini tatizo alikuwa wa kivyake mno.

Tukawa tunakunywa thupu, taratibu tu, naye Tesha akawa anasimulia kwa wanawake jinsi alivyojikuta anakabwa na vibaka na kuibiwa simu; bila kuongelea masuala ya wanawake aliokutana nao bar lakini. Akatania kwa kusema alitaka kurudi huko leo na kisu ili akawatafute hao vibaka, nasi tukamwambia awe mwangalifu kisije kikageuziwa kwake.

Kwa hiyo maongezi hapo yalikuwa mepesi tu mpaka tulipomaliza supu, Miryam na mimi tu ndiyo tukiwa tumekula chapati moja moja, kisha yeye na mdogo wake wakatuaga na kuelekea kwao. Tesha alikuwa anataka kwenda kuuweka mwili wake sawa zaidi ili baadaye nimsindikize kwenda kituo cha polisi kuangalia suala lake la simu, nami nilikuwa nimemwambia haina tatizo.

Bila shaka, wawili hao wangeenda kujaribu kuweka hali vizuri zaidi pale kwao, lakini bado nilikuwa na hofu kuelekea suala la huyo Joshua. Sikutaka kuwachanganyia habari kwa kuwaambia mambo niliyosikia huyo mjinga akisema, maana najua ningeizidisha tu hofu ya Miryam kutokana na vitu ambavyo mdogo wake angeweza kufanya.

Kwa sasa ingekuwa busara kutulia tu, lakini ningehakikisha nakuwa makini ili kuiepusha familia hiyo kutoka kwenye matatizo ambayo Joshua alitaka kuyaendeleza; hasa kumlinda Mariam.

★★

Muda mfupi baada ya Miryam na Tesha kuwa wameondoka hapa kwa Ankia, nikawa nimefanya usafi wa chumba na mwili, kisha nikavaa vizuri ili niweze kwenda pale kwao kushughulika na binti Mariam.

Ni leo ndiyo nilitaka kumpa Ankia hela ya kodi kwa ajili ya mwezi uliofuata, basi tu yaani ili wiki ambazo zingefuata nisiwaze kabisa kuhusu hilo suala. Nilipotazama matumizi yangu ya pesa za pembeni toka nimekuja mapumziko, nikaona nilikuwa nimetafuna nyingi kiasi, lakini hakukuwa na shida sana juu ya hilo.

Baada ya kupangilia mambo vyema, nikamfata Ankia na kumpatia pesa. Kama kawaida yake, alianza kujishaua mara JC mbona hivi, mbona vile, nami nikalazimisha azichukue na kumwambia akate mashauzi yake. Nikamuaga baada ya hapo, nikisema ndiyo naenda kwenye wajibu wangu wa kidaktari, nami nikaelekea mpaka kwa jirani yetu.

Tesha akawa amekuja kunifungulia geti, naye akasema kitu ambacho hata Bi Zawadi aliwahi kuniambia mapema sana kuhusu geti hilo. Ni kwamba kama mlango mdogo wa geti ungekuwa unaweza kufungukia kwa nje basi ningekuwa naingia tu badala ya kusumbuka kupiga hodi, hivyo nikaona nisaidie kuirekebisha hali hiyo kidogo.

Nikamwomba Tesha atafute kamba nyembamba, msumari, na nyundo ikiwezekana ili tujigeuze mafundi hapo. Akatii na kufata kamba nyembamba iliyoendana na zile walizoweka hapo nje kwa ajili ya kuanikia nguo, msumari mrefu, lakini hakukuwa na nyundo. Akaleta tu jiwe.

Nikaikata kamba hiyo kwa urefu uliotoshea upana wa kimlango hicho, kisha nikaifunga kwenye kale kadude ka kuvuta kwenye kifungio cha geti na kuipitisha nje kupitia uwazi mdogo mwanzoni mwa ukuta ambapo geti lilianzia. Nikatoka nje na kuugonga msumari ukutani, mwanzoni kabisa karibu na geti, kisha nikaifunga kamba hapo.

Tukaanza kufanya majaribio kwa kufunga kimlamgo cha geti, kisha naivuta kamba kiasi nikiwa kwa nje ili ikikivuta kile kidude kwa ndani, kiachie, na huo mlango ukafunguka. Akili mtu wangu! Ilikuwa ni njia ndogo tu ya kurahisisha kazi kwa sisi tuliozoea kuja hapo, naye Tesha akasema ilikuwa ni njia nzuri sema aliona uvivu tu kushughulika na geti hilo.

Nikaingia tena, na wakati huu ndiyo nikatilia maanani kuwa gari la Miryam halikuwepo, kumaanisha alikuwa ameshakwenda kazini. Nikamuuliza Tesha hali kwa sasa ilikuwaje, naye akaniambia tu twende ndani ili tukaongelee huko.

Kweli tukaenda, nami nikakuta hali isivyo kawaida na nilivyokuwa nimezoea. Sikuwakuta Bi Jamila na Bi Zawadi wakiwa wamekaa kwenye sofa lao kama kawaida, na sikumwona Mariam pia. Nikadhani labda wapo chumbani maana kulikuwa na hali ya utupu hapo.

Tukakaa na Tesha sofani, nami nikamuuliza, "Mariam yuko poa?"

"Eeh, ila ndo' hayupo. Wote hawapo," akasema hivyo.

"Wapi tena?"

"Da' Mimi kawachukua kuwapeleka kwa Joshua. Wakaongee huko," akasema hivyo kwa njia ya kukerwa.

Nikamwangalia kwa umakini na kuuliza, "Kampeleka Mariam kwa Joshua?"

"Ndo' maana yake."

"Lakini si Miryam amesema anaenda kazini?"

"Ndiyo, kawapeleka huko wote na mama wakubwa, halafu ataenda kazini... labda na baadaye ataenda tena huko... kuwafata."

"Mbona we' hujaenda?"

"Kwani haiko wazi? Sitaki tu. Lakini nimesingizia kwa dada kwamba sijisikii fresh bado. Hapo wanaenda kudanganywa-danganywa tu na huyo fala."

"Aisee! Yaani akimgusa Mamu, atanitambua," nikajikuta nimesema hivyo kwa hasira.

"Nini? Nani, Joshua? Anataka kumuumiza Mamu?" Tesha akaniuliza hivyo kwa mkazo.

Nikamwangalia na kusema, "Aa... hapana, yaani namaanisha... hali ya Mariam siyo nzuri kivile bado, ikiwa ataogopeshwa sana na kaka yako itakuwa kurudi nyuma tena. Nimeongea tu vibaya."

"Siyo vibaya, me mwenyewe nitamuua huyo mjinga ikiwa Mamu atarudi hapa bila unywele hata mmoja. Sema ndiyo nimemwahidi dada kuwa mpole, kwa hiyo natulia tu."

"Ila ungeenda nao Tesha, huwezi kujua," nikasisitiza.

"Usiogope bro. Me najua Joshua anachokifanya hapa mwanzoni ni kuigiza tu, kwa hiyo lazima na mimi niigize pia. Hawezi kumgusa mtu yeyote sa'hivi, utaona," akanihakikishia.

Nikaangalia pembeni nikiwa nimeudhika kiasi. Sikujua nifanye nini maana hali hii ilikuwa ya kushtukiza, na hii ikanipa somo kuhusu kuwa chonjo zaidi na hii familia ili Joshua asije kufanikiwa kwenye mipango yake, mimi nikabaki tu mdomo wazi.

"Wanarudi saa ngapi?" nikamuuliza hivyo.

"Jioni. Hapa doro tu kaka. Nataka nikazurure wee mpaka hiyo jioni," akaniambia hivyo.

Nikatulia tu na kushusha pumzi.

"Oy... kama vipi tuoshe, ama nini?" akaniuliza.

"Kuelekea wapi?"

"Nataka nikazunguke Kigamboni leo. Halafu baadaye tutazamia kwa mshkaji fulani hivi, nina siku sijamwona. Unasemaje?" akasema hivyo.

Lengo la kuja hapa ilikuwa kuendelea na mazoezi yangu pamoja na Mariam, lakini hakuwepo. Sikuwa na jambo lingine muhimu la kufanya kwa hiyo nikaona nimkubalie tu rafiki yangu. Labda na matembezi yangeleta jambo jipya mbali na yale niliyokuwa natazamia yafike.

Alikuwa ameshaoga kwa hiyo nikakaa kumsubiri alipokwenda kuvaa. Alivalia kawaida tu kama mimi, na kofia yake kama kibandiko kichwani ikanifanya na mimi nitake kwenda kuichukua ya kwangu, lakini nikaahirisha.

Tukatoka pamoja, akafunga milango na geti, nasi tukaenda kwa Ankia ili Tesha amwachie funguo za kwao ili endapo kama ndugu zake wangewahi kurudi kabla yake basi wazikute hapo. Ankia akatutakia matembezi mema huku akisema tukirudi tumletee zawadi, nasi tukaingia barabarani baada ya hayo.

★★

Basi, tukawa tunatembea mdogo mdogo kuelekea Mzinga. Baada ya kufika Mzinga, kibishoo tu yaani, tukaamua kuifata Kongowe kwa kutembea pia. Mwendo wa taratibu tu, huku tukipeana story nyingi za mambo yetu wanaume ukatufikisha mpaka hapo Kongowe, na hii ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika eneo hilo tokea nimepajua Mzinga; na hata Mbagala pia.

Mwanzoni mwa eneo hilo kunakuwa na sehemu nyingi zenye biashara ndogo na kubwa za wajasiriamali sanasana, nasi tukaelekea upande ambao daladala zingesimama kwa ajili ya kubeba abiria. Tukakuta moja ambayo ilikuwa ikielekea Kigamboni ndiyo, nasi tukaingia na kukaa siti za nyuma kabisa. Mwonekano wangu na Tesha ungefanya watu wafikiri sisi ni ndugu wa damu labda, maana kuna sehemu kubwa ya pigo zetu iliyokuwa inafanana sana.

Tukiwa tu ndiyo tumekaa, Tesha siti ya dirishani kabisa na mimi pembeni yake, nikapokea ujumbe kutoka kwa mtu ambaye sikuwa nimetarajia kabisa kwa muda huu. Ilikuwa ni Adelina, dada mkubwa wa Joy; ama niseme marehemu Joy.

Yaani tokea tumebadilishana namba pale msibani sikuwahi kumtumia salamu hata mara moja, ijapokuwa nilikuwa kwenye harakati za kumtafutia mdogo wake haki kwa mauaji yaliyomsibu. Alikuwa ametuma salamu fupi, 'habari yako,' nami nikatuma jibu kuwa 'niko salama' na kuuliza yeye aliendeleaje.

Nikaanza kumsikia konda kutokea nje akisema kwa abiria fulani waingie kukaa, kwamba siti hazikuwa zimeisha. Yaani alikuwa anawashawishi kwa kusema tena kuna waarabu ma-handsome wamekaa huko mwishoni, na ndiyo Tesha akanishtua nitazame nje.

Nikaangalia kupitia kioo na kuona wanawake wawili pamoja na mwanaume kijana mmoja, wote wakiwa ni waislamu, na mwanamke mmoja alivalia yale manguo meusi yanayoficha mpaka uso kasoro macho, lakini kale kengine uso ulikuwa wazi tu na kuzungukiwa kwa hijab kichwani. Kalikuwa kembamba, keupe, kenye macho mazuri kweli, na nahisi wao walikuwa waarabu kasoro huyo mwanaume kijana aliyekuwa mweusi kabisa; akionekana kuwa mwandamani wao.

Huyo mwanamke aliyeficha uso alikuwa kama hataki kuingia kwa kuwa labda hakupenda kukaa mwishoni, naye Tesha akawa ananishurutisha tufanye jambo ili hako kadada kaingie maana alikuwa amekaelewa tayari. Adelina akawa amenitumia ujumbe akisema yuko poa na kuuliza kama bado nilikuwa Mbagala, naye Tesha akaendelea kunibonyeza-bonyeza mpaka nikahisi kero.

Agh, nikasogea kufikia uwazi wa kioo na kuwaangalia wanawake hao, nami nikasema, "Dada, ingieni tu. Nafasi ziko tatu, yaani kama vile zimebaki kwa ajili yenu tu."

Mwanamke aliyekuwa amefunika mpaka uso akawa ananiangalia sana, naye konda akaongeza spidi ya kuwashawishi.

Nikakaa sawa tena na kumwambia Tesha, "Nimeweka jitihada hiyo kama ulivyotaka. Umefurahi?"

Akacheka kidogo na kusema, "We' ni chizi! Ndo' mpaka utuchoreshe? Ona washamba wanavyotuangalia."

"Unasumbua mno," nikamwambia hivyo nikiwa makini na simu.

Nikamjibu Adelina kwamba bado niko Mbagala ndiyo, na kumuuliza kama alisharudi Mbezi. Tesha akanibonyeza kidogo, nami nikaangalia mbele na kuona wale wanawake wameshapanda na kuja upande wa nyuma. Yule mwanaume kijana hakupanda, inawezekana labda alikuwa anawasindikiza tu, nao wakaja kukaa pamoja nasi; nafasi iliyobaki ikiwa imetutenganisha katikati.

Kale kadada kenyewe kakawa dirishani kabisa, huyo mficha uso akiwa pembeni yangu, nami nikamtazama Tesha na jamaa akajikausha tu kama vile siyo yeye aliyenisisitiza kuwashawishi waingie. Inaonekana kwa muda huu abiria waliokuwa wanataka kuelekea huko mbele walikuwa wachache, kwa sababu hakukuwa hata na mtu aliyesimama na safari ikaanza.

★★

Vuuu, mwendo ukaendelea huku na mimi nikiendelea kuchat na Adelina. Ilianza kidogo kidogo tu lakini mpaka ikafika hatua tukaanza kutaniana, kirafiki yaani. Akawa ameniambia kuwa kwa sasa hivi alikuwa amekwenda pale Mbagala kwa rafiki yake mmoja kumsalimia na ndiyo alifikiria uwezekano wa kupata nafasi ya kuja kunitembelea mimi na Ankia pale nyumbani.

Unajua, mpaka leo Adelina alikuwa anafikiri mimi ni mume wake Ankia, ndiyo ikabidi nimwambie kwamba ile ilikuwa danganya toto tu niliyofanya pamoja na Ankia; wala hata hakuwa mke wangu, na ndiyo matani baina yangu na Adelina yalianzia hapo.

Mwendo ulikuwa mrefu kiasi kuelekea Kigamboni, mara kwa mara watu wakiongezeka kwenye gari na kupungua, na uvumilivu ulikuwa unamshinda Tesha. Alitaka sana kuipata namba ya kale kadada keupe pembeni yetu, lakini alihofia kwamba huenda huyo mwanamke mwingine alikuwa mama yake kwa hiyo kungekuwa na utata.

Lakini akawa ananishawishi kwa kunitumia sms nijaribu kumsemesha maana alikuwa na uhakika kwamba mwanamke huyo aliingia tu kwenye gari kwa sababu yangu, nami nikamwambia Tesha aache umalaya la sivyo ungekuja kumuua siku moja.

Kama ninavyosemaga, mimi siyo mtu wa kuogopa mtu kabisa, na kama ningekuwa nataka kupata namba za mwanamke yeyote niliyekutana naye, ningezipata. Ila kuanza kumwelezea Tesha kwamba nilikuwa sitaki tu najua ingegonga mwamba, na hata hivyo nilikuwa nataka rafiki yangu huyu ajisikie vizuri tu baada ya mambo yote aliyokuwa amepitia jana, kwa hiyo nikamwambia atulie ili nimrekebishie mitambo.

Adelina bado nilikuwa nachat naye, akiwa amesema kwamba anaweza hata akaja leo kunitembelea mimi na Ankia pale nyumbani, nami nikaona nimjibu kwanza. Nikamwandikia kuwa kwa sasa nilielekea Kigamboni kwa hiyo endapo kama alikuwa na mpango wa kwenda kwa Ankia muda huu, asingenikuta, lakini labda kama ni jioni ndiyo tungeweza kuonana.

Ilishangaza kiasi kwamba hakuwa hata amemtafuta Ankia bado kuongelea suala la kwenda kumtembelea ilhali walikuwa ni marafiki, lakini labda ni kwa sababu tu hakuwa amewahi kuwasiliana nami kabisa, na kule kudhani mimi ndiyo kichwa sasa pale kwa Ankia.

Nilipomaliza kumweleza, nikamtazama mwanamke yule mwislamu. Hilo baibui jeusi alilovaa lilificha uzuri wa ngozi nyeupe aliokuwa nao, maana nilitazama vidole vyake vyenye kucha ndefu kidogo na nyekundu, vilivyoshikilia simu ya macho matatu, na kiuhakika nikaona kwamba havikuwa na hata chembe ndogo ya sugu nyeusi. Sijui walikuwa waarabu kweli?

Tesha akanibonyeza tena na kunipa ishara kwamba eti nichangamke, nami nikatabasamu kiasi na kufungua simu yangu tena upande wa sms.

Nikaandika pale patupu hivi, 'Habari? Naomba namb yako kam hutojal'

Nikanyoosha simu kwa chini kumwelekea mwanamke huyo, naye akaitazama. Sikuwa hata nikimwangalia lakini nikamwona akinyanyua uso wake kuniangalia, hivyo na mimi nikamwangalia. Huwa naweza kuweka macho fulani hivi ya kumvuta mwanamke aamshe upendezi kunielekea, macho ya ushawishi yaani, nami nikawa namtazama kwa hiyo njia.

Akaangalia mbele tu kama vile hataki, kisha akaichukua simu yangu kichinichini na kuiunganisha na yake. Nilikuwa nimeweka uso makini, nikiona wazi jinsi Tesha alivyojikausha kwa kujifanya anatazama nje tu, na kwa jicho la mbali nikaweza kuona mwanamke huyo anaandika kitu fulani kwenye simu yangu.

Kisha, akaitelezesha simu kwenye hiyo siti kuelekea upande wangu bila kuitazama, kukiwa na pete nene zenye kuonekana kuwa kama za dhahabu kwenye vidole vyake viwili, nami nikaipokea nikiwa nimeweka mwonekano makini bado. Mambo ya siri hayo, na Tesha ndiyo akawa ameniingiza majaribuni!

Wanawake wa hivi nawaelewa sana, yaani wanapoamuaga kujitafutia vitulizo vya nje huwa wanapenda mno usiri wa hali ya juu, na huyu inaonekana alikuwa amenielewa sana ndiyo maana akakubali kufanya hivyo akiwa pembeni ya binti yake, sijui mdogo wake, sikujua.

Tesha akakunja ngumi yake karibu na paja langu, akiwa anataka tugonge tano ya ushindi, nami nikaweka kiganja changu hapo huku nikimnyanyulia kidole cha kati. Nikatazama simu yangu na kukuta namba za simu zikiwa zimeandikwa hapo, nami nikazitumia ujumbe.

'Jina lako mremb?'

Nikajikausha kama simwangalii, nami nikaona anaandika kitu fulani kwenye simu yake kisha akatazama pembeni.

Ujumbe ukaingia kwenye simu yangu, namba hiyo hiyo, ukisomeka, 'niambie lako na wew.'

Nikajibu, 'JC'

'Ndiyo nn'

'Ndiyo my name'

'Me naitw Ibtisam'

'Ooh saw. Jina lako zur kam wew mremb'

'Uremb wang umeon wp'

Nikiwa bado sijajibu ujumbe wake huo ndiyo tukawa tumeingia maegesho ya daladala kwenye eneo la Kigamboni, na watu wakawa wanasimama ili washuke.

Nikamwandikia hivi, 'Ngj tushuke nikwambie'

Kweli tukaanza kushuka mpaka nje, nami pamoja na Tesha tukaenda upande wa nyuma wa gari na kuwaangalia wanawake hao waislamu. Wenyewe wakaelekea upande mwingine kwa pamoja, huku kale kembamba kakigeuka kututazama mara moja.

Nikaangalia simu na kukuta ujumbe wa huyo mwanamke akiwa amejibu, 'Saw, lkn ntakuchek badae. Kun shm naend sahiv'

Tesha akaniuliza, "Oy, umemwambiaje? Anasemaje?"

"Kaka utakuja kuniweka matatizoni siku moja!" nikamwambia hivyo.

Tukaanza kutembea kuelekea sehemu iliyoturuhusu kuiona vyema Bahari ya Hindi.

"Kwani vipi?" akaniuliza.

"We' kila demu unataka tu, wengine ni majini."

"Ahahahah... me kwani nilikwambia namtaka huyo jini wako? Mimi nilikuwa nakataka kale kengine, we' si umechukua namba ya huyo maza'ake kwa upendo wako?"

"Nimeomba namba yake ili uje kuipata ya hako unakokataka. Halafu Tesha!"

"Hahahah... JC bana! Kwo' jini linasemaje?"

"Atanicheki baadaye, na linaonekana limeolewa. Ah, sijui hata kwa nini nimemwomba namba!"

"Si kwa ajili yangu? We' ukishamzuzua utanifanyia unyama na mimi nipate ya hako kengine. We' utakula mazeli, mimi kimweli. Tena tutafanyia kwenye double deka kabisa."

Nikacheka kidogo tu na kusema, "Tesha tunaingia Kigamboni, wanawake wazuri kama wote, utawasahau hao uliowaona. Tulia mdogo wangu."

"Ah, kwenda huko! Huu ndiyo wakati wangu, we' ushazeeka ndo' maana. Twende tukapande meli huko."

Nikacheka na kutikisa kichwa, nami kweli nikaanza kumfata.

Tukapita sehemu nyingi zenye biashara, watu wengi, wadada wazuri ndiyo usiseme, nasi tukaelekea sehemu ya kununulia kadi za tiketi kwa ajili ya kuvuka bahari kwenda upande wa pili wa Kigamboni; ule wenye majengo ya ukweli. Tesha akapata kadi, nasi tukaenda kuvuka kwa kupanda meli ndogo ya uvukishaji abiria na magari. Watu walikuwa wengi kufikia kiasi kilichohitajika, na wakati tukiwa tumeanza kuvuka mvua ikaanza kunyesha.

Mpango ulikuwa kwenda kuzurura sehemu kadha wa kadha kwa eneo hilo, lakini mvua ikaongezeka mno kiasi kwamba jambo hilo likaingiwa na utata. Yaani ile tumeshuka tu, ikatubidi tuingie kwenye daladala ambazo zilielekea Kariakoo, na safari ikaanza tena. Hii haikuwa mara ya kwanza kutembelea Kigamboni na hata niliwahi kutoka na mwanamke fulani aliyekuwa wa pande hizi, ila hiyo ni hadithi nyingine, ya kusimuliwa kwa wakati mwingine.

★★

Mwendo wa dakika kadhaa ukatufikisha mpaka Kariakoo, na kwa huku mvua ilikuwa ishakatika. Tukashuka, Tesha akiwa bado anawashwa kutembea, hivyo tukachukua mwendokasi na kwenda pande za Ubungo. Tukazurura wee, Tesha hata akanipitisha kule alikokuwa anaenda kufata wanawake wa kulipwa, chimboni yaani, naye akawa akisema hizo mishe siku hizi hafanyi.

Tukatoka huko na kuzunguka mpaka Uhasibu, nasi tukashukia hapo. Tesha alikuwa na rafiki yake mwanachuo aliyekaa eneo la Uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo tukatembea mdogo mdogo kuelekea huko. Alikuwa ameshawasiliana naye. Yaani safari hii yote leo ilikuwa ni kwa udhamini wa Tesha, mimi ndiyo nilikuwa kama mtalii wake, nasi tulipokuwa tu ndiyo tumeyapita malango ya uwanja nikaanza kuona mdada fulani akija upande wetu taratibu.

Tesha alikuwa ameniambia kwamba tunaenda kumsalimia tu mshkaji wake, kwa hiyo sikuwa nimetarajia kwamba ingekuwa ni mwanamke mpaka mdada huyo alipotukaribia na kukumbatiana na Tesha kirafiki. Alikuwa mfupi kiasi, mweusi, mwili wa kawaida tu, na tabasamu lake lilionyesha mwanya mdogo katikati ya meno yake ya mbele.

Wakawa wanasemeshana kirafiki sana, naye akaniangalia na kunisalimu pia. Alikuwa mchangamfu sana, jina lake ikiwa ni Dina, naye akatuongoza kuelekea pale alipoishi. Ilikuwa ni kwenye zile nyumba za wapangaji zilizojaa hasa wanafunzi wa chuo, nasi tukaingia kwenye chumba chake.

Kilikuwa simple tu, safi, godoro chini kwenye sakafu ya vigae, friji ndogo, begi la nguo pembeni ya shehena ndogo ya vyombo, vifaa vya mapodozi na manukato, viti vitatu vya plastiki. Jiko dogo la gesi lilibeba sufuria lenye chakula kwa ndani bila shaka, nasi tukakaa na kuanza kupiga story.

Mimi nilikaa kwenye kiti, Tesha na Dina wakakaa kwenye godoro, na ni wao sanasana ndiyo walioongea huku mimi nikichangia mada mara moja moja kukoleza ucheshi. Dina akaniuliza natumia soda gani, nami nikamwambia Pepsi. Tesha vilevile akasema Pepsi ingawa alitania kutaka bia.

Dina akatoka kwenda kufata soda, nasi tukabaki hapo, nikisikiliza maneno ya kipuuzi ya Tesha kuhusu jinsi nilivyotakiwa kubaki hapa leo ili nifanye jambo fulani na Dina. Ni hapa ndiyo nikawa nimepokea ujumbe kutoka kwa yule mwanamke mwislamu tuliyekutana kwenye daladala, akiwa ametuma tu 'mambo,' nami kabla hata sijamjibu, simu yangu ikaanza kuita. Mpigaji? Bertha. Hatimaye!

Sikutaka Tesha asikie jambo lolote ambalo lingemfanya atambue nani naongea naye, hivyo nikapokea nikiwa nimejihakikishia kutosema lolote litakalomshtua jamaa.

"Hallo?" sauti yake Bertha ikasikika.

"Hello, vipi?" nikasema hivyo.

"Poa. Uko wapi?"

"Niko kwa Mkapa hapa."

"Unafanyeje huko?"

"Nimekuja kwa mshkaji wangu, niambie..."

Tesha akaniuliza kwa ishara, "nani?" nami nikamwonyesha ishara pia kuwa atulie.

"Nataka uje. Au biashara uliyonayo sasa hivi huko ni muhimu sana?"

"Hakuna chochote muhimu zaidi yako dear."

"Usiniite dear, mazoea ya hivyo sitaki."

"Sawa dear," nikasema hivyo makusudi.

"Halafu wewe!" akasikika kwa ukali.

Nikajikaza nisicheke na kumwambia, "Pole, nimejikwaa tu. Ulimi hauna mfupa."

"Na nitakuja kuuwekea mfupa usipoangalia."

"Sorry."

"Toka huko sasa hivi. Niko Masai," akaniambia hivyo.

Ni muda huu ndiyo Dina akawa ameingia ndani tena, lakini wakati huu alikuwa pamoja na mwanadada mwingine mweupe, mwembamba, mrefu kiasi, aliyekuwa amevalia T-shirt nyeusi na suruali ya jeans ya samawati iliyobana. Nywele zake zilisukwa kwa mtindo wa dread nyeusi na fupi, naye akaenda kukaa godoroni baada ya Tesha kunyanyuka na kukaa kwenye kiti.

"Umeelewa?" Bertha akasikika kwenye simu.

Nikasema, "Eeh, nimeelewa. Ila... niko mbali kama hivi, naweza kuchelewa kidogo."

Dina akawa ametufungulia soda zetu na kutupatia, na ukimya mfupi uliofuata kwenye simu ukanifanya nitambue kwamba Bertha alikuwa amekasirishwa na maneno yangu.

Nikamwambia, "Ila nakuja. Nitakuwa nimeshafika muda siyo mrefu."

Likakata simu!

Kazi nilikuwa nayo. Nikashusha pumzi na kumwangalia Tesha, aliyekuwa akinitazama kama anasubiri nijielezee.

"Kuna dharura bro. Natakiwa nifike location mara moja," nikamwambia hivyo.

"Tumekuja wote, unataka kuondokaje mwenyewe bana?" Tesha akaniuliza kwa uthabiti.

"Iih, unataka kutukimbia?" Dina akaniuliza hivyo.

"Kuna dharura imetokea, nahitajika sehemu haraka ndo' maana..."

"Acha bangi! Hautoki hapa. Keki tamu kama hizi unakimbia kweli?" Tesha akasema hivyo kiutani.

Tukacheka kidogo, na Dina akamsonta huku akisema, "Afu' wewe!"

"Inanibidi tu kaka," nikamwambia Tesha.

"Jamani, mbona ghafla? Chakula hiki napakua," akasema Dina.

"Oh usijali Dina, niko poa. Labda umpakulie huyu mbwa," nikamwambia hivyo.

Akacheka kidogo, naye Tesha akasema, "Em' pakua mama, tule."

"Basi kunywa hata soda, imeshafunguliwa," akaniambia hivyo yule mdada mwingine.

"Ee, kunywa soda ndiyo uende kaka," Dina akaniambia.

"Poa," nikajibu.

Ingenibidi nipige hii soda fasta maana huyo Bertha hakuwa mtu wa subira hata kidogo, na hiki ni kitu ambacho nilikuwa nimekisubiria sana kwa hiyo wiki nzima kwa hiyo nisingeweza kuchezea nafasi hata kama ningepewa ofa ya utatu na hawa wadada!

Nikawa napiga fundo ndefu ndefu, huku nikiwa nimeanza kuchat na yule mwanamke mwislamu pia. Alikuwa mmoja kati ya wale wanawake ambao walipenda mtu aende moja kwa moja kwenye pointi ya kitu ambacho alitaka kutoka kwake, nami nikamwambia ndiyo, nilimkubali sana kutokana na kupenda macho yake na ngozi yake.

Akaniambia ooh nimeshaolewa, kwa hiyo ukinitaka lazima upande ngazi, nami nikamwambia hakuna ngazi za kupanda; ikiwa alinikubali pia basi tuje kucheza, lakini asipotaka basi sitalazimisha. Kwa kauli hiyo akawa ametulia kwanza, nami nikawa nimemaliza soda.

Nikamshukuru Dina na kusimama, Tesha bado akiwa analalama kuhusu mimi kuondoka, hivyo ikanibidi nitoe ahadi ya kuja naye tena kesho ikiwezekana kumtembelea rafiki yetu. Dina alipenda sana hilo wazo na kusisitiza nisije kuacha kuja, nami nikamwambia aondoe shaka. Huyo rafiki yake mwingine alikuwa akiniangalia sana kwa sura yake ya kiupole, nami nikamuaga pia nikiwa hata simjui jina.

Nikawaacha marafiki hao hapo na kuanza kuelekea barabarani, nikiwa natumaini kuwahi, na Tesha asijue kwamba sehemu niliyokwenda ilikuwa ni Masai. Angeshangaa sana!

★★

Nilifanikiwa kupata usafiri wa daladala zilizoelekea Mbagala, na mpaka kufikia huko tayari ilikuwa inaelekea kuingia saa moja. Nilikuwa nikijiuliza ni kwa nini madam Bertha alikuwa ameamua kuja Masai mapema sana leo, lakini hayo yote ningeyajua nikishafika pale.

Badala ya kuchukua daladala tena kutokea Rangi Tatu, nikaamua kupanda bodaboda ili niwahi zaidi, brrrr mpaka Mzinga, nami nikaunganisha moja kwa moja kufikia Masai, lakini nikaona nielekee kwa Ankia kwanza.

Nikafika hapo dukani kwa Fatuma na kumkuta huyo dada pamoja na wanawake wengine wengine wakiwa wamekaa kama kikundi cha kupiga umbeya, nami nikamwambia bodaboda anisubirie nikachukue mzigo ndani kisha anirudishe Masai upesi. Nikawapita hao wavaa dera kama siwaoni, nami nikaelekea mpaka ndani na kuingia.

Akili yangu ilikuwa imekazia fikira jambo moja tu kiasi kwamba mpaka nikashtuka kiasi moyoni baada ya kuingia na kumkuta Ankia akiwa amekaa pamoja na Adelina! Ile hali ya kutotegemea kumkuta mwanamke huyu hapa ingawa tulikuwa tumewasiliana ilikuwepo yaani, halafu nilikuwa kwenye kasi kwelikweli.

Wawili hao, baada ya kuniona, wakatabasamu kwa pamoja, nami nikatabasamu pia na kusogea karibu zaidi na walipokaa.

"Mume amerudi," Adelina akasema hivyo.

"Ee, baba mwenye nyumba ndiyo kafika," Ankia akasema hivyo pia.

Nikajikuta tu natenda bila kufikiri sana kwa kuinama na kumkumbatia Adelina, nami nikamwambia, "Karibu."

Nafikiri alikuwa ameshangaa kiasi lakini akaweza kucheka kidogo kwa pumzi, naye akasema, "Asante."

Nikamwachia na kusema tena, "Karibu sana."

Kisha nikaelekea chumbani, bila shaka nikiwaacha wanawake hao wanatazama haraka yangu.

Nikaingia chumbani na kutoa yale madawa niliyotengeneza, nami nikachukua kiasi kidogo na kukiweka kwenye karatasi tu baada ya kuwa nimekosa pa kuwekea, kwa kuwa sehemu niliyohifadhia dawa yote ilikuwa ndani ya mifuko minene; madawa yakionekana kama glucose. Nikachomeka hicho kikaratasi mfukoni, kisha nikaelekea sebuleni tena.

"Unatoka?" Ankia akauliza hivyo.

"Ndiyo, kuna sehemu nafika mara moja lakini... sikawii, nakuja. Sawa?" nikaongea hivyo nikiwa nimeelekeza fikira zangu kwa Adelina.

Akatikisa kichwa kukubali, naye Ankia akasema, "Unawahi nini kinachokutoa kijasho hivyo? Tuambiane..."

"Utajua tu, ngoja nirudi," nikasema hivyo na kuelekea mlango.

Nikawaacha wanawake hao wakicheka kidogo, nami nikaenda mpaka nje tena. Nikapanda bodaboda na kugeuza kuirudia Masai, nasi tukafika hapo huku sasa giza likiwa limeshaingia. Nikamlipa jamaa na kumwambia atokomee, kisha nikaelekea pale ndani.

Wanywaji walikuwepo na nafikiri kuna wahudumu wapya waliokuwa wameongezwa hapa na wachache niliowajua kuondoka, nami nikawa nimemwona Bobo pamoja na DJ fulani hivi wa hapo Masai. Nikamfata.

"Oyo, mchina..." akaniambia hivyo tukiwa tunagonganisha mabega yetu kirafiki.

Nikagongesha tano kwa yule DJ pia, kisha nikamwambia Bobo, "Oya umepotea kweli."

"Ah, mimi, wewe? Yaani hutokei Masai siku hizi mwanangu. Check watu wanavyokuangalia kama vile hujawahi kuonwa hapa," akasema hivyo.

Nikatabasamu na kusema, "Na mimi nimetingwa kaka, ila mdogo mdogo narudi. Ishu zinakwendaje?"

"Kama kawa budha. Oy... mtu wako yupo huko ndani," akaniambia hivyo kwa kuninong'onezea sikioni.

"Eeh, nimeona gari nje," nikamwambia.

"Yuko VIP, kamchangamkie..."

"Ndo' mpango mzima," nikasema hivyo.

Tukacheka tena pamoja, kisha nikamwacha hapo na kuelekea pande ya VIP. Na Bobo alikuwa sahihi kabisa, watu walikuwa wananiangalia kweli, lakini umakini wangu wote ulikuwa kumfikia huyo madam.

Nilipofika mlangoni, nikajiwekea hali ya utulivu, kisha nikaingia ndani hapo. Nikamkuta madam Bertha akiwa amekaa sofani, glasi yenye wine kiganjani, na kwenye sofa la pembeni alikaa yule baunsa wake; a.k.a shemeji.

Kama kawaida ya mwanamke huyo, alikuwa amependeza kwa kuvaa kigauni kifupi chekundu, kilichoyaacha mapaja yake meupe wazi kutokana na namna alivyokuwa amepiga nne, na inaonekana kilikuwa cha mgongo wazi. Wakati huu alishonea wigi la nywele za kizungu kichwani, na baunsa wake alikuwa amevaa kaushi tu na suruali nyeusi, akionyesha misuli yake imara.

Nikasogea usawa wa meza moja hapo, nami nikamtikisia kichwa jamaa kama salamu, naye akairudisha. Nikamwangalia Bertha, ambaye alikuwa akinitazama tu kwa utulivu, nami nikamwambia, "Nimefika madam."

"Umechelewa," akaniambia hivyo.

"Kweli? Mbona naona kama bado party haijaanza?" nikamuuliza hivyo.

Baunsa wake akamwangalia na kucheka kidogo, naye Bertha akawa amenikazia macho yake.

"Tupishe," Bertha akamwambia hivyo jamaa.

Baunsa akasimama na kuja upande wangu, naye akaniuliza, "Una ule unyama jembe?"

"Nakosaje labda?" nikamuuliza hivyo.

Akatabasamu huku akitikisa kichwa taratibu, nami nikaitoa ile dawa na kumfungulia.

"Si iko kama ile?" akaniuliza hivyo.

"Kwa asilimia zote," nikamwambia.

Akachovya kwa kidole na kulamba, kisha akatikisa kichwa kwa nguvu kiasi na kunishika begani. "We' dogo ni nyoko!" akaniambia hivyo.

Nikatabasamu kidogo, naye akanipita na kutoka ndani humo.

Nikabaki na madam. Alikuwa ananitazama kwa yale macho ya kuhukumu bado, naye akasema, "Njoo."

Nikatii na kumfata. Sikuwa na hofu kumwelekea huyu mwanamke, ila kujifanya mnyenyekevu sana ilikuwa lazima. Nikasimama usawa wa sofa alilokalia na kubaki mtulivu.

"We' vipi, si ukae?" akaniambia hivyo.

Nikasogea na kukaa kwenye sofa karibu yake.

Akawa ananitazama sana, naye akasema, "Yaani hiyo sura! Kama mwanamke!"

Dah! Kashfa hizo.

Nikatabasamu kwa kujilazimisha na kusema, "Asante. Moja kati ya silaha zinazonisaidia kupita huku na kule ni hii sura."

Akacheka kwa mguno, kisha akaweka glasi yake pembeni.
"Nimekufatilia kwa hiyo wiki dogo, naona una maisha magumu sana mpaka ukaamua kutoka Goba Center kuja kuishi Mbagala," akaniambia hivyo.

Umeona sasa? Nilikuwa sahihi. Huyu mwanamke alikuwa amefanya uchunguzi kunihusu mpaka kujua kitu ambacho bado sijaelezea kujihusu. Nikataka kujua anaelewa mambo mengi kadiri gani kuhusu maisha yangu.

"Ahah... eeh... maisha magumu. Nimekaa sehemu nzuri lakini... hazijanifiti ndo' maana nimeangukia huku sasa hivi," nikaongea hivyo kiupole, ikiwa kimtego zaidi.

Akasema, "Me sijali ulikuwa unaishi vipi. Nataka tu ujue nikiamua kukuharibia maisha yako endapo kama utanigeuka basi sitosita kuanza hata na familia yako."

"Usiwe na hofu juu ya hilo madam. Siwezi kukusaliti. Kwanza... familia yangu iko Mwanza, mimi huku ni mtafutaji tu kwa hiyo niko mwenyewe," nikamdanganya.

"Una uhakika na kile ulichojiingiza kukifanya huku dogo?" akaniuliza.

"Ndiyo najua. Nina ujanja mwingi, usinichukulie poa. Sema mambo huko Goba hayakwenda fresh tu ndo' maana nikaja huku kujitafuta, na najua nimejipata tena kwa kuwa chini yako. Sitakuangusha madam. Najua nachokifanya, na nitafata utakachonielekeza kufanya," nikamwambia hivyo.

Akatulia kidogo, kisha akasema, "Sawa. Nipe hiyo kitu nionje."

Nikamfungulia kikaratasi chenye dawa ya cocaine, naye akachovya na kulamba kidole chake huku akinitazama kwa macho makini. Kidogo tu yakalegea naye akawa ananiangalia utadhani ananitaka kimapenzi. Ah mimi nilikuwa mtaalamu bwana!

Na angalau kufikia hapa nikawa nimetambua kwamba hakujua mengi zaidi kuhusu maisha yangu isipokuwa tu kuwa amefatilia na kujua nilikotokea kihalisi kabla ya kufika huku, kwa hiyo mchezo wangu kwake ungeendelea taratibu.

Vibe likiwa limemgonga, akaniambia, "Unyama mzuri huu."

Nikatabasamu kidogo.

"Kuna ishu nataka nikushirikishe," akasema hivyo.

Pasi ndefu hiyoo! Nikatikisa kichwa kuonyesha namsikiliza.

"Kesho utakuja pale pale ulipokuja siku ile, uje jioni," akasema hivyo.

"Sawa. Nije na unyama wetu?" nikamuuliza.

Akaweka macho ya udadisi, naye akauliza, "Unamaanisha kwamba unao mwingi?"

"Nimetengeneza kiasi fulani. Hakijazi mifuko mikubwa lakini si unajua ni tamu mno, kwa hiyo kidogo tu...."

"Ni nyingi," akamalizia maneno yangu.

Nikatikisa kichwa kukubali.

Akaninyooshea kidole chake na kunipiga kofi laini shavuni, naye akasema, "Safi sana. Kumbe we' kweli wa faida. Uje nao kesho. Nitakuelekeza mengine ukishafika."

"Imeisha hiyo," nikamwambia hivyo.

Akawa ananitazama kwa njia fulani utadhani alikuwa ananisoma, naye akasema, "Nataka kuona kama we' siyo mwanaume sura tu."

Nikamsogelea karibu zaidi na uso wake na kumuuliza, "Kivipi?"

"Kesho. Kesho ndiyo nitaona," akasema hivyo huku akipindisha shingo yake kiasi, midomo yetu ikiwa karibu sana.

Nikasema, "Ahaa... nilidhani unataka nikuonyeshe sasa hivi."

Akatabasamu na kuangalia chini, kisha akatoa tusi kunielekea bila kuniangalia.

Nikatabasamu pia baada ya kuona kwamba alikuwa ameanza kuonyesha roho ya kuniamini kiasi, na bila shaka ishu hiyo ya kesho ingehusiana na mengi ya vitu nilivyotaka kuhakikisha vinaporomoka kwa msaada wa askari Ramadhan. Ingebidi kusubiri kuona.

Akawa amekivuta kinywaji chake tena na kuikunjua miguu yake, naye akaniangalia usoni. "Kwa hiyo toka mpenzi wako amekufa, haujaingiza substitute?" akaniuliza hivyo.

Nikatazama chini kwa ufupi, nikielewa alimaanisha Joy.

"Oh, nimegusa pabaya? Mhm... inawezekana ulikuwa unampenda sana."

"Joy na mimi ilikuwa kama biashara tu. Wala hakukuwa na kitu tense kivile," nikamwambia.

"Mm? Unanidanganya mimi? Ahah... unajua bado natakiwa niwe mwangalifu sana juu yako maana inaweza ikawa unataka kumlipizia kisasi mpenzi wako," akasema hivyo.

Dah! Lina akili!

Nikatoa kicheko cha kujilazimisha na kusema, "Madam una vituko. Najua hauamini hilo kwa sababu tayari unaniamini mimi."

"Unajuaje?"

"Usingemwambia bodyguard wako atoke nje kama ungeamini naweza kukufanyia kitu kibaya. Hadi dawa nayotengeneza unakula, kama ingekuwa kukuua si ningewekea hata sumu?"

Akatulia kidogo akiniangalia kwa umakini, naye akasema, "Huwezi kuwa na uhakika sikuzote. Ndiyo maana bado nataka nikupime."

Nikaegamia sofa, huku nikimwangalia kizembe na kusema, "Fanya chochote madam... JC ni mali yako sasa hivi."

"Nhhaa... unanifurahisha. Bado akili yako ni ndogo sana."

Nikamshika kiunoni taratibu, naye akawa makini na kuniangalia machoni. "Ndiyo unifunze sasa. Mi' wa faida kweli," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

Akabaki kuniangalia tu huku akizungusha-zungusha kinywaji ndani ya glasi aliyoshika, na ni hapo ndiyo mlango wa kuingilia ndani humo ukasikika ukifunguka. Kwa sababu nilikuwa nimeupa mlango mgongo, nisingeweza kujua nani kaingia upesi, lakini nikaona macho yake Bertha yakimtazama aliyeingia kwa njia ya kukerwa.

Nikiwa nafikiri ni mhudumu labda au yule baunsa, nikageuka bila kuwa na utayari wa kumchukulia serious huyo mtu aliyeingia mpaka nilipojikuta nashangaa kiasi baada ya kuona ni Chalii Gonga mwenyewe!

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 2
 
Whatsapp +255 678 017 280
Ok
 
MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Mkono wangu bado ulikuwa kiunoni kwa Bertha, nami nikautoa taratibu na kukaa kwa njia tulivu tu, huku nikimtazama jamaa bila hisia yoyote usoni. Kitambo eh? Ndiyo nilikuwa namwona leo sasa, akiwa ndani ya T-shirt jeupe la Manga na suruali ya jeans iliyopauka, huku kofia ikificha nywele zake kichwani.

Akasogea mpaka usawa wa meza ya mwanzo huku akitutazama kwa umakini, naye Bertha akaweka glasi yake pembeni.

"Vipi?" Bertha akamuuliza hivyo.

"Kwa hiyo dogo... ukaona haitoshi kumchokonoa Joy sasa hivi umehamia kwa mke wangu, si ndiyo?" Gonga akaniambia hivyo kwa sauti yenye uzito.

"E-eeh honey, tuliza bass. Mimi siko kama wewe, unanielewa?" Bertha akamwambia hivyo.

"Nakuuliza JC. Umekosa wanawake wengine mpaka umfate MKE WANGU?!" akaongea kwa kufoka.

Nikamwangalia kwa hisia kali.

"Ahaa... kumbe una kiburi?" jamaa akaniambia hivyo.

Kilichofuata ikawa ni yeye kurudisha mkono wake nyuma na kuchomoa bastola, naye akawa ananiangalia kama vile anataka kupasuka. Eti ana uchungu sana! Sijui hata alikuwa ametokea wapi ghafla namna hiyo.

Bertha akaanza kucheka kwa dharau, naye akasimama kabisa na kuyumba kidogo. Nikamwahi na kumshika mkono, mimi pia nikiwa nimesimama sasa, naye akatabasamu na kunipiga kifuani mara mbili kwa kiganja chake.

Akaanza kuelekea pale ambapo Chalii Gonga alikuwa amesimama na kumfikia karibu zaidi, naye akajishika kiuno chake huku akimwangalia kibabe.

"Unafikiri hicho kimguu kinamwogopesha mtu yeyote humu ndani? Mhm... una panick attack Chaz. Tena unajikosha kifala sana. Hata haikupendezi. Unataka kushoot mtu? Anza na mimi," Bertha akamsemesha hivyo bila woga.

Ukimya wa Chalii Gonga kumwelekea mke wake ulifanya ionekene wazi kwamba mwanamke ndiye aliyekuwa na sauti, na undani wa haya maigizo yaliyomleta Chalii mpaka hapa na kutaka kuhamisha hasira zake kwangu ulikuwa ni mpana. Nikaendelea tu kusimama na kuwaangalia.

"Umepata kimjusi cha kuku(.....) unaona sifai sa'hivi, si ndiyo?" Chalii akamuuliza hivyo mke wake.

"Acha ungese Chaz. Kwa kipi ambacho kinakupa wewe hadhi ya kufaa labda? Huo unafiki wako haukusaidii lolote. Kwamba nini, unafikiri ndiyo nitaanza kurukaruka 'eeh mume wangu ananipenda jamani!' Ahahahah... Chaz... stop it. Mimi ni mke wako, siyo kama malaya zako, na japo unaendelea kuchafua mambo mengi, bado ni mimi ndiye nayekusafishia kwa sababu tu ya kuenzi kule tulikotoka. Lakini we' si umeshapasahau? Ndiyo maana unafikiri leo ukinitolea bunduki nitaogopa..." Bertha akasema hayo.

"Siyo hivyo. Yaani... kwanza, haifai kuongea haya yote mbele ya huyu pakashumi. Unataka kusema unamwamini sana kuliko Mimi? Amekupa nini mama G?" Chalii akamuuliza hivyo.

"Usiniite hivyo!"

Sauti ya Bertha iligeuka kuwa na uzito aliposema hivyo, na aliongea taratibu tu lakini ilikuwa kwa ukali ule wa kutoka moyoni. Chalii Gonga akaangalia pembeni.

"Huyu ana fungu lake hapa. Hakuhusu. Mbona hata wewe mwanzoni ulitaka kumchukua kabla ya malaya wako kuuliwa? Acha unafiki Chaz... wewe ndiyo pakashumi," Bertha akamwambia hivyo.

Chalii Gonga akaniangalia na kusema, "Dogo leo unasikia natukanwa na mke wangu kwa sababu yako. Haki ya Mungu utalipia!"

"Ahiii... Charles!" Bertha akasema hivyo kwa mkazo.

Nikawa nimetulia tu, kila kitu nikikisoma fresh.

"Charles! Nije kusikia umemgusa huyu kijana, ndiyo utajua kwa nini huwa wananiita madam! Tena unajua. Unanijua. Ole wako! Aisee, nitakachokufanya zamu hii? Utatamani hata ujute lakini hautaweza," Bertha akamwambia hivyo.

Nikatazama pembeni na kuachia tabasamu la kiburi kiasi. Huyu mwanamke ndiye mtu ambaye umakini wangu wote wa kumporomosha ulikuwa kwake, lakini kwa wakati huu yeye ndiyo akawa amesimama kama malaika wangu. Ha! Wazungu husema twists in turns, yaani hali zisizotazamiwa ndani ya mizunguko ile ile, ndiyo kitu ambacho kilikuwa kinatokea hapa.

Sikuwa hata nimefanya mengi lakini tayari nikawa nimeshaanza, ama labda kuendelea kuwavuruga wanandoa hawa walioonekana kuwa na uhusiano wa kimaslahi tu. Na sasa nikawa nimetengeneza uadui wa wazi kabisa na mume, huku mke mwenye sauti akiwa ndiyo mlezi wangu. Na kumsikia Bertha akisema "zamu hii" ilimaanisha kwamba tayari alikuwa ameshawahi kumfundisha adabu Chalii Gonga huko nyuma, kwa hiyo ni kweli huyu mwanamke angepaswa kuwa kuchunga.

Chalii Gonga akaniangalia kwa macho yenye chuki kali, kama kusema "sisi si milima, tutakutana," kisha akaiweka bastola yake kiunoni na kuondoka hapo hatimaye. Bertha akaachia msonyo mrefu kweli na kunigeukia, naye akaninyooshea mkono wake kama kuniita nimfate. Nikaenda mpaka alipokuwa na kukishika kiganja chake.

"Usimwogope huyo, hawezi kukugusa, sawa?" akaniambia hivyo.

"Najua. Nikiwa na wewe, siogopi hata nyoka," nikamtania.

Akatabasamu na kukitoa kiganja chake kwenye changu, naye akasema, "We' nenda sasa. Nimwambie Dotto akusindikize?"

Kwa haraka nilitambua kwamba Dotto ndiyo yule baunsa wake, na ilishangaza kiasi kwamba tokea jamaa alipoondoka mpaka Chalii Gonga kuingia ndani humu, hakuwa amerudi kabisa.

Nikamwambia Bertha, "Hakuna shida, home hapo tu. Tutaonana kesho. Niombee ili Chalii asiturushie bomu."

"Si umesema hauogopi?"

"Ndiyo siogopi. Ila kuna raha gani nikifa mapema?"

Akaachia tabasamu hafifu na kuangalia pembeni, naye akasema, "Nenda. Usisahau kesho."

"Uhakika," nikamwambia.

"Hiyo kitu iache," akasema hivyo, akiwa amemaanisha yale madawa.

Nikatikisa kichwa kukubali, kisha nikampita na kutoka.

Nikashusha pumzi na kufumba macho kwanza, nikiwa najitahidi sana kutuliza hasira niliyokuwa nahisi. Kiukweli nilikuwa nimejawa na chuki kali sana moyoni kuwaelekea hawa watu wawili, na haijalishi hali ilikuwa vipi wakati tuko humo ndani, yaani kuwaona hivyo kwa pamoja kulikuwa kumenifanya nitamani hata kuwa na bastola ya kuwaangamiza!

Kuna kitu kilichokuwa kinaniambia kwamba suala zima la kumuua Joy halikutokana na kitu kama wivu wa mapenzi tu, na hii hasa ni baada ya kuona namna ambavyo huyo mwanamke alimwendesha mume wake.

Chalii Gonga alimwogopa Bertha kwa sababu fulani, sababu ambayo huenda ndiyo ilifanya mwanamke huyo akasirike sana mume wake alipomwita "Mama G." Ningehitaji kuendelea kujiweka karibu zaidi na huyo boss lady, na kuwa chonjo zaidi na mume wake kuanzia sasa.

Nikapitia geti la nyuma na kuanza kuelekea upande tofauti na nyumbani, nikiwa makini sana kuona ikiwa nilifatiliwa. Si unajua haingekuwa poa endapo kama mtu angetaka kuniua halafu niende moja kwa moja kwa Ankia na kumpelekea shida zisizomhusu dada wa watu? Ingawa nilielewa kwamba Chalii Gonga aligongwa marufuku, bado nilitaka tu kuwa makini, nami nikafanikiwa kuzungukia njia nyingine mpaka kufikia pale tulipoishi bila kutatiliwa. Dah! Likizo yangu ilikuwa imeanza kujaa visa!

Nikalipita duka la Fatuma na kwenda mpaka ndani ya geti, nami nikasimama karibu na ukuta; sehemu ile ile niliyotulia ule usiku na kumsikia Joshua akiongea maovu yake. Nikaona kupitia matundu ya ukuta gari la bibie Miryam hapo nje, nami nikaelewa kwamba walikuwa wamerudi kutoka kwa huyo mpuuzi.

Nikawa nimeingiwa na hamu ya kutaka kwenda kumwona Mariam, nijue anaendelea vipi, lakini tena nikakumbuka kwamba Adelina alikuwa hapo kwa Ankia; na nilimwahidi kuwahi kurudi ili angalau tupatane kidogo. Ikiwa ningeenda kumwona Mariam najua ningehitaji kukaa tena hapo kwa muda zaidi. Aigh! Ningejigawaje, maana na akili yangu tayari ilikuwa imevurugwa na maadui zangu?

Nikaona nimpigie kwanza Tesha kumuuliza ikiwa alikuwa amesharudi... aaah kweli, nikakumbuka simu yake ilikuwa imeibiwa, hivyo nisingeweza kumpata. Nikaachana naye na kuamua niende tu kwa mgeni wetu, nami nikavaa sura ya kondoo na kwenda mpaka ndani.

Nikakuta Adelina akiwa amekaa pale pale sofani huku akiwa bize na simu yake, na baada ya kuniona akaachia tabasamu hafifu tu. Ankia hakuwepo hapo, nami kwa wakati huu ndiyo nikaweza kumchora vyema zaidi Adelina tofauti na nilivyokuja mara ya kwanza nikiwa na haraka.

Alivaa T-shirt la mikono mifupi, lenye rangi mchanganyiko wa nyeupe, zambarau, na pink, kwa mtindo wa mistari minene kama ngozi ya pundamilia, na miguuni ilikuwa ni suruali ya jeans iliyobana vyema umbo lake kuniruhusu kuona kwamba alikuwa na shepu nzuri sana. Yaani alikuwa na miguu mirefu, halafu paja lilikuwa nono na hips kujaa, na kwa jinsi alivyochomekea hiyo T-shirt kwenye suruali na kuivuta suruali mpaka kufikia tumboni, nilijua huko nyuma kwake kungenifanya nije kumwangalia kwa macho yenye dhambi!

Alikuwa black beauty, msafi, na wakati huu niliona msuko wake kichwani kuwa wa zile rasta ndefu zenye rangi ya kahawia, zikiwa zimemwagikia mgongoni kwake. Mkufu mzuri shingoni, mabangili mkononi, saa, yaani kama huyu mwanamke hakuwa na kazi ya maana hapa jijini, basi ni lazima kuna njemba iliyokuwa inagharamika mno hapo. Alionekana kujipenda kama tu Joy alivyokuwa.

"Adelina... nilifikiri ningekuta umeshasepa," nikamwambia hivyo baada ya kufunga mlango.

"Hamna, nipo. Vipi mishe?" akasema hivyo.

"Fresh. Ankia?"

"Yuko chumbani, ameingia sasa hivi tu," Adelina akanijibu.

"Ahaa, sawa," nikasema hivyo na kukaa kwenye sofa hilo hilo karibu naye.

"Vipi wa Kigamboni wanasemaje?" akaniuliza.

"Ah, unafikiri hata tumezungukia huko sana? Tumepita kivuko tu, mvua ikaanza kunyesha, kwo' ikatubidi tutimkie Kariakoo na kuzungukia sehemu zingine."

"Aaa... pole lakini. Mwenzako je?"

"Tuliachana pale Uhasibu, ye' akaelekea kwingine. Umefika zamani?"

"Hamna... ni kwenye saa kumi na moja..."

"Asa' si hata ungenitumia ujumbe kuniambia, labda hata ningewahi," nikamwambia hivyo.

"Aa, hamna. We' ulipaswa kumaliza mizunguko yako, me hapa ungenikuta tu," akaniambia hivyo.

"Au siyo?" nikamuuliza hivyo.

Akacheka kidogo kwa pumzi.

"Mbona huyu naye kakuacha peke yako tena?" nikamuuliza.

"Ameenda kuongea na simu," akaniambia hivyo.

"Ahaa, sirini eti? Watu na wapenzi wao..."

"Ahahahah... inawezekana," akasema hivyo.

Alikuwa na kicheko kizuri sana, nami nikiwa nataka kuendeleza story ndiyo ile "kwechee" ya mlango wa chumba cha Ankia ikasikika. Sote tukaangalia upande huo na kumwona Ankia anatoka, lakini bado alikuwa anamalizia kuufungua mlango wake taratibu huku macho yake yakiwa kwenye simu kiganjani, na huo mlango ukawa unamalizia kelele zake kama vile unacheka. Eee-he-he-e-e-e-e-e-e...!

Nikacheka kidogo na kusema, "Unausikia huo mlango lakini?"

Adelina akacheka kidogo, naye Ankia akaja upande wetu na kusema, "Hiyo sauti me mwenyewe inanikera!"

"Ni kukukera tu eeh, sijui shauri ya umaskini? Hadi mlango unakucheka kwa sababu umeuacha uzeeke," nikamtania hivyo Ankia.

Adelina akacheka tena, na mimi nilikuwa nataka tu nisikie kicheko chake, naye Ankia akacheka pia na kusema, "Kichwa chako."

Mwanamke huyo alikuwa amevaa kawaida yake ya nyumbani na kilemba, huku leo tena ndiyo nikimwona na pini puani kwa mara nyingine tokea mara ya kwanza nimefika hapa.

"Wakina Bi Zawadi wamefika zamani sana?" nikamuuliza Ankia.

"Siyo sana. Muda ule umerudi na kuondoka tena, ndiyo Miryam akaja kuchukua funguo zao. Tesha umemwacha wapi?" Ankia akauliza.

"Yupo Uhasibu, atakuja baadaye," nikamwambia.

"Ahaa sawa. Kwa hiyo unaenda kuwaona warembo wako?" Ankia akauliza hivyo.

"Nitawapigia simu baadaye kumsalimia Mamu pia maana... ishakuwa usiku kwenda kabisa," nikamwambia hivyo.

"Na unavyompenda Mamu! Mhm..." Ankia akasema.

"Ni mgonjwa wake, kumpenda lazima," Adelina akasema.

"Umeona? Kana wivu haka!" nikamwambia hivyo Adelina, naye akatabasamu.

"Haya bwana. Zawadi yangu iko wapi?" Ankia akauliza.

"Ah... nimesahau, mambo mengi. Kesho basi," nikamwambia hivyo.

"A-aah... me sitaki. Nipe zawadi yangu, uliniahidi. Tena... unapaswa kumpa na mgeni," akaniambia hivyo.

"Ila Ankia! Nitatoa wapi sasa na msimu wa Krismasi bado?" nikamuuliza pia.

"Ahahah... ameanza kudeka sasa," Adelina akasema.

"Nipe bwana hata nimfatie mgeni K-Vant," Ankia akaendelea kulazimisha.

"Ankia mbona una king'anganizi hivyo? Na mimi sitaki hiyo K-Vant usimpe presha mwenzako bwana," Adelina akamwambia hivyo.

"Unatumiaga K-Vant?" nikamuuliza Adelina.

"Nikiwa tu nataka kulewa, na sasa hivi sijisikii," akanijibu.

"Basi hata Dompo tu jamani," Ankia akasema hivyo.

Niliweza kuona kwa jicho la pembeni kwamba Adelina alikuwa anajaribu kumzuia Ankia kwa ishara ya kichwa asiombe hayo mambo, nami nikatabasamu na kutoa wallet yangu. Nikachomoa shilingi elfu kumi na kumpa Ankia, naye akaipokea kwa furaha huku aking'ata mdomo wake.

"Ngoja nikafate Dompo," Ankia akasema hivyo kwa madoido.

"Masai?" nikamuuliza.

"Hamna, kuna grocery tu hapo pembeni. Nakuja sasa hivi," akasema hivyo na kuondoka upesi.

Inaonekana alikuwa na hamu sana na kileo!

Nikamtazama Adelina machoni, naye akaniangalia pia, kisha nikauliza, "Ulijuaje kwamba Mariam ni mgonjwa wangu? Unamjua?"

Akasema, "Hapana. Ankia ndiyo kaniambia. Kasema wewe ni daktari kabisa na unamsaidia huyo msichana. Nimemwona na dada yake leo alipokuja kuchukua funguo."

"Ahaa, sawa. Haukufahamiana na hiyo familia eti?"

"Ndiyo, siwafahamu. Zaidi... Ankia alishawahi tu kuniambia kuhusu huyo Miryam, walisaidianaga zamani sana. Wanaheshimiana yaani, na huyo dada anaonekana mstaarabu."

"Ndiyo, wote ni watu wazuri. Vipi wewe... nyumbani, hali ikoje?"

"Panatulia kadiri siku zinavyoenda. Jumamosi wanaanza mchakato wa kujenga kaburi la Joy kule Nachingwea," akaniambia.

"Ahaa, kumbe bado walikuwa hawajajenga?"

"Eeh. Nitakwenda huko ikifika Ijumaa. Kama ukiwa na nafasi, nilikuwa nataka nikwambie... nikuombe unisindikize," akasema hivyo.

Nikaangalia pembeni kwa ufikirio.

"Au... kama utakuwa na... mambo mengi... haina shida, nitapata tu...."

Nikakishika kiganja chake na kuanza kukisugua ili kumtuliza kiasi, naye akaniangalia kwa utulivu. "Usijali. Tutaenda pamoja. Utafika kwa... itakuwa nyumbani kabisa, si ndiyo?"

Akatikisa kichwa kukubali, naye akasema, "Asante. Nimemwalika na Ankia pia, kwa hiyo... asante kwa kukubali kuja, ingawa nimekushtukiza."

"Haina shida kabisa rafiki yangu. Tuko pamoja," nikamhakikishia hilo.

Akabaki kuniangalia tu kwa umakini, nami nikajikuta naendelea tu kumtazama. Huyu mwanamke hakuwa wa namna ya kupindisha maana, yaani niliona wazi kabisa kwamba alikuwa jasiri na aliyejua aliyoyataka, kwa sababu hakukwepesha macho yake wala kuonyesha shau yoyote ile kunielekea.

Alikuwa mwanamke ambaye unaweza kusema ni mkomavu, asiyeona uajabu wa hali zozote zile ambazo kikawaida zinakuwa za kawaida, kama hivyo nilivyomshika kiganja, na hilo nililiheshimu. Angekuwa mwingine hapo angeanza kujichekesha kimashauzi kisa tumebaki wawili, lakini huyu ndiyo moja ya wale wanaothibitisha kwamba siyo wote wako namna hiyo. Wengine wanajielewa.

Nikakiachia kiganja chake na kumuuliza, "Vipi... ishu ya Joy... mapolisi wameshawaambia lolote?"

Akatikisa kichwa kukanusha, naye akasema, "Hakuna lolote la maana kabisa. Japo... juzi hapo yule mpelelezi alinipigia akasema... hajasahau kuhusu mauaji ya mdogo wangu kwa hiyo niendelee... mimi na familia yetu yaani, tuendelee kungoja tu, na muda siyo mrefu sana watawakamata waliofanya yale mambo. Sijui hata kama naweza kuwaamini hawa mapolisi maana... ni chenga tu ndiyo zitakazofata mpaka litasahaulika."

"Hapana, usiseme hivyo. Kuwa na imani tu. Hata mimi najua Joy atapata haki ya kifo chake," nikamtia moyo.

"Ngoja tuone. Hao watu wakikamatwa kweli... labda ndiyo tutapumua maana mpaka sasa hivi mama yetu hatoki ndani kwa kuhofia watu wa nje... amekuwa kama mgonjwa yaani," Adelina akasema hivyo na kupiga ulimi mdomoni kwa njia ya masikitiko.

Ilinifanya nimwonee huruma, lakini bado nikawa najizuia nisimwambie kuhusiana na mambo niliyokuwa nikifanya pamoja na huyo huyo mpelelezi aliyemsemea ili kuwakamata wasababishi wa kifo cha mdogo wake.

Ankia akawa amerejea, nami nikabadili mada upesi ili hali ya uchangamfu irudi. Alikuwa amepata chupa kubwa ya wine ya Dompo, naye akafata glass za vioo ili aje kutuwekea tushushe taratibu. Alikuwa ameshapika kabisa lakini tungekunywa kwanza ili kuchangamsha miili kisha ndiyo msosi tungepiga baadaye.

Joto nililokuwa nahisi lingehitaji kuondolewa kwa kwenda kujimwagia, lakini nikaamua kuendelea tu kukaa na marafiki hawa na maji ningekuja kupiga baadaye.

★★

Kwa hiyo tukanywa taratibu tu na kuendelea na maongezi mpaka nikasahau kupiga simu kwa Bi Zawadi ili kuwasalimia. Ankia akatufanyia wepesi wa kupakua vyakula ili tule pamoja na kinywaji taratibu, nami nikahisi kushiba na kuridhika kwa ushirika wa kirafiki pamoja na marafiki hawa. Hata nikasahau kabisa kuhusu vitisho vya Chalii Gonga masaa machache yaliyopita vilivyokuwa vimeniharibia amani kiasi.

Imeingia mida ya saa tano ndiyo Adelina akasema anahisi usingizi na alihitaji kulala mapema ili kesho awahi kuamka kwa ajili ya kwenda Mbezi; alihitajika kuwahi kazini. Wakati huu nilikuwa nimeshafahamishwa kwamba mwanamke huyu alifanya kazi ya kutengeneza mabatiki kwenye duka moja kubwa huko Mbezi, na alikuwa amepanga vyumba maeneo ya Kinyerezi kusiko mbali sana na alipofanyia kazi.

Kwa hiyo Ankia akawa ameenda pamoja naye chumbani kwake ili wakapangane sijui, na ndiyo nikawa nimetumia nafasi hiyo kumpigia Bi Zawadi. Akapokea, nasi tukasalimiana vizuri sana, na baada ya kumuuliza mambo yalikwendaje kwenye matembezi yao leo, akaniambia kwamba yalikuwa mazuri sana tofauti na matarajio yake.

Akasema kwamba huyo Joshua aliwaonyesha mabadiliko makubwa aliyokuwa ameanza kuyaweka maishani mwake, kwamba alimtendea mke wake vizuri sana kama mwanamke anavyostahili kutendewa, na aliwatendea kwa fadhili na heshima; wote kwa ujumla kama familia. Akaniambia kesho niende hapo kwao mapema maana Mariam alikuwa amenimiss sana leo, nami nikakubali na kumtakia heri ya usiku mwema.

Nikashusha simu na kutikisa kichwa kidogo kwa kusikitika. Jinsi sauti ya Bi Zawadi ilivyoonyesha imani mpya kuelekea suala la huyo Joshua, ilinifanya nimwonee huruma sana, familia hiyo yote kwa ujumla, kwa sababu mioyo yao mizuri ilikuwa ikichezewa vibaya na huyo mwanaume kwa mara nyingine tena bila wao kujua. Lazima tu kuna vitu ambavyo Joshua alikuwa anafanya kuwaaminisha kwamba amebadilika kiasi cha kumfanya hadi Bi Zawadi asifie nyendo mpya za jamaa.

Aisee, ningehitaji kuongea na Miryam. Alikuwa anapenda kutafuta amani sawa, lakini hapo angekuja kujikuta anaangukia kubaya zaidi ya kule alikodondokea kipindi cha nyuma kutokana na kusukumwa na huyo huyo kaka yake. Najua nisingeweza kuwa sehemu zote kwa wakati wote kuhakikisha ulinzi kwa Mariam, ndiyo sababu ningepaswa kumpa mwanga dada yake kwa yale niliyofahamu kabla mambo hayajaharibika.

Nikiwa bado natafakari vitu vya kufanya, Adelina akawa ametoka chumbani kwa Ankia na kuja upande wangu. Nilipomtazama, nikajikuta nimezubaa kiasi baada ya kumwona akiwa amejifunga khanga moja kutokea kifuani, iliyofikia mwanzo wa magoti yake hasa kutokana na yeye kuwa mrefu.

Alikuwa anaenda kuoga bila shaka, naye akanipita huku akisema macho yangu yamelegezwa kweli kwa wine niliyokuwa nimekunywa, nami nikatabasamu tu na kumsindikiza kwa jicho la chini mpaka alipokwenda nje. Hilo limlima huko nyuma! Siyo poa.

Nikageukia upande aliotokea pale chumbani na kukuta Ankia akiwa amesimama huku akinitazama, tabasamu la kuhukumu likionekana midomoni kwake, nami nikamuuliza 'nini?' lakini akacheka kwa mguno na kupiga kofi viganjani kuthibitisha kwamba kweli alikuwa ananihukumu kutokana na jinsi nilivyomwangalia Adelina akiwa ndani ya khanga.

Nikamnyooshea kidole na kumwambia 'wewe!' kisha nikanyanyuka na kuelekea chumbani kwangu; nikimwacha hapo anacheka baada ya yeye kunisukuma kidogo mgongoni. Najua na wine pia ilikuwa imemchangamsha kwa hiyo hata sikumkazia fikira. Nilikuwa tu nahisi uchovu wa mwili kiasi kutokana na mizunguko ya leo, nami nikashusha neti na kutulia tu kusikilizia Adelina atoke bafuni ili nami nikajimwagie.

Baada ya kusikia amerudi ndani, nikaenda zangu bafuni pia na kujimwagia maji, kisha nikaingia kujipumzisha. Ningeweza kuwasikia wanawake wakizungumza mambo yao yenye kufurahisha huko chumbani mpaka kufikia mida ya saa saba, ndiyo wakatulia baada ya hapo. Kwa sababu fulani, usingizi ulikuwa unanipinga mpaka kufikia saa nane kabisa, ndiyo hatimaye nikaingia ndotoni.

★★★

Nimekuja kushtuka kutoka usingizini pakiwa pameshakucha zamani sana, nami nikavuta simu yangu kuangalia muda. Ilikuwa ni saa nne asubuhi sasa, na kiukweli nilikuwa nimelala. Ile kulala ya moja kwa moja bila kushtuka hata mara moja usiku yaani. Nikakuta jumbe kadhaa kutoka kwa marafiki zangu, na namba ngeni.

Hiyo namba ngeni ilikuwa ni namba mpya ya Tesha. Alikuwa ameniambia kwamba alilala pale pale kwa Dina jana na sasa ndiyo alikuwa njiani kurejea huku, na ni mwanadada huyo ndiye aliyekuwa amempatia simu yake ya ziada ili jamaa atumie mpaka akinunua nyingine. Soraya pia alikuwa ametuma ujumbe wa salamu, Latifah aliuliza ningerudisha vile vifaa vya hospitali lini, na Adelina aliacha jumbe ya kuniaga, kwamba tayari aliondoka na alitarajia tungeonana Ijumaa.

Nikawajibu wote chap chap; Tesha nikimwambia sawa, Soraya nikimwambia ningemtafuta baadaye, Latifah nikimwamdikia tu "Jumamosi," na Adelina nikamtakia safari njema na kuomba radhi kuchelewa kuamka maana hata sikumsindikiza mpaka hapo Mzinga, kisha ndiyo nikatoka kitandani ili niianze siku kwa kawaida yangu ya kufanya usafi wa mwili.

Kama kawaida ya mwenye nyumba wangu, alikuwa ameshaamka na kufanya usafi wa ndani, na chai ilikuwa tayari. Nilipomaliza kuoga na kuvaa, akaniwekea chai na maandazi ya nguvu, nami nikanywa na kushiba. Akawa ameniambia kwamba leo alitamani sana kutengeneza pilau na nyama ya kuku yeye mwenyewe hapo nyumbani, nami nikampatia hela ya kumchangia kununua vyote alivyohitaji. Akafurahi sana!

Baada ya hayo ndiyo nikamuaga sasa ili niende kumwona Mariam. Nilikuwa na mwonekano wangu safi kabisa na niliwapita wakina Fatuma na mashosti zake hapo nje wakiwa wamekaa kwa kutulia tu, nami nikaingia moja kwa moja getini kwao Tesha na kuelekea mlango wa kuingilia ndani ya nyumba. Niliweza kuona viatu vya kike vilivyokuwa vigeni machoni kwangu, na kwa sababu gari la Miryam halikuwepo hapo, hiyo ilimaanisha kwamba bila shaka kulikuwa na mgeni.

Nikafungua mlango huku nikisema "Hodi, hodii," na sauti ya Bi Zawadi ikajibu, "Karibu, karibuu."

Nikaingia huku nikitabasamu kiasi, lakini nilipomwona mgeni aliyekuwa amekaa sofani pamoja na Mariam, tabasamu langu likatoweka.

Ilikuwa ni mke wake Joshua, mwanamke mwenye kiuno na miguu mirefu pia. Alikuwa amevaa kijora chenye rangi kama vile moto unawaka nguoni, na alizificha nywele zake kwa kilemba cha hiyo nguo. Alikuwa akinitazama kwa macho yenye utulivu tu, naye binti Mariam, akiwa ndani ya dera pia, akatoka sofani na kunifuata huku akitabasamu kwa hisia sana.

"Mamu huyoo... hi-five," nikasema hivyo nikiwa nimenyanyua kiganja changu juu.

Mariam akagongesha kiganja chake hapo na kusema, "Shikamoo?"

"Marahabaa. Umeisema kwa wepesi hiyo, safi sana," nikamwambia hivyo.

"Asante. Karibu," Mariam akaniambia hivyo.

"Wacha!" nikamwambia hivyo, naye akacheka kidogo.

Ingawa wakati huu Mariam alikuwa akizungumza, hiyo haikumaanisha kwamba alikuwa amepona kabisa, kwa sababu tabia za kitoto kwenye utu wake bado zilikuwepo, na ndiyo mazoezi ya juu zaidi yalitakiwa kufata ili ziondolewe. Lakini hawa wakina Joshua walikuwa wameanza kuleta tena michezo yao ya kijinga ambayo ingepaswa kukoma haraka kabla hawajamvurugia mtoto maendeleo yake.

"Shikamoo cheupe wangu?" nikamwamkia Bi Zawadi.

"Marahaba baba, karibu ukae," akaniambia hivyo.

Mariam alikuwa ameshanizoea vya kutosha kunishika mkononi na kunivuta ili nikakae, lakini sikutaka kukaa pale alipozoea mimi kupenda kukaa kwa sababu huyo mke wake Joshua alikuwa amekaa hapo wakati huu. Lakini sikuwa na jinsi kwa kuwa binti mwenyewe alinivuta kwa raha zote, nami nikasogea mpaka hapo kwa kumfuata.

Huyo mwanamke akasogea pembeni kiasi ili nafasi iwe ya kutosha, na Mariam akakaa mwishoni mwa sofa ili mimi nikae katikati. Yaani mimi ningekaa katikati ya Mariam na mke wake Joshua, na ile nimeketi tu, katika kujisawazisha vizuri, nikawa nimemkanyaga kiasi mwanamke huyo mguuni kwake. Ha, makosa! Sijui tu akawa amefikiria nini.

"Bi Jamila hajaamka bado?" nikamuuliza hivyo Bi Zawadi.

"Mh? Mpaka sa'hivi? Hamna ametoka na Mimi. Ameamka hajisikii vizuri kwa hiyo Miryam kampeleka apigwe check-up kabisa," akanifahamisha hilo.

"Ahaa, sawa. Kwa hiyo watarudi pamoja?" nikauliza tena.

"Hamna, Shadya ndiyo anampitia wanakuja naye. Miryam yeye anapitilizia kazini," Bi Zawadi akasema hivyo.

"Sawa. Bora kupima kabisa, wamefanya la maana," nikamwambia.

Bi Zawadi akasema, "Eeh ni kweli. JC baba... huyu ni mke wa Joshua, anaitwa Khadija."

Nikamwangalia huyo mwanamke pembeni yangu na kusema, "Sawa sawa. Nimefurahi kukujua."

Bila kuniangalia, huyu Khadija akasema, "Asante," lakini nikahisi namna ambavyo alinikanyaga mguuni kwa njia ya kukonyeza. Dah!

Nikajikausha na kumwangalia Mariam.

"Huyu ndiyo daktari wetu mahiri. Yaani unavyomwona Mamu sasa hivi ujue ni yeye ndiye kasaidia," Bi Zawadi akamwambia hivyo mkwe wake.

"Aaa... hongera sana kaka. Umemsaidia sana Mamu mpaka amepona," Khadija akaniambia hivyo.

"Bado hajapona kabisa. Tunatakiwa kuendelea na mazoezi yetu, au siyo Mamu?" nikasema hivyo.

"Ndiyo kaka. Leo tutacheza mchezo gani?" Mariam akaniuliza.

Huku nikimwona Bi Zawadi anatabasamu, nikamwambia binti, "Leo tutacheza mchezo wa kuchora. Inabidi ukamwibie dada Mimi kalamu na karatasi haraka ili tuje tumchore halafu uje kumwonyesha, sawa?"

Mariam akatikisa kichwa na kwenda upande wa chumba upesi, naye Bi Zawadi akacheka kidogo.

"Za jana? Huyu alitulia wakati mpo huko?" nikamuuliza hivyo Bi Zawadi.

"Ndiyo. Aa... ni mambo mengi sana... mazuri ya jana. Ahah... ngoja nikakuwekee chai kidogo baba," Bi Zawadi akasema hivyo na kunyanyuka.

Nilielewa upesi kwamba mwanamke huyo hakutaka tuzungumze mengi yaliyotokea jana nyumbani kwa Joshua huku mke wake akiwa hapa, yawe mazuri au mabaya, ili asitoe picha ya kwamba huwa wanawazungumzia wawili hao kwangu pia. Kwa hiyo kisingizio cha kuniletea chai kilifaa ili akate hiyo mada, lakini kuniacha hapo na huyo mwanamke likawa suala la utata.

Nafikiri alikuwa mwanamke jasiri kiasi, yaani hakuwa na aibu juu ya mambo aliyotaka, kwa sababu baada tu ya Bi Zawadi kuelekea jikoni papo hapo akaanza kutelezesha kidole chake cha mguuni kwenye mguu wangu bila kuniangalia, akijifanya ametazama mbele tu kwa utulivu. Haloo! Yaani kosa tu kidogo kumkanyaga likawa limeiingizia akili yake jambo ambalo hata halikuwa karibu na himaya ya fikira zangu.

Nikamwangalia usoni kwa umakini, naye akaibana midomo yake na kunitazama kwa macho yenye uvutio eti. Kwa hiyo sekunde mbili tu kukaa naye akawa amenitaka? Sikupendezwa na jambo hili, lakini uharaka wake ukawa umenipa wazo.

Ikiwa mwanamke huyu alikuwa akishirikiana na mume wake katika mipango yake mibaya ama tu kuijua, ningehitaji kupata jambo fulani hakika kutoka kwake ambalo lingesaidia kuthibitisha na kuitibua mipango hiyo. Mara nyingi ushahidi huwa ni muhimu sana kwenye visa vya namna hii, na sikujua kivipi tu lakini nikawaza kwamba kwa njia moja ama nyingine kuwa na ukaribu wa kisiri pamoja na mwanamke huyu kungesaidia kufanikisha wazo langu, kwa hiyo nikaamua kwenda na mchezo aliofikiri nilikuwa nimeanzisha. Si unajua kwa wanawake sinaga mbambamba?

Nikaangalia upande wa jikoni kupitia pale dining na kuona kwamba Bi Zawadi alikuwa anamimina chai kikombeni, nami nikarudia kumwangalia Khadija. Sijui alikuwa mwislamu aliyebadili dini? Maana Joshua ni mkristo bila shaka, lakini hayo nikayaweka pembeni kwanza.

Mwanamke huyu akawa ananiangalia kama vile anasubiria nifanye jambo fulani au kumpa ishara yoyote ile, kwa sababu sasa alikuwa ameacha kunisugua mguuni, nami nikaweka kiganja changu kwenye titi lake la kushoto lililofichwa kwa nguo yake na kulikamata. Hakuwa amevaa sidiria maana lilihisika vyema kiganjani kwangu. Na hakunizuia, bali akaweka kiganja chake kwenye paja langu na kuanza kulipa massage huku akielekea kati taratibu. Huyu alikuwa na ile akili sharp ya kimya kimya, asipindishe maana wala kujishaua, na hiyo ilikuwa nzuri.

Nikaifinya chukuchuku yake na kuivuta kwa nguvu, naye akaniangalia huku amekunja sura yake utadhani alikuwa anataka kuanza kulia, na kiganja chake kikaishika sehemu yangu ya siri iliyokuwa imeanza kuvimba ndani ya jeans. Huyu hakuwa mwoga yaani, na mimi nilikuwa makini kuhisi wakati ambao Bi Zawadi angeanza kurudi, ila likafuata jambo ambalo sikuwa nimetarajia.

Kutokea upande wa korido lililoelekea vyumbani, akatokea Joshua akiwa anakuja upande wetu kwa mwendo wa taratibu tu! Nikashtuka machoni kwa sababu ya ughafla wa jambo hilo ambalo sikutazamia kabisa. Alikuwa ametokea wapi?

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Ile nimemwona tu jamaa, pigo la moyo lilidunda kwa nguvu kiasi kutokana na kutotarajia jambo hilo, nami nikaliachia titi la Khadija. Mwanamke huyo akautoa mkono wake kwangu pia, akijikausha kwa kutazama pembeni, na Joshua alikuwa amesimama usawa wa sofa huku akitutazama. Nikawa namwangalia kwa umakini tu, nikishindwa kuelewa alikuwa ametokea wapi.

Cha ajabu ni kwamba, baada ya kuwa amesimama na kutuangalia namna hiyo, akaachia tabasamu hafifu huku akiniangalia kwa njia ya kirafiki usoni, nami nikaendelea kumtazama kwa umakini tu. Nilikuwa na uhakika kabisa kwamba aliona kile ambacho kilikuwa kinatokea hapo baina yangu na mke wake, lakini akajifanya kama hajaona ili kuendeleza unafiki wake.

Hapo ndiyo Bi Zawadi akawa ametokea jikoni, akiwa ameshika kikombe chenye chai na kusema, "Joshu... hadi nilikuwa nimeshasahau kama uko ndani jamani."

"Eeeh, nisamehe tu mama, huko tunakotoka hatuna vyoo vya kukaa. Hiki chenu kizuri hadi kidogo nisinzie," jamaa akasema hivyo.

Kumbe jamaa alikuwa chooni anajisaidia muda wote huo? Na inaonyesha alikuwa ameshusha limzigo lizito kweli maana alikaa zaidi ya nusu saa huko. Na wengine huwa wanakaa mpaka masaa!

Bi Zawadi akacheka kidogo na kuja kunipatia chai, naye akaenda kukaa kwenye sofa lake pale alipozoea.

Nikataka kunyanyuka ili nimpishe Joshua aketi na mke wake, lakini jamaa akasema, "Ah we kaa tu bro, me niko safi hapa."

Nikawa namwangalia tu kwa utulivu, naye akakaa kwenye mkono wa sofa huku akilaza mkono wake juu ya egamio la sofa karibu na Bi Zawadi. Mke wake alikuwa ameushona tu pembeni, akitulia kama malaika mpya aliyezaliwa leo. Ni hapa ndiyo Mariam akawa amerudi tena, na sijui kwa nini tu alikawia mno.

Akaja mpaka sofani akiwa ameshika penseli, boksi lenye rangi, pamoja na counter-book kubwa, naye akasema, "Hizi hapa. Tumchore sasa."

"Mamu subiri kwanza kaka anywe chai," Khadija akamwambia hivyo.

"Eeh, ngoja kwanza. Mtachora baadaye," Bi Zawadi akasema hivyo pia.

Mariam akaweka uso wenye kuonyesha kwamba alikwazika, nami sikupenda kumwona hivyo. Lakini ningefanyaje na sukari ilikuwa imeshakorogwa kwenye chai?

"Mamu... usinune mama, eti? Anamalizia tu kunywa chai halafu ndiyo mtachora. Tena na mimi nitachora na nyie, sawa?" Joshua akamsemesha hivyo kwa kubembeleza.

Mariam akawa bado amenuna, naye akanyanyua bega lake kuonyesha kwamba hataki.

Nikasema, "Haina shida, tutachora huku nakunywa na chai. Cheupe wangu, asante. Mamu... twende."

Nikasimama pamoja na Mariam, ambaye bado alikuwa kama amenuna lakini akaridhia kwenda nami upande wa dining, nasi tukakaa vitini na kuanza kuchora.

Nilikuwa namchorea mambo rahisi kama kiti, mpira, yai, kikombe, naye angeiga kwa kujitahidi kabisa kuvifananisha. Nikawa namsifia, hata Bi Zawadi na Joshua wangekuja hapo na kuangalia kazi za binti na kumpongeza, na hii ilisaidia kumwongezea Mariam hali ya kujiamini zaidi nilipoanza kumpa michoro ya mambo tata zaidi.

Aisee Joshua alikuwa anajua kuigiza! Yaani nilikuwa nikitazama namna alivyoongea na kuwatendea wanawake hawa kana kwamba alikuwa amezaliwa kwa mara ya pili na kuwa mtu tofauti kabisa, lakini ukweli wa utu wake mbaya bado ulikuwa pale pale.

Sikupenda kabisa alipomsogelea Mariam na kumsemesha ama kumgusa, na nilikuwa nimeona niendelee kutulia tu ili amani ambayo niliiona ndani yake Mariam kwa wakati huu ibaki hapo hapo kwanza. Huyu Joshua angehitaji kuumbuliwa na kuondoshwa hapa kwa nguvu ya Miryam pekee, ambaye alikuwa ndiyo njia iliyofanya jamaa akapata kiburi cha kurudi tena.

★★

Kufikia mida ya saa saba mchana tayari mke wake Joshua alikuwa ameshaanza kufanya harakati za mapishi hapo ndani, na sijui kwa nini tu lakini mpaka sasa hivi bado tu Tesha hakuwa amefika. Hali yake Mariam kwa wakati huu ilikuwa changamfu kweli baada ya mimi kufanya kitu kilichompa furaha sana.

Alikuwa ameleta picha moja nzuri sana ya Miryam kutoka kwenye album, naye alinitaka nimchore dada yake. Nilikuwa najua kuchora lakini ikifikaga kwenye pua za watu ndiyo huwaga naharibu kabisa, ila nilipoichora pua ya Miryam niliikuza sana kwa makusudi ya kumchekesha Mariam. Na walicheka mno! Bi Zawadi, Khadija, na hata Joshua Iskariote, wote wakawa wanaiongelea mno, na kilichokuwepo ilikuwa kuja kuwaonyesha wengine na hasa Miryam, ili waone itikio lake.

Halafu huyo Khadija, tokea muda ule Joshua katushtukiza, alikuwa analeta pigo za kimahaba kunielekea kwa kunitazama kwa yale macho na tabasamu la "ninakutaka," ama kujipitisha-pitisha dining ili niangalie jinsi kalio lake lilivyonesa huko nyuma, lakini mimi bado nilikuwa tu nawaza kuhusu usalama wa Mariam kwa ujumla kwa kuwaza zaidi juu ya mume wa huyo mwanamke.

Jamaa hakuwa amenisemesha tena kwa sababu nilionyesha wazi kwamba sikutaka mazoea naye hata kidogo, lakini niliweza kuona namna alivyokuwa ananitazama sana kama vile ananichora kutambua nimekaaje-kaaje, na nadhani alikuwa ameshatambua kwamba sitaki shobo naye kabisa.

Hazijapita dakika nyingi sana toka imeingia saa saba ndiyo tukasikia mlango wa geti nje ukifunguliwa na kufungwa, na baada ya hapo mlango wa kuingilia sebuleni hapo ukafunguka pia na Tesha kuingia. Mwonekano wake ulikuwa ule ule wa jana, lakini bila shaka kwa siku hii alikuwa ametoka huko kwa Dina akiwa ameoga.

Baada ya yeye kuingia, akamsalimu mama mkubwa wake na kuitikiwa vizuri tu, lakini nikaona anamtazama Joshua kwa njia ya kusita kutoa salamu. Akawa ameniona nikiwa na Mariam hapo dining, nami nikamtikisia kichwa kisalamu. Akairudisha salamu yangu namna hiyo hiyo, naye Joshua akaona amsemeshe.

"Vipi mdogo wangu?" jamaa akamuuliza hivyo Tesha.

"Poa," Tesha akamjibu kibaridi tu na kumpita.

Akaja mpaka upande wetu na kumsalimia Mariam, na binti akamwonyesha ule mchoro wa picha ya dada yao.

Tesha akacheka na kusema, "Dah! Kaka naona unataka kutangaza vita na Mimi! Akiiona anaweza akavimba wiki nzima."

"Kweli? Itabidi Mamu asimwonyeshe," nikamwambia.

Mariam akasema, "Tamwonyesha... atacheka."

"Eeh usiache kumwonecha... atacheka chana," Tesha akasema hivyo kwa kuiga ongea ya Mariam.

"Bado hizo silabi silabi hazijakaa safi mdomoni kwa Mamu eh? Ila baada ya muda ataongea vizuri kabisa kama zamani," Joshua akadakia kwa kusema hivyo kutokea pale masofani.

Tukaangaliana na Tesha machoni kwa njia ya kukerwa na hilo. Utafikiri alijua lolote, eti silabi silabi!

Bi Zawadi akamwambia Joshua, "Eeeh mazoezi yataendelea kumsaidia sana."

Tesha akakaa kitini na kutoa simu yake huku akiniambia, "Dah! JC
mwana bora jana usingeondoka yaani Dina alipika bonge la msosi."

Nikatabasamu tu.

"Hivi Dina hajamalizaga tu kusoma?" Bi Zawadi akamuuliza Tesha.

"Eti?! Yaani mpaka Leo bado tu anakomaa na vitabu. Siyo mbaya lakini, kwao wanazo kwo' lazima aongeze mamiaka," Tesha akamwambia hivyo.

Inaonyesha wanafamilia wa Tesha walimfahamu Dina pia kutokana na jinsi ambavyo Bi Zawadi alimwongelea, labda hata alikuwa mtoto wa rafiki wa karibu. Simu yangu ikaingiwa na ujumbe, nami nilipouangalia nikakuta ni Tesha ndiyo kanitumia. Sikumtazama kwa sababu tayari nilielewa kwamba alikuwa ananisemesha bila kutaka wengine wajue amesema nini, nami nikausoma.

'Huyu fala amekuja saa ngp,' ikasomeka hivyo sms yake.

Nikajibu, 'Nimemkut mapem. Labd amekuj asubh San'

Bi Zawadi na Joshua wakawa wanaendelea na maongezi mengine, huku mke wa jamaa akiwa ameenda kukaa sofani na mume wake kwa kile kilichoonekana kuwa kumaliza kupika mboga, naye Tesha akawa anamsemesha Mariam huku akiendelea kuchat na mimi.

'Bado analet maigizo yak tu hap,' ujumbe mwingine wa Tesha ukasomeka hivyo.

Nikajibu, 'Uhakika. Ila we mtulizie tu kwanz'

'Na Bi mkubw mbn simwon?'

'Dada yako kampelek kupim, hakuw frsh'

'Aa, barid. Tunakaa hapa hapa kuhakikisha huyu bwege haondok hat na bakul'

Nikatabasamu kidogo na kumwandikia, 'Kuna kitu ntakwambia, ila baadae'

'Kuhusu Joshu?'

'Mke wake.'

'Si uniambie now?'

'Tulia. Ni ubuyu mwing'

'Au siyo? Kama vile nshaanza kunusa haruf yak. We mkal san'

'Haha akil yako hiyo'

'Kam yakwako tu. Twend hat kw Ankia tukaongee'

'Poa.'

Nilipomaliza kumjibu hivyo, nikawatazama wale wengine pale sebuleni na kusimama, kisha nikasema, "Mrembo wangu, me wacha niwakimbie sasa."

Bi Zawadi akasema, "He! JC baba, tunaivisha."

"Ahah, usijali... na ningependa sana kuenjoy mlo. Sema... kuna ka-appointment sehemu... nahitajika kwenda," nikamwambia hivyo.

Nilikuwa nataka tu kwenda kwa Ankia ndiyo nikale maana alikuwa anaandaa msosi wa ukweli! Nilikuwa nimepitisha muda sijala pilau kwa hiyo masikio yalikuwa yamenisimama.

"Una kaapointinamenti wapi na wewe? Utafikiri umeoa!" Bi Zawadi akasema hivyo.

Tesha akacheka kwa furaha na kusema, "Kaapointinamenti? Ma' mkubwa hauendi mbinguni!"

Wengine wakacheka kidogo pia.

"Kisa?" Bi Zawadi akauliza.

Tesha akasimama na kusema, "Unaharibu lugha za watu bwana. Oya... unajua ile 'what's wrong' wazungu wanayoisemaga kuonyesha wanajalii? Mwambie ma' mkubwa aiseme... utacheka! Eti 'wothilong'o mai diya!'"

Wote tukacheka kwa pamoja, naye Mariam akasimama pia huku akiniangalia kwa furaha.

"Ila Tesha! Ahahah... ananizingua tu huyu. Me naisemaga hivyo?" Bi Zawadi akalalamika.

"Hebu iseme umpinge," Khadija akamwambia hivyo Bi Zawadi.

"Whots wrongg," Bi Zawadi akaivuta kama kwa lafudhi ya mzungu.

Tesha akacheka sana.

"Sasa je! Mbona ameisema vizuri?" Khadija akamwambia hivyo Tesha.

"Eeh, umeisema vizuri sana mama. Kama mzungu uliye wewe," Joshua akampamba namna hiyo.

"Muone kwanza! We' ndiyo huendi mbinguni Tesha," Bi Zawadi akasema hivyo kimaringo.

Tesha akasema, "Haya bwana, kisura umeshinda. Twende nikutoe nje bro."

Nikiwa natabasamu tu, nikamwambia Mariam, "Tutaonana baadaye rafiki yangu. Endelea kuchora-chora hizi hapa... na hizi... halafu uje umwonyeshe dada, sawa?"

Akatikisa kichwa kuonyesha uelewa, na baada ya Tesha kuyaangalia yale niliyomwambia Mariam ayachore, akatabasamu kidogo.

Nikaanza kuelekea hapo walipokaa wengine, Tesha na Mariam wakinifuata kwa nyuma, na ile tu ndiyo nataka kumpita Bi Zawadi, Joshua akasimama. Alikuwa amekaa pale ambapo niliketi na mke wake mwanzoni, Khadija akiwa pembeni yake wakati huu, kwa hiyo aliposimama ikawa ni kama vile amenizibia njia. Nikamtazama machoni kwa umakini.

"Kaka... ninaomba kuongea na wewe kabla hujaenda," akaniambia hivyo, kistaarabu tu.

Nikaendelea kumtazama kwa umakini, huku jicho pana likiona namna ambavyo mke wake alituangalia kama mtu mwenye wasiwasi.

"Maongezi tu mafupi ya kiume. Na Tesha pia. Twendeni hapo nje," Joshua akasema hivyo.

Nikatikisa kichwa kuonyesha nimekubali, nami nikamtazama Tesha na kukuta ananiangalia kwa umakini. Yale macho yanayojuana yaani. Haya, nikamuaga Bi Zawadi na Mariam kwa mara nyingine tena, na kisha sisi watatu tukatoka ndani hapo na kwenda pale kibarazani. Jua lilikuwa kali siyo mchezo!

Mimi na Tesha tukasimama kama vile tumemzingira Joshua, akiwa katikati ya ile pembetatu itengenezwayo na watu watatu kusimama pamoja, naye akawa anatuangalia kwa njia yenye upole.

"Eh bwana... nimeona nichukue hii nafasi kuzungumza na nyie kwa pamoja kwa sababu sisi wote ni wanaume, sawa? Tunaelewana kwa mapana zaidi ya vile ambavyo wanawake wanaweza kutuelewa... kwa hiyo... najua nitakayosema mtayaelewa kwa akili pana zaidi..." akaongea namna hiyo.

Alikuwa ameanza kuongea kwa njia iliyoonyesha kwamba alifanyia mazoezi kile ambacho alitaka kusema, nasi tukaendelea tu kutulia huku mimi nikitazama chini, na Tesha akimwangalia jamaa machoni kwa umakini.

"Najua kuna mambo mengi yametokea na... mengi niliyofanya ni mabaya..."

"Hapana, ni yote," Tesha akamkatisha kwa uthabiti.

Joshua akatulia kidogo, kisha akasema, "Ndiyo... yote niliyofanya ni mabaya. Siwezi kusema naweza... kufanya chochote kile kutangua mabaya yote niliyofanya, mabaya yote niliyosema, na kwa wewe Tesha... naelewa bado una hasira na mimi. Najua nimekufanya unichukie sana... na najua itachukua muda mpaka kufikia kipindi ambacho utanisamehe kabisa mdogo wangu... lakini hiyo ndiyo sababu niko hapa sasa hivi. Nimetambua kwamba niliwaumiza sana, na huwa natamani hata muda urudi nyuma ili paap, nifute yote mabaya, lakini haiwezekani kabisa. Ndiyo maana niko hapa sasa hivi... nimerudi ili tuijenge upya tena familia yetu... kuwe na amani tena. Hii yote naifanya ili niweze kuja kufa nikiwa na amani ya rohoni, siyo kuja kuingia kaburini nikiwa nachukiwa na ndugu zangu kabisa Tesha. Nyie ndiyo familia niliyonayo, niliyobakiza, na ninajua... najua nimewakosea sana kwa sababu ya kuendekeza tamaa lakini Tesha... Tesha nakuapia kwa majina ya marehemu wazazi wetu... niko hapa tena ili nirekebishe mambo upya... kwa ajili ya kumbukumbu ya wazazi wetu..." mwamba akaongea hivyo kwa upole.

Nilimtazama usoni kwa mkazo sana, nikiwa nahisi hasira ya kutaka hata kumtandika ngumi moja tu ya pua, lakini nikaendelea kutulia. Tesha akawa ameangalia pembeni baada ya kaka yake kusema hayo, naye Joshua akanitazama.

"Bro... nyie wote ni ndugu zangu. Najua mara ya kwanza tumekutana tulizinguana, na ilikuwa ni makosa yangu. Leo ndiyo nikuombe msamaha kaka. Kwa... kukutukana, kukutishia kukupiga, yaani..."

"Ahah... ungemweza sasa JC?" Tesha akamkatisha kwa kumuuliza hivyo.

Nikacheka kwa pumzi ya chini na kuangalia pembeni.

"Eee... tena unasema kweli. Nisingemuweza... angenivuruga kabisa. Unaona mdogo wangu... matatizo hayo yote ningejisababishia tu kwa kazi isiyokuwa na faida, na... Miryam ndiyo akanifanya nifungue akili yangu tena. Aliniita, akanikalisha, huyu mwenyewe alikuwepo hiyo siku ofisini kwake... aliniita, nikaenda kumsikiliza, nikamwelewa..." jamaa akaongea hivyo.

Tesha akaniangalia na kuuliza, "Da' Mimi alimwita huyu ofisini kwake? Na wewe ulikuwepo?"

Kabla sijamjibu, Joshua akadakia, "Eeh, aliniona pale, nilienda. Miryam huyu! Miryam ndiyo dada! Yaani kama nisingekuwa fala fala huko mwanzo, sasa hivi tungekuwa tunaishi bila misukosuko yote. Na ni makosa yangu..."

Aliongea, yaani, kama mtu mwenye huzuni sana, nami nikatazamana na Tesha kama vile bado hatumwelewi jamaa.

"Sikilizeni. Mimi hapa nipo... kutafuta tu amani tena... kuwaenzi wazazi wetu Tesha, na... ili Miryam na Mariam wawe na furaha. Nakuomba tu Tesha yale mapito ujaribu kuyaweka pembeni mdogo wangu. Hata kama itakuchukua muda mrefu kunisamehe, haina kwere, la muhimu tu kuwe na amani kwa muda huu wote. Mimi sitaacha kuwaonyesha jinsi nilivyobadilika... na Miryam amenisaidia sana, mpaka sasa hivi Mamu haniogopi tena, umeona? Kwa hiyo ni hivyo. Halafu nyie yaani... washkaji sana, tena huyu... JC... msomi hahah... tukiwa good hapa mambo mengi sana yatanyooka," Joshua akasema hivyo.

Alipokuwa ametamka jina langu, alinishika begani kwa njia ya kirafiki, lakini Tesha akautoa mkono wake kwangu taratibu.

"Sikia Joshua. Kama ulivyosema... kukusamehe itachukua muda. Sijui kuhusu wengine, ila mimi... itachukua muda. Kwa hiyo, we' endelea na shenanigan yako ya kutafuta amani, fresh, hakuna shida. Me nimetulia. Sikugusi, sikufukuzi tena. Ila... nitoe tu kaonyo. Ikitokea tu yaani, kale kashetani kako kakakurudia... kakakuingia tu tena ukaamsha majini-wizi yako, aisee! Siyo Mimi, ma' mkubwa, wala Mzee Hamadi watakaoweza kukusave tena. Zamu hii tutatibuana haswa... na nakwambia haya yote JC yuko hapa anasikia, kwa hiyo tusije tukalaumiana. Ushanisoma?" Tesha akasema hivyo kwa sauti ya chini lakini imara.

Kijana huyu alikuwa ameongea kile kitu ambacho hata mimi ningesema pia, lakini kwa wakati huu nilikuwa nataka kuyatimiza hayo maneno ya Tesha kwa sababu nilijua vizuri sana kwamba hako kashetani bado kalikuwa kichwani kwa huyo mwanaume.

Joshua akajichekesha kidogo na kusema, "Haina shida mdogo wangu. Usikonde. Umekuwa simba kweli, nakuaminia sana."

"Imeisha hiyo," Tesha akasema hivyo na kutazama pembeni.

Simu yangu ikaanza kuita papo hapo, nami nikaitoa na kukuta ni Ankia ndiye aliyekuwa ananipigia. Nikapokea na kumsikia mwenye nyumba wangu akiniambia niende kunywa supu ya kuku na pilau ilikuwa mbioni kuiva, nami nikamwambia poa.

Nikashusha simu na kusema, "Nahitaji kuwahi."

Niliongea hivyo bila kumwangalia Joshua hata kidogo, huku nikiona yeye ananikodolea tu, nami nikampa Tesha ishara ya kichwa kuwa anifuate. Tukatoka hapo kibarazani bila kusema lolote lile kwa huyo Joshua, tukimwacha anatusindikiza tu kwa macho mpaka tulipokwenda nje.

Nikawa nimemweleza Tesha kwa ufupi kuhusiana na lile suala la kukutana na Joshua kazini kwake Miryam, nikimwambia ilikuwa ni wakati ambao nilienda kwa dada yake ili kumzungumzia Mariam, ikionekana ni kutokea kipindi hicho Miryam ndiyo alikuwa ameanza kumvuta tena Joshua kwa ajili ya kuleta amani na ndugu yake. Lakini ndugu mwenyewe alikuwa ovyo!

Nilikuwa najihisi kuchafukwa rohoni yaani! Basi tu yaani huyo mwanaume hakuwa muungwana kabisa hata kwa jicho la kawaida tu, yaani hakufaa. Mpaka anatumia uzito wa kumbukumbu ya vifo vya wazazi wao ili tu ajionyeshe kuwa mtu mpya eti, kiukweli alinifanya nimchukie mno. Ila zake zingetimia tu, na hazingekawia.

Tukaingia kwa Ankia pamoja na kumkuta akiwa na mama Chande, best yake. Ndani palinukia kweli pilau na vitunguu swaumu na kuku, na kama kawaida yake, Tesha akaanza kutaniana na wanawake na kuwafanya wacheke kwa furaha. Inaonyesha Ankia alikuwa amepata msaada wa mapishi kutoka kwa mama Chande ndiyo maana aliwahi kutengeneza vyakula, na kwa msukumo wa jiko la gesi mambo yalikuwa fasta tu.

Wanawake wakiwa wamekaa hapo sebuleni, sisi tukaelekea chumbani kwangu ili kwanza tusimuliane mambo yetu vijana ambayo Tesha alipenda kupita maelezo. Alitaka kujua kuhusu mke wake Joshua, lakini mimi nikataka aanze yeye kunisimulia kuhusiana na yule Winny. Yaani siku wamekutana ilikuwa vipi na mpaka sasa hivi walikuwa wapi.

Ah, akasema yaani yule alikuwa na dharau sana. Eti alipokwenda kukutana naye, mwanamke huyo alimwona kuwa kama mtoto mdogo na alifikiri hangeweza kazi. Winny hakuwa wa aibu, alimpa Tesha penzi lakini alikuwa haridhiki. Tesha akasema alipiga vitano bila kutumia dawa na bado mwanamke akawa anataka waendelee!

Nikacheka na kumwambia huyo alikuwa anataka kumkomoa tu, na yeye akasema ni kweli kabisa kwa kuwa baada ya hapo alipoendelea kumtafuta kwa simu demu akawa anamkwepa tu; kumaanisha alikuwa na mishe zake nyingine za kuzungushia utamu. Ila akadai kwamba alimkubali sana huyo mwanamke kwenye ukataji wa viuno, na angalau alimla bila gharama!

Hiyo yote ilinifurahisha sana hasa kutokana na njia yake Tesha ya kuongea, na sasa ndiyo akataka kujua kuhusu mke wa kaka yake. Nikamwambia kwamba huyo mwanamke alikuwa ananitaka, nami nikamwelezea mambo yote yaliyotokea pale kwao baina yangu na huyo Khadija.

Akashangaa! Yaani haingeingia akilini mwake kufikiri huyo mwanamke alikuwa wa hivyo, akieleza sababu kuwa Khadija alikuwa mpole sana na mtulivu wa ndoa, ila ndiyo hapa akaona ukweli wa ule msemo 'kamwe usichukulie kuyajua yaliyo ndani ya kitabu kwa kuhukumu tu jalada lake.'

Nikamwambia sikuwa na uhakika wa kitu cha kufanya kuelekea suala hilo, lakini Tesha akasema ish! Piga tu! Kama mwanamke aliitaka kwa nini anyimwe? Nikacheka na kumuuliza hana kwere kwa sababu ya mwanamke huyo kuwa shemeji yake? Akaniambia hakuna kitu kama hicho, yaani hata kama Khadija angekuwa amejisogeza kwake na kuanza kumsugua-sugua miguu, hata yeye angepiga tu!

Aisee, nikamwambia ndiyo hivyo, na mimi sikuwa na ile kusema nimemtaka sana huyo mwanamke ila kama angelazimisha mambo basi ningemkoa tu na yeye. Tesha akasema tena kwa hilo aliniunga mkono wake kwa asilimia zote, akifikiri ni masuala ya kujifurahisha tu, kumbe mimi nilikuwa nataka kuchimba zaidi ndani ya suala la maovu ya Joshua.

Maongezi hayo yote yalifanywa kwa sauti ya chini ili wanawake pale sebuleni wasitusikie, na ndipo Ankia akawa ametuita twende huko. Nikamwambia Tesha huo ulikuwa ni mwito wa kunywa "thupu" ya kuku, na sikuwa nimekosea.

Kweli tukakuta Ankia akiwa ametuwekea mimi na Tesha supu pamoja na nyama kwenye mabakuli, nasi tukakaa ili kujinywea. Alikuwa kwenye harakati za kwenda kuanza kukaanga nyama za kuku ili aziunge vizuri kwa mchuzi wa nyanya na mapocho ya upishi wajuayo wanawake, nasi tukaendelea kunywa huku tukipiga story.

Mada ilikuwa sanasana kuhusiana na Simba na Yanga, jinsi timu hizi zilivyokuwa zimeingia kwenye michuano ya kimataifa barani mwetu, na mechi ya watani wa jadi iliyokuwa inakaribia kuchezwa. Ubishi na maneno ya sutu uliwajaa sana Tesha na mama Chande, hadi Tesha alikuwa anamfanyia mwanamke huyo zile pigo za kike za "ng'oo ng'oo" huku akikandamiza pua kwa kidole, nasi tukawa tunacheka sana. Wanaume tulikuwa Simba, wanawake Yanga, kwa hiyo utani wa maneno hapa ulikuwa mwingi sana.

Tukiwa tunaendelea kufurahia maongezi bwana si simu yangu ikaita? Mpigaji hakuwa mwingine ila madam Bertha, mwanamke shupavu, muuaji, na mwenye jeuri kama lote. Nikapokea hapo hapo na kumsikiliza. Alikuwa ananitaka niende kule Royal Village sasa, ikiwa ndiyo muda alioona unafaa wa mimi kutoka huku nilikokuwa. Akasema nisisahau kubeba na unyama wote niliokuwa nimetengeneza, nami nikamwambia poa. Akakata simu.

Nikaangalia muda; saa tisa kasoro. Dah! Huyo mwanamke alijua kunikatishia hamu! Yaani na hapa pilau na kuku ningezikosa tu kisa kufuata amri zake! Lakini haikuwa na noma. Nikamtaarifu Ankia kuhusu safari yangu ya ghafla kuelekea jijini zaidi, naye akaanza kununa. Eti yaani kanipikia pilau halafu naondoka? Sawa tu.

Nikacheka kidogo na kumwambia hapo naenda kusaka hela za likizo ndiyo maana, ila nikamwambia ningekuja tu kuila pilau yake baadaye. Tesha akaniuliza ikiwa hii ndiyo dharura iliyokuwa imefanya niondoke na kwao pia, nami nikakubali, nikisema kuna jamaa aliniita ili akanipange juu ya mambo fulani.

Kwa hiyo nikatoka hapo sebuleni na kwenda chumbani tena, na nilikuwa nawaza labda niende kuoga tena ila kutokana na uharakishi wa madam nikaamua tu nibadili mavazi na kuvaa kwa mtoko bomba zaidi. Nikajitengeneza vyema, kisha nikachukua lile begi langu la mgongoni na kulipunguzia vitu nilivyokuwa nimeweka humo, halafu nikachukua mifuko ile yenye madawa ya cocaine na kuitumbukiza kwenye begi.

Nilihakikisha kuacha nguo chache na vifaa nilivyochukua hospitali ili dawa zifichike pia, kisha nikavaa viatu na kutoka hatimaye. Marafiki zangu walifikiri labda nataka kusafiri kwa siku kadhaa kutoka huku, lakini nikawahakikishia kwamba ningerudi leo leo, ama kesho. Tukaagana vizuri baada ya hapo, nami nikaondoka kwenda kupanda daladala.

★★

Safari ya kuelekea Makumbusho ilidumu kwa masaa mawili kabisa. Hii ilisababishwa na msongamano wa magari hasa tulipofikia eneo la Keko, na kwenye ile round-about pale sipajui jina, lakini ilikuwa jam kali kweli mpaka kuhitaji mwongozo wa askari wa usalama barabarani. Kwa hiyo nimekuja kufika Makumbusho ikiwa ni saa kumi na moja jioni, na kwa muda wa nusu safari nilikuwa nimesimama baada ya kumpisha mwanamke mjamzito aketi kwenye siti yangu, hivyo miguu ilikuwa inaita kwa kiasi fulani.

Nikatoka Makumbusho, kama kawaida nikapanda Uber na kuanza kuitafuta Royal Village Hotel. Nikiwa njiani, nikaona nimpigie madam Bertha kumuuliza kama na leo nilitakiwa nipande lifti pale hotelini, kisha labda kwenye lifti hiyo ningekutana na mwanamke ambaye angenipa funguo ya chumba ambacho madam angekuwepo. Akaniambia niache ujinga na nifike kule tu kisha nimjulishe, na ile nataka tu kusema kwamba nimekaribia, akakata simu. Doh!

Nikajikuta tu nacheka mwenyewe, lakini hiyo haikumaanisha kwamba nilikuwa nimeshasahau dhumuni langu la kufanya haya yote. Bado, pamoja na kuwa nimejiweka upande wake, huyo mwanamke alikuwa ni adui yangu. Tumeangalia filamu nyingi zinazoonyesha kwamba mara nyingi ukitaka kufanikiwa kuwaangusha maadui zako, basi jiweke karibu nao ili uweze kufanikiwa kuwaangusha kwa njia bora.

Ndiyo nilichokuwa nikikifanya wakati huu. Ningeendelea kujichekesha tu heheh ili siku huyo mwanamke akija kunikuta serious, ajue kuna watu wasiopenda michezo kwenye maisha ya wengine kama ile aliyoifanya kwangu mpaka kuua mwanadamu mwenzetu. Na sikuwa nimempa taarifa askari mpelelezi Ramadhan kuhusu mkutano wangu huu na mwanamke huyo, ili nione kwanza huu mchezo ungenipeleka wapi kwa leo.

Nikaifikia Royal Village hatimaye, nami nikamlipa dereva na kwenda ndani ya geti. Nikatembea mpaka kufikia usawa wa bustani na kisha nikampigia tena madam. 'Haya ndiyo nimefika, niende juu au?' Akarusha dongo kwa kusema niache kuwa na kiherehere, na kwamba bado yeye hakuwa amefika hapo hotelini ingawa alikuwa anakaribia.

Nikamuuliza yuko sehemu ipi kwa sasa. Akasisitiza tu tena kwa kusema ndiyo alikuwa amekaribia kufika hotelini hapo, yaani ni dakika mbili tu angeingia, hivyo niende kumsubiri ule upande wa maegesho ya magari ya nyuma kwenye jengo hilo. Sikudhani kwenye hoteli hiyo kulikuwa na maegesho ya namna hiyo lakini hilo lilikuwa jambo hakika, hivyo nikamkubalia na kukata simu, kisha nikazungukia mpaka upande huo kwenda kumsubiri. Ah kumbe na hoteli hii ilikuwa ya ubora bwana!

Maegesho ya huku nyuma yalikuwa mapana, safi, nguzo ama ngome nyingi nene zikilibeba jengo hilo la hoteli na magari ya maana yakionekana kuegeshwa hapa na kule. Hizi ndiyo zile sehemu ambazo mara nyingi tunaonaga kwenye filamu hasa za wazungu jinsi ambavyo majambazi hupenda kuzitumia kwa ajili ya kutoroka wakishafanya maovu yao, na kweli hapa nilikuwa nimekuja kukutana na majambazi!

Nilitembea mpaka kufikia sehemu ambayo iliniruhusu kuuona mlango wa lifti ya nyuma kwenye jengo hilo, na bila shaka baada ya Bertha kufika tungeitumia hiyo kuelekea juu, hivyo nikasimama usawa wa nguzo moja na begi langu mgongoni kumsubiri madam afike.

Hakukuwa na nafsi hata moja iliyoonekana kwa upande huu, pakiwa kimya kweli, nami nikawa naangalia mpangilio maridadi wa sehemu hiyo pamoja na CCTV camera zilizowekwa kwenye kila pembe. Nikasikia kengele ya mlango wa lifti iliyoashiria kwamba kuna watu walikuwa wanatoka, na ile nimenyanyua tu uso wangu kutazama huko, nikajikuta nakunja sura kimaswali kutokana na kutotegemea kabisa kumwona niliyemwona.

Mwanamke niliyemfahamu, akiwa amevaa gauni jeupe lililo la mtindo mzito kama sweta laini, refu kufikia miguuni, lenye kubana mwili wake ulioumbika vyema. Alikuwa ameshika mkoba mkononi, na hilo gauni liliacha mikono yake myeupee wazi kutokea mabegani, na aisee alinifanya nibaki nikimtazama kwa mshangao sana. Bibie Miryam!

Yaani sikuwahi kutegemea kumwona hapo kabisa, tena akiwa ndani ya mtindo mzuri kama huo uliompendezesha vibaya mno. Alikuwa amevaa viatu vya kuchuchumia vyekundu, vikiwa vimeendana na rangi ya mkoba wake, na mwonekano huo uliniambia kwamba alikuwa sehemu hiyo kwa mkutano wa masuala binafsi; labda date na mtu wake, na huku ilikuwa ni mbali kweli!

Ila ilimfaa, nami nikaona nijibanze kwenye nguzo hiyo ili asiweze kuniona kabisa. Nisingefikiria hata mara moja kwamba ningemwona hapo hasa kwa kujua alikwenda zake kazini baada ya kumpeleka mama mkubwa wake hospitali. Alikuwa anakuja upande wangu lakini kwa kupitilizia sehemu iliyokuwa imeegeshewa magari, nami ndiyo nikawa nimeiona ile pickup yake.

Pamoja na kuwa mwanamke mwenye mvuto sana lakini hakupenda makuu mno, na kuwa mtu aliyethamini zaidi mambo yaliyokuwa na maana kwake kuliko kutafuta vitu vya kumpa sifa tu; yaani huyu hata kama angekuwa ameamua kutembelea gari aina ya Range Rover Evoque asingeshindwa, lakini aliendelea kutumia pickup iliyokuwa ya baba yake ili kumuenzi. Lakini dah! Miryam ndiyo alikuwa maana ya mwanamke. Sijui nani tu alikuwa anakula hapo!

Akawa amenipita bila kuniona maana nilijibanza vizuri, nami nikawa naangalia miondoko yake ya taratibu ambayo ingemfanya mwanaume yeyote agande kumtazama kwa jinsi alivyokuwa amebarikiwa huyo dada. Siyo kwa sura tu, siyo kwa shepu tu, hata tabia, yaani kila kitu kwake ni kama kilikuwa kamili.

Sikutaka anione maana mishe zilizokuwa zimenileta huku hazikuwa nzuri kuendana na jinsi dada wa watu alivyokuwa ananifahamu, lakini Shetani bana, akaona aniharibie tu. Sijui labda namsingizia bure? Simu yangu ikaanza kuita. Muito wa simu ulikuwa ni mdundo wa wimbo wa Ozuna uitwao "Una Lodura," wabrazili hao na ni ngoma kali, hivyo sauti ya mwanzoni tu ikawa imesikika kwa bibie. Agh!

Nimeshtuka ile nataka kuitolea sauti, sauti ya viatu vya Miryam ikakata, na hilo likaniambia kwamba alikuwa amesimama, kwa hiyo ikanibidi nitoke hapo kwenye hiyo nguzo na mimi nijifanye kwamba ndiyo nilikuwa nimetokea tu upande huo na sikuwa nimemwona. Nikaweka uso makini kweli nikiiangalia simu, na nilikuwa nimeanza kupiga hatua chache kisha nikasimama.

Mpigaji alikuwa ni rafiki yangu mmoja wa Mwanza, hivyo nikaitolea tu simu sauti huku nikimrushia laana ya kimoyomoyo huko alikokuwa kwa kusababisha nikachomeshwa namna hiyo. Nikajifanya naangalia tu pembeni kama vile sina habari na mwanamke huyo ambaye nilijua wazi kwamba alikuwa amesimama na anaangalia upande wangu, na ndipo hatua zake kunielekea zikaanza kusikika.

Nikafumba macho kwa kutotaka jambo hilo kabisa, kwa sababu nilihofia sana kuhusiana na mambo ambayo yangetokea ikiwa Bertha angefika na kunikuta nikiwa na Miryam hapo. Sijui ni kwa nini tu yaani mwanamke huyu alitakiwa kuwa hapo kwa muda huo! Ningepaswa nimwepuke upesi, kwa njia yoyote ile.

Nikamgeukia na kujifanya kushangaa, kama vile ndiyo nimemwona sasa, naye akawa ananifata huku funguo ya gari lake ikiwa kiganjani, na akitabasamu kiasi.

"Hey, vipi?" akaniuliza hivyo.

"Safi tu. Ih! Upo huku kumbe?" nikamsemesha namna hiyo.

"Ndiyo," akajibu hivyo na kusimama mbele yangu.

"Mishe gani?"

"Aa... nimekuja tu kukutana na mtu, alikuwa ameniita huku ndiyo nikaja haraka," akaniambia hivyo na kasauti kake katamu.

"Aaa... umedamshi kweli. Lazima uwe mkutano wa maana," nikazungumza kwa wasiwasi kiasi.

"Ahah... acha bwana. Ni mikutano tu ya kikazi," akasema.

"Aaa... sawa. Si ndiyo unaondoka?"

"Eeh."

"Haya sawa, basi,... baadaye. Kama kawaida tu, nitakuja kwa Mamu," nikamwambia hivyo kama namfukuza yaani.

Akauliza, "Na wewe? Mbona uko huku?"

"Kuna... na mimi kuna mtu nakutana naye... hapa. Ni rafiki. Kwa hiyo, we' nenda tu, si unaenda kuendelea na kazi? Nisikucheleweshe," nikamwambia.

Akawa ananiangalia kwa utafakari, naye akasema, "Mbona kama una wasiwasi? Kuna tatizo lolote?"

"Hapana. Kila kitu kiko sawa," nikamwambia hivyo na kutabasamu.

Akatikisa kichwa kuonyesha uelewa, naye akasema, "Okay. Basi... tutaonana baadaye... kama ulivyosema."

Nikatikisa kichwa kukubali hilo.

Akageuka na kuanza kuondoka, nami nikaangalia pembeni na kushusha pumzi ya utulivu. Nikawaza kuwa angalau tu kama dada wa watu angeondoka, maana, hapo sikuwa sehemu nzuri kabisa ya....

Ilikuwa mapema sana kufikiri kwamba nilipata ushindi kwa kumwondoa Miryam upesi, kwa sababu alikuwa amepiga hatua chache tu kisha akasimama tena. Nikamwangalia. Akanigeukia tena na kunitazama, kisha akaanza tena kurudi kwangu. Aisee! Sijui alikuwa amesahau nini!

Akafika karibu tena, nami nikajitahidi kuonyesha utulivu usoni lakini moyoni palidundika mithili ya ngoma, naye akasema, "Nilikuwa nataka nikwambie jambo fulani."

Nikatikisa kichwa kuonyesha aendelee.

"Ni kuhusu jana... na... kila kitu ambacho kimeendelea kwa Tesha na Mamu. Huwa... sitegemei sana mtu yeyote anisaidie kwa... mambo ya familia yaani, sijazoea... ila... kwa yote ambayo wewe unafanya... nataka tu kusema asante..." akaongea hayo.

Dah! Hii ingepaswa kuwa pindi moja nzuri sana maana huyu dada alikuwa ameanza na kunisemesha kabisa, tena kunishukuru, lakini muda na sehemu ya tukio hili haikufaa. Nilikuwa naangalia upande ule wa mwingilio wa magari kwa wasiwasi kiasi, nikiomba Mungu Bertha aendelee kukawia tu.

Miryam akaendelea kusema, "Niliongea na Tesha hiyo jana... na jinsi alivyokuwa ameonyesha kutulia kiakili kwa kweli... sijaiona kwa muda mrefu kiasi. Anasema yote hiyo imewezekana eti kwa sababu ulimpa therapy ahahah..."

Nikalazimisha kicheko pia na kusema, "Eeh, ndiyo, ndiyo..."

"Yaani una effect nzuri hata kwa Mamu, mpaka ameanza na kuongea tena. Niseme tu... yaani, hatujawahi kuzungumza sana ndiyo maana nimeona nichukue hii nafasi ku..."

Maneno ya Miryam yakakatishwa baada ya sote kuona gari aina ya Harrier new model ya silver likiwa linaingia, nami nikajiambia eh Mungu! Huyu mwanamke alipaswa kutoka hapa sasa hivi!

Miryam yeye akiwa haelewi somo akaona aendelee kuzungumza tu kutoa shukrani yake, na hilo gari likaingia sehemu ya maegesho isiyo mbali sana na hapo tulipokuwa tumesimama. Dereva aliposhuka hakuwa mwingine ila yule baunsa wa madam, naye akaonekana kuufungua mlango wa nyuma wa gari.

Nikamgeukia Miryam na kumkatisha kwa kusema, "Miryam... tafadhali... tuta... tutaongea wakati mwingine... yaani, tukionana tena, sawa?"

Akaibana midomo yake taratibu huku macho yake yakiwa kwangu kwa utulivu tu.

"Unaweza kwenda tu Miryam. Naowasubiri wamefika, we'... kaingie kwenye gari dada..."

Yaani nilikuwa najaribu kumfukuza kistaarabu, na nilihitaji sana aondoke maana sikutaka Bertha amjue Miryam. Katika watu ambao sikutaka mwanamke huyo awaingie kabisa ilikuwa ni huyu dada, lakini kwa hapo nikawa nimechelewa.

"HB..." sauti ya Bertha ikasikika akiniita.

Ah!

Nikageuka kumwangalia, Miryam bado akiwa hapo hapo, nami nikamwona madam akiwa anakuja kwa mwendo wa madoido. Alikuwa amevaa gauni jeupe fupi sana lililoubana mwili wake. Mapaja yalikuwa wazi, mikono na mabega yalikuwa wazi pia, na sehemu ya mbavu zake ilikuwa wazi pia kama vile gauni hilo limechanwa humo pembeni kwa njia ya urembo.

Miguuni alivaa mabuti ya kike yenye rangi ya kahawia, na usoni alikuwa amevaa miwani pana nyeusi ya urembo. Baunsa wake alikuwa anafata nyuma huku ameitanua mikono na sura yake ikiwa makini, nao wakafika karibu yetu; Bertha akisimama karibu nasi zaidi na kuitoa miwani yake machoni.

Nikaendelea kuonyesha utulivu tu, huku nikiona jinsi Bertha alivyokuwa akimtazama Miryam kwa macho yenye udadisi, kisha akaniangalia mimi. "Za jioni?" akauliza hivyo.

"Fresh tu," nikajibu hivyo kwa sauti ya chini.

"Nimefika wakati mbaya? Mlikuwa mna..." Bertha akasema hivyo.

"Hamna, me ndiyo nimefika tu upande huu sa'hivi..."

"Sikumbuki kukwambia uje na mtu," Bertha akanikatisha kwa kusema hivyo.

Nikamwangalia Miryam kiufupi, ambaye alikuwa ananiangalia kwa utulivu tu, nami nikamwambia Bertha, "Hapana. Nimekuja mwenyewe. Sijaja na mtu."

"Huyu ni nani?" Bertha akaniuliza.

Miryam akaanza kusema, "Mimi ni..."

"Nimekutana tu na huyu dada hapa, alikuwa amedondosha funguo yake hiyo... ndo'... nikamsaidia kuipata..." nikamkatisha Miryam.

Jinsi ambavyo mwanamke huyo aliniangalia, yaani, alikuwa ndani ya mshangao mzito bila shaka, na ilieleweka kwamba hakuwa amenielewa.

Bertha akaniuliza, "Kwa hiyo ndiyo mmekutana hapa hapa?"

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Hamfahamiani kabisa?" Bertha akaniuliza tena.

Macho yake Miryam yakanitazama kwa njia ya subira, na najua alikuwa anataka kuona ningejibu nini, na aisee! Roho iliniuma sana kwa kitendo nilchokifanya.

Nikatikisa kichwa kukataa na kumwambia Bertha, "Hapana. Simjui."

Siwezi kujua undani wa mshtuko niliofanya Miryam auhisi hapo aisee! Aliniangalia kwa njia ya kawaida tu, lakini naelewa alikuwa akinishangaa sana. Sana!

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom