Shinyanga: Wazee walalamika kuuawa kwa njama wasipogawa urithi

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,138
4,213
Nipashe 1.jpg

======

Wazee waeleza sababu zinazosababisha kuuwawa

WAZEE wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wameeleza sababu inayosababisha wazee mengi kupoteza maisha kabla ya muda wao ni kulazimishwa kugawa urithi wa mali walizonazo kwa watoto wao na wanapokataa wanatengenezewa mazingira ya kuuawa kwa kusingiziwa cha ushirikina.

2.jpg

Katibu wa Baraza la wazee Halmashauri hiyo Laurent Nkwambi ameyabainisha hayo leo tarehe 21/06/2023 wakati wa kampeni ya Rais Dk. Samia Suruhu Hassani ya msaada wa kisheria uliofanyika katika kijiji na kata ya Ngogwa,amesema kila mzee anatakiwa kujisimamia wakati wa ugawaji wa mirathi kwa watoto na sio kulazimishwa.

Amesema, wazee wengi hususani wanaoishi pembezoni na maeneo ya vijijini wamekuwa wakiuwawa na watoto wao ndani ya familia kwa kulazimishwa kugawa urithi na wanapokata wanatafutiwa sababu au mazingira ya kuuwawa kwa kisingizio cha ushirikia hivyo haitakubalika kuendela kutokea.

“Manispaa hii inajumla ya wazee 6692 na asilimia 50 ya wazee wanaishi maeneo ya pembezoni ambapo ndipo kunafanyika vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi yao na mauaji, yote haya yanasababishwa na watoto kutaka mgawo wa mali hususani mashamba”Alisema Nkwambi.

Mkazi wa eneo hilo Victoria Thomasi amesema,alijifungua watoto 10, kati ya hao watatu walipoteza maisha kwa sababu mbalimbali, mmoja aliugua ugonjwa wa surua, wapili alipata kiharusi na watatu alifariki akiwa ni mama mtu mzima, lakini chakushangaa wajukuu zake wanatapakaza maneno mitaani kuwa yeye ni mchawi.

Naye Wakili wa serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi amesema,wananchi hawana elimu ya kutosha juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wazee na makundi maalumu, maswala ya mirathi na wosia inasababisha kuwa na migogoro kwenye familia hivyo watahakikisha wanawafikia na kuwaelimisha.

Nipashe
 
Inasikitisha, halafu wazee nchi hii ni wachache sana,tatizo kuzaa watoto 20 halafu hauwawekei msingi wa kujitegemea.Halafu ni ngumu kulea watoto 20 ,matokeo yake ndo haya.
Tatizo watu wa kanda ya ziwa wanatumia akili kidogo miguvu mingi wanahisi kuzaliana kama nguruwe ndo mafanikio matokeo yake wanaingia kwenye mtego wa kuuawa
 
ukiona wenzio wananyolewa we tia maji .... tujitahidi kuwapenda na kuwatunza wazeee na tujitahid jenga misingi ya watoto wetuu
 
Inasikitisha, halafu wazee nchi hii ni wachache sana,tatizo kuzaa watoto 20 halafu hauwawekei msingi wa kujitegemea.Halafu ni ngumu kulea watoto 20 ,matokeo yake ndo haya.
Tatizo linaanzia kwa wazee wenyewe, wanapenda kuwa na idadi kuwa ya watoto bila ya kuwa na mipango madhubuti wala malengo yoyote kuhusu hao watoto wenyewe..
Tatizo watu wa kanda ya ziwa wanatumia akili kidogo miguvu mingi wanahisi kuzaliana kama nguruwe ndo mafanikio matokeo yake wanaingia kwenye mtego wa kuuawa
Waliambiwa wazae tu, serikali will take care of the rest
 
Mitoto ya ovyo ipewe laana na sio maua, tatizo sio kuzaliwa masikini, tatizo kufa masikini, wapo watu wamezaliwa masikini Ila wamepambana wametafuta wenyewe, diamond kazaliwa kwenye Mali, au RP mengi, tuache kuwalaumu wazee wetu kwa uvivu wetu, na kung'ojea mgao, au kusubili kila mtu afe na chake, kuuzwe hapa, huo ni ufala Sana.
 
Yaani mzee ana ng'ombe 1000 ,mbuzi kama wote halafu eti watoto wake wanaishi maisha ya kuunga unga hawana nyuma wala mbele! Kwanini usiwagawie hizo ng'ombe ili waishi vizuri?

Disclaimer:

Sisapoti mauaji ya wazee na vikongwe naamini kuwa wao ni hazina kubwa ya maarifa kwa vizazi vipya.
 
Unazaa Watoto wengi huwezi kuwatunza wala kuwalea unategemea nini. Acha wauawe
Ni ujinga kuzaa Watoto usioweza kuwatunza. Hata wanyama hawafanyi kitu kama hicho.
 
======

Wazee waeleza sababu zinazosababisha kuuwawa

WAZEE wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wameeleza sababu inayosababisha wazee mengi kupoteza maisha kabla ya muda wao ni kulazimishwa kugawa urithi wa mali walizonazo kwa watoto wao na wanapokataa wanatengenezewa mazingira ya kuuawa kwa kusingiziwa cha ushirikina.

2.jpg

Katibu wa Baraza la wazee Halmashauri hiyo Laurent Nkwambi ameyabainisha hayo leo tarehe 21/06/2023 wakati wa kampeni ya Rais Dk. Samia Suruhu Hassani ya msaada wa kisheria uliofanyika katika kijiji na kata ya Ngogwa,amesema kila mzee anatakiwa kujisimamia wakati wa ugawaji wa mirathi kwa watoto na sio kulazimishwa.

Amesema, wazee wengi hususani wanaoishi pembezoni na maeneo ya vijijini wamekuwa wakiuwawa na watoto wao ndani ya familia kwa kulazimishwa kugawa urithi na wanapokata wanatafutiwa sababu au mazingira ya kuuwawa kwa kisingizio cha ushirikia hivyo haitakubalika kuendela kutokea.

“Manispaa hii inajumla ya wazee 6692 na asilimia 50 ya wazee wanaishi maeneo ya pembezoni ambapo ndipo kunafanyika vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi yao na mauaji, yote haya yanasababishwa na watoto kutaka mgawo wa mali hususani mashamba”Alisema Nkwambi.

Mkazi wa eneo hilo Victoria Thomasi amesema,alijifungua watoto 10, kati ya hao watatu walipoteza maisha kwa sababu mbalimbali, mmoja aliugua ugonjwa wa surua, wapili alipata kiharusi na watatu alifariki akiwa ni mama mtu mzima, lakini chakushangaa wajukuu zake wanatapakaza maneno mitaani kuwa yeye ni mchawi.

Naye Wakili wa serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi amesema,wananchi hawana elimu ya kutosha juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wazee na makundi maalumu, maswala ya mirathi na wosia inasababisha kuwa na migogoro kwenye familia hivyo watahakikisha wanawafikia na kuwaelimisha.

Nipashe
Tatizo hili limetengenezwa na wazee wenyewe, kijana akioa kwa tamaduni ya kisukuma anaishi kwa wazazi wake, na inakuwa sehemu ya nguvu kazi yake kwenye Mashamba na mifugo yake. Atatoka kwa mzazi wake baada ya kupewa shamba.
Kwa ufupi kijana na familia yake wamekuwa wakiishi katika hali ya kutegemea raslimali za wazazi wao
 
Back
Top Bottom