Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,139
- 4,218
======
Wazee waeleza sababu zinazosababisha kuuwawa
WAZEE wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wameeleza sababu inayosababisha wazee mengi kupoteza maisha kabla ya muda wao ni kulazimishwa kugawa urithi wa mali walizonazo kwa watoto wao na wanapokataa wanatengenezewa mazingira ya kuuawa kwa kusingiziwa cha ushirikina.
Katibu wa Baraza la wazee Halmashauri hiyo Laurent Nkwambi ameyabainisha hayo leo tarehe 21/06/2023 wakati wa kampeni ya Rais Dk. Samia Suruhu Hassani ya msaada wa kisheria uliofanyika katika kijiji na kata ya Ngogwa,amesema kila mzee anatakiwa kujisimamia wakati wa ugawaji wa mirathi kwa watoto na sio kulazimishwa.
Amesema, wazee wengi hususani wanaoishi pembezoni na maeneo ya vijijini wamekuwa wakiuwawa na watoto wao ndani ya familia kwa kulazimishwa kugawa urithi na wanapokata wanatafutiwa sababu au mazingira ya kuuwawa kwa kisingizio cha ushirikia hivyo haitakubalika kuendela kutokea.
“Manispaa hii inajumla ya wazee 6692 na asilimia 50 ya wazee wanaishi maeneo ya pembezoni ambapo ndipo kunafanyika vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi yao na mauaji, yote haya yanasababishwa na watoto kutaka mgawo wa mali hususani mashamba”Alisema Nkwambi.
Mkazi wa eneo hilo Victoria Thomasi amesema,alijifungua watoto 10, kati ya hao watatu walipoteza maisha kwa sababu mbalimbali, mmoja aliugua ugonjwa wa surua, wapili alipata kiharusi na watatu alifariki akiwa ni mama mtu mzima, lakini chakushangaa wajukuu zake wanatapakaza maneno mitaani kuwa yeye ni mchawi.
Naye Wakili wa serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi amesema,wananchi hawana elimu ya kutosha juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wazee na makundi maalumu, maswala ya mirathi na wosia inasababisha kuwa na migogoro kwenye familia hivyo watahakikisha wanawafikia na kuwaelimisha.
Nipashe