Nitajie wasanii wawili Tanzania ambao ni genius sana

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,793
45,428
Kwa mimi binafsi naona
1. Nikki Mbishi wa Tamaduni Muzik
2. Leonardo wa Cheka Tu

Wote ni wasomi wenye taaluma zao ambazo, zinahitajika kichwa Cha hesabu Nikki ana degree ya computer science huku Leonard yeye ana bachelor ya water resources engineering.

Kwenye interview zao utagundua wako smart wanafuatilia current issue. Na kwenye kazi zao ndo Balaa huyu wa stand up comedy yuko vizuri na Nikki yeye ni hatari.

Taja wa kwako
 
Genius kwenye kipengere gani mkuu. IQ kubwa au fani yake? Kama u-genius kwenye fani yaani mbinu za kuji-adjust kwenye industry yake nampa kura diamond platnumz, kama genius unamaanisha IQ hapo sijui kwa kweli sina taarifa za kitaaluma za msanii yoyote.
 
Kwa mimi binafsi naona
1.Nikki mbishi wa tamaduni muzik
2.Leonardo wa cheka tu

Taja wa kwako
1. Huwezi kuwa Comedian halafu usiwe Genius na hata Kisaikolojia Watu ambao Kiasili ni Wacheshi na wapenda Utani huwa na IQ Kubwa kwani hadi kumfanya Mtu au Watu wacheke kwa kile ulichokibuni Kichwani mwako ( tena kwa haraka haraka ) si Kazi ya Kitoto na rahisi hivyo basi Kwangu Mimi Mtu Genius ni Mchekeshaji Marehemu Mzee King Majuto na ndiyo hadi sasa wengi Wanajaribu tu ila sijaona bado hata wa Kumkaribia.

2. Pia kwa Afrika ya zamani ( wakati wa Ukoloni ) na ilivyokuwa huku Waafrika wote wakiutafuta Uhuru wao kwa njia ya Vita kutoka kwa Wazungu ( Wakoloni ) ili waupate lakini kwa Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. wala hakutumia Nguvu au Silaha Kuuomba kutoka kwa Wazungu na badala yale alitumia tu Akili, Hekima na Busara hivyo Kwangu nae ni Genius wangu.
 
Back
Top Bottom