Nguvu za kijinsia katika tendo la ndoa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
9,034
12,282
Ni jumla ya utimamu wa kimwili, kiasaikolojia, kiakili na kiroho katika kushiriki kikamilifu kwenye tendo ndoa. Concentration ya kimwili, kiakili, kiasaikolojia na kiroho yafaa kua kwenye tendo husika. Kukiwa na setback yeyote miongoni mwa hayo tatizo la nguvu kupungua huanzia hapo.

Na kwahivyo, kutokua timamu mathalalani kimwili labda kwasababu ya magonjwa au maradhi fulani, kunaweza kukadhoofisha utayari wako katika kushiriki kikamilifu kwenye tendo. Unaeweza kujilazimisha na ukakwamia njiani. Na hiyo huwa ni aibu na fedheha kubwa sana kiasaikolojia.

Kutokuwa timamu na mtulivu kiakili mathalani, labda una msongo wa mawazo, madeni makubwa, kesi mahakamani, kuhisi usaliti, stress za umaskini, ukosefu wa ajira nakadhalika, mambo haya kwa uchache yanaweza kudhoofisha usiweze kua na ashiki ya kushiriki tendo kikamilifu na kupelekea aidha ushiriki kwa dakika chache sana na usiweze tena kurudia mshindo mwingne kwa siku hiyo.

Kutokua na utimamu wa wa kiasaikolojia na kiroho, pia kunaweza kuchochea kupotea kwa hamu, uwezo na nguvu za kujamiiana, mathalani kwa kua na hofu ya kutenda dhambi, hofu ya kupata ujauzito kabla ya ndoa, familia na watu wata kuona naje, hofu ya kutokua na nguvu za kijinsia, hofu ya kuparfom chini ya kiwango na kadhlika.

kwa kifupi ni kwamba hakuna asie na nguvu za kijinsia, lakini pia nguvu za kijinsia sio tatizo kwa yeyote. Shida ni kwenye hayo mambo muhimu niliyoyataja kutatiza mtiririko mzuri wa uzalishaji na utoaji wa hizo nguvu za kijinsia 🐒

Kwahiyo, tukiimarisha utimamu wa kimwili, kiasaikolojia, kiakili na kiroho, hususani kabla ya kushiriki tendo, mathalani kwa kula vizuri, kushiriki mazoezi mwili mara kwa mara, kupumzika vizuri na vya kutosha, kunywa vizuri, kuepuka madeni yasiyo yalazima na yanayoleta stress na msongo wa mawazo, kuepuka maugomvi yasio na mbele wala nyuma, kuachana na kuangalia picha na video za ngono, punyeto n.k.

Hii itasaidia kua na nguvu na uwezo wa kutosha, kujiamini na kushiriki kikamilifu na kwa uhakika katika tendo muhimu sana la ndoa, na kufurahia raha na utamu wa tendo lenyewe kwa kushirikiana kwa pamoja bila uvivu, wala kubaniana.

Mi tamu askwambie mtu.
 
kama nguvu ziko sawa yaani za kiume hata kama una stress au unaumwa ukipata mzigo unagonga vizuri na kanasimama safi
tafuteni tiba na siyo visingizio
una miaka wa ujana halafu unasingizia stress- aaaah weee si kweli
 
kama nguvu ziko sawa yaani za kiume hata kama una stress au unaumwa ukipata mzigo unagonga vizuri na kanasimama safi
tafuteni tiba na siyo visingizio
una miaka wa ujana halafu unasingizia stress- aaaah weee si kweli
binafsi sidhani kama tatizo ni nguvu za kijinsia, bali ni kwa kiasi gani muhusika ameathirika na moja kati ya mambo niliyoyataja au yote kwa pamoja 🐒
 
Yaani una stress za maisha halafu mashine nayo inagoma kusimama dede au tako moja wareno hao stress juu ya stress!
hiyo maana yake, physically, saicolojicaly and mentally the man is done badly. Lazima kwanza aende gereji na achukue likizo ya lazima utulivu ili kujiformat na kujimodifie, other wise tutamkosa kabisa kijana 🐒
 
Back
Top Bottom