Nissan Dualis: Dxf Nyingine Imewaka Moto

byakunu

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
517
1,145
Ni katika muendelezo ule ule wa Dualis a.k.a sigala na vayolensi za moto, nakuletea nyingine hii ni DXF imelipuka huko iliko lipukia. Ifike mahali hizi gari na kuwaka moto zimalize tofauti zao. Ni dualis ya 6 inawaka moto katika nilizowahi kusikia.

Nadhani hizi gari zina shida katika mfumo wake wa umeme, kwamba mfumo hautaki iwekewe kitu chochote ambacho ni after market kuanzia balbu, honi, alarm, mziki, GPS, au modification yoyote itakayo gusa component ya umeme.

Tuendelee kujifunza tabia za hii gari, ila ki ujumla hii siyo gari reliable kwa sasa ya kuweka milioni zako, huyu mwali atakutia hasara. Hapo nimecheki nimeona ina bima Comprehensive, lakini nijuavyo mimi mashirika ya bima ya bongo, dana dana zitakuwa nyingi sana na kusubiri hela hadi uchoke, ama akalipwa kidogo au asilipwe.

Na itafika wakati hata mashirika ya bima watakataa kuzikatia dualis kwa hii changamoto ya kupenda moto kama sigara.
 
Ni katika muendelezo ule ule wa Dualis a.k.a sigala na vayolensi za moto, nakuletea nyingine hii ni DXF imelipuka huko iliko lipukia. Ifike mahali hizi gari na kuwaka moto zimalize tofauti zao. Ni dualis ya 6 inawaka moto katika nilizo wahi kusikia.

Nadhani hizi gari zina shida katika mfumo wake wa umeme, kwamba mfumo hautaki iwekewe kitu chochote ambacho ni after market kuanzia balbu, honi, alarm, mziki, GPS, au modification yoyote itakayo gusa component ya umeme.

Tuendelee kujifunza tabia za hii gari, ila ki ujumla hii siyo gari reliable kwa sasa ya kuweka milioni zako, huyu mwali atakutia hasara. Hapo nimecheki nimeona ina bima Comprehensive, lakini nijuavyo mimi mashirika ya bima ya bongo, dana dana zitakuwa nyingi sana na kusubiri hela hadi uchoke, ama akalipwa kidogo au asilipwe.

Na itafika wakati hata mashirika ya bima watakataa kuzikatia dualis kwa hii changamoto ya kupenda moto kama sigara.
Ka milioni kumi na kitu kamernda kama sio ishirini na kitu
 
Hayo maeneo nayafananisha na njia ya beach fulani hivi.

Pole sana kwake. Nissan Dualis a.k.a Dasalamu sweetheart a.k.a sigara kali.

Hizo ndinga hazitaki aftermarket modifications zinazolink na mfumo wa umeme. Anytime unalala na viatu!

-Kaveli-
 
Soma hapo juu utapata mawili matatu juu ya hizo nissan dualis
 
Nadhani hizi gari zina shida katika mfumo wake wa umeme, kwamba mfumo hautaki iwekewe kitu chochote ambacho ni after market kuanzia balbu, honi, alarm, mziki, GPS, au modification yoyote itakayo gusa component ya umeme.

Boss shida siyo aftermarkets.

Tafuta gari 10 tofauti tofauti, zilizofungwa Android radio, chomoa radio angalia waya zilivyokatwa na zilivyoungwa. Ni majanga.

Hiyo radio ni mfano tu, ila hivyo ndio baadhi ya mafundi wanaunga aftermarkets kwenye magari ya watu.

Hapan nina voice note ya mtu ambaye amenicall 20:55 usiku wa leo ana mazda Cx5 amotoka kufunga adroid radio, gari inawaka ila ukikanyaga accelerator kimya, inawaka check engine na abs.

I doubt, wahuni wameungia radio waya ya throttle, au wamepigisha shoti fuse ya throttle😂😂😂😂. wao wameshaamsha wamemuacha jamaa anataabika.

Week 3 zilizopita jamaa alifunga taa za booster kwenye mark 2 grande, akiwasha taa wire unaotoka kwenye battery unapata moto unayeyuka taa zina zima, Yaani badala ya kuungua fuse eti unaungua waya(waya za bei rahisi ni chanzo cha moto).

Aftermarkerts siyo shida, shida ni ufungaji, Imagine mtu anachukulia umeme popote ambapo yeye amepima na testa ameona kuna umeme bila kujali ni umeme wa nini.

Me nimefunga/ninafunga GPS trackers kwenye gari nyingi sana including hizo Dualis. Umeme tunachukulia kwenye main suppy yoyote. Waya naunga proper(kwa crimping). Sijawahi pata case ya kuungua wire au fuse ya aftermarkets ninazofunga.
 
Boss shida siyo aftermarkets.

Tafuta gari 10 tofauti tofauti, zilizofungwa Android radio, chomoa radio angalia waya zilivyokatwa na zilivyoungwa. Ni majanga.

Hiyo radio ni mfano tu, ila hivyo ndio baadhi ya mafundi wanaunga aftermarkets kwenye magari ya watu.

Hapan nina voice note ya mtu ambaye amenicall 20:55 usiku wa leo ana mazda Cx5 amotoka kufunga adroid radio, gari inawaka ila ukikanyaga accelerator kimya, inawaka check engine na abs.

I doubt, wahuni wameungia radio waya ya throttle, au wamepigisha shoti fuse ya throttle. wao wameshaamsha wamemuacha jamaa anataabika.

Week 3 zilizopita jamaa alifunga taa za booster kwenye mark 2 grande, akiwasha taa wire unaotoka kwenye battery unapata moto unayeyuka taa zina zima, Yaani badala ya kuungua fuse eti unaungua waya(waya za bei rahisi ni chanzo cha moto).

Aftermarkerts siyo shida, shida ni ufungaji, Imagine mtu anachukulia umeme popote ambapo yeye amepima na testa ameona kuna umeme bila kujali ni umeme wa nini.

Me nimefunga/ninafunga GPS trackers kwenye gari nyingi sana including hizo Dualis. Umeme tunachukulia kwenye main suppy yoyote. Waya naunga proper(kwa crimping). Sijawahi pata case ya kuungua wire au fuse ya aftermarkets ninazofunga.

Asante mkuu kwa madini yenye uzoefu na ushauri mzuri, nakubali unachosema,

Mimi nimewahi fungiwa Gps kwenye Ist, waya wa main power (+ve) fundi alichukulia kwenye boya lile tunapo chomekea OBD Scanner, kaungia kwenye waya unaoenda kwenye control box, ground katafuta anakojua yeye basi gari ikawa inakata moto fyuzi zinaungua,

Kila nikiwasha gari dashboard yote inakua imezima hai display chochote, kuifupi gari ikachanganyikiwa, ndioo kutafuta fundi mwengine aka tafuta positive kwenye waya mwingine gari ikawa sawa.
 
Back
Top Bottom