Nissan Dualis: Dxf Nyingine Imewaka Moto

Ni katika muendelezo ule ule wa Dualis a.k.a sigala na vayolensi za moto, nakuletea nyingine hii ni DXF imelipuka huko iliko lipukia. Ifike mahali hizi gari na kuwaka moto zimalize tofauti zao. Ni dualis ya 6 inawaka moto katika nilizowahi kusikia.

Nadhani hizi gari zina shida katika mfumo wake wa umeme, kwamba mfumo hautaki iwekewe kitu chochote ambacho ni after market kuanzia balbu, honi, alarm, mziki, GPS, au modification yoyote itakayo gusa component ya umeme.

Tuendelee kujifunza tabia za hii gari, ila ki ujumla hii siyo gari reliable kwa sasa ya kuweka milioni zako, huyu mwali atakutia hasara. Hapo nimecheki nimeona ina bima Comprehensive, lakini nijuavyo mimi mashirika ya bima ya bongo, dana dana zitakuwa nyingi sana na kusubiri hela hadi uchoke, ama akalipwa kidogo au asilipwe.

Na itafika wakati hata mashirika ya bima watakataa kuzikatia dualis kwa hii changamoto ya kupenda moto kama sigara.
Poleni. Ila kwa nini uweke vifaa zaidi ya vilivyopo ktk gari? Na kama ni lazima, ni vizuri kutumia mafundi wenye uzoefu au dealer wa aina ya gari husika.
 
nilishawahi jiuliza sana zile rubber huwa zina msaada gani?😂😂kumbe ni urembo tu!!!! Basi nilikiwa najua pengine milango inalegea hivyo wanakazia hiyo midude
Na kuna raba fulani wanaweka kwenye milango, ha ha mi hizo mambo ndio mbali mbali kabisa.
 
Si kwamba tunaharibu biashara zenu...ila kuna aina ya urembo mnauleta, unafanya magari ya vijana yanakuwa kama majini...

Yaani kuna hawa vijana wadogo walioajiriwa jeshini, ukiona hizo IST zao na Rumion walivyozijaza maurembo, gari zimekuwa jini..

Hivi kuna siri gani wanajeshi wapya na Rumion?

Au ni maagizo kutoka juu

Yaani kama hajanunua Rumion basi premio/IST

Ili akaweke kale kamkanda,na fog light za blue blue
 
Hivi kuna siri gani wanajeshi wapya na Rumion?

Au ni maagizo kutoka juu

Yaani kama hajanunua Rumion basi premio/IST

Ili akaweke kale kamkanda,na fog light za blue blue
Rumion ni gari nzuri nafikiri kwa toyota gari zake ndogo ndo gari nzuri kuliko zote. Rumion ni ist ama spacio sababu zina engine inayofanana. Ndio gari unaezasafiri nayo mbali kwa gharama nafuu.japo ulaji wake unazidi kidogo sana kwa spacio na ist na hii ni sababu ya umbile lake ambali linapingana na aerodynamics yenyewe haipenyi kwenye upepo bali inapingana nao. Ila utofauti wa ulaji huu ni negligble.
 
Mwaka 2021 kama sijakosea mwezi Machi pikipiki yangu iliwaka moto yote, source ya moto ni kuwa fundi alikuwa anarekebisha compression.

Kuna namna wanafungua pale inakaa plug wanaweka oil chafu halafu wanapiga kiki

Sasa huyu fundi alichonishangaza yeye ile oil chafu anaichanganya na petroli na ndio shida ilianzia hapo, alifungua koki akachukua petroli kidogo ili achanganye na oil...

Kule kwenye koki hakufunga vizuri matone yakawa yanadondoka moja moja.. akachamoa plug na ule waya inakovishwa plug uko pembeni ya block ... Najua unajua nini kilifuata

Basi mtaalamu akamimina ile mixer ya oil+petroli kwenye tundu la plug, akaanza kupiga kiki kumbe ule waya wa plug unatoa cheche, kiki ya kwanza ya pili ya tatu ikakutana na tone la petroli.. Ni hivi ile pikipiki iliwaka moto yote kibaya zaidi nilikua nimejaza mafuta full tank niende mashambani na safari ikakomea hapo hapo.

Ilinichukua week kadhaa kusahau ule moto nikawa kila nikiona moto nakumbuka ulivyoifanya bike yangu, kwa hiyo ni kweli moto wa petroli ni mkali sana na una blaze kubwa maana kuna jamaa walikua wanakuja na mchanga kila wakimwagia moto ndio unazidi.

Dakika kadhaa tu pikipiki iligeuka screpa moto wa sio mchezo ila wa petroli hatari yake sio ndogo acha kabisa.
Mlimalizanaje na fundi mkuu??
 
Huwa nasikia vibaya nikiyaona...au wwngine wanafunga kale kamkanda sehemu ya kuvutia gari..
Wengine wanakaweka karefu mpaka kanaburuza chini pamoja na clip kwenye kila corner ya bumper mbele na nyuma.
 
Hivi kuna siri gani wanajeshi wapya na Rumion?

Au ni maagizo kutoka juu

Yaani kama hajanunua Rumion basi premio/IST

Ili akaweke kale kamkanda,na fog light za blue blue
Wale machalii ni ushamba wa kuigana...
Wengi wao ndiyo wana miaka 2 kazini..

Kazi ni kununua Rumion na kuzipimpu..

Kisha apangishe single self, aweke flat screen kiubwa na mziki mnene...

Akimaliza hapo, kazi iliyobaki ni kula wake za watu...mtaani kwangu ndoa nyingi zimevunjwa na hivi hichalii..
 
Kwa kifupi, achana na kufanya modifications zozote kwenye wiring ya Nissan yoyote...
Haswa haya matakataka yanaitwa Android radio...
Mataa ya rangi rangi ndani mwngine yanawekwa mpaka chini ya siti..
Sheria ya kwanza ya kumiliki NISSAN. Keep it as close to OEM as possible. Maana yake wiring OG, spare OG.

Ila Dualis zina shida ya kiwandani. Firewall yake iko karibu sana na exhaust manifold, zile clip za plastic zikikatika zinailalia exhaust manifold na kwasababu inakuwa ya moto, inawasha. Ndio moshi mweusi huo nahisi.

NB firewall ni ile plastic inayokaa nyuma kwenye bonnet chini ya kioo kuzuia joto la engine kuja kwenye body/ndani
 
Back
Top Bottom