Mke anamnyima mumewe tendo la ndoa, nini kifanyike?

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,657
4,552
Habarini wajukuu wema na wabaya. Nimeletewa mashitaka na huyu kijana mwenye ndoa ya miaka mitano sasa.

Anasema alitahadharishwa na watu kuwa unaoa dada wa Kilimanjaro, jiandae kwenda kunyimwa tendo la ndoa, hakuwasikiliza. Sasa yamemfika. Anadai kuwa wanaweza kukaa hata miezi sita bila kushiriki tendo hilo. Na jamaa anapohitaji anaweza kuomba hata wiki ndio apewe tena kwa masimango, mara huwezi mara umezeeka nk..

Amejaribu kuzungumza na mkewe bila mafanikio. Mwanamke anadai hajiskii, sasa ananiomba ushauri afanyeje ili ndoa yake idumu na apate tendo la ndoa kama kawaida?
 
Khaa!

Hivi huwaga nashangaa unawezaje kufanya tendo na mtu asiyekupenda.

Mtu akishakunyima mara mbili mfululizo bila sababu, si maana yake unapiga chini? Maana ana roho ya uuaji aisee!

Kusini huku hakunaga kunyimwa, kwanza we ndo unalazimishwa na binti wa kimwera umfumue. Utalia lia ooh umechoka, anazira!
 
Amejaribu kuzungumza na mkewe bila mafanikio.. Mwanamke anadai hajiskii.. Sasa ananiomba ushauri afanyeje ili ndoa yake idumu na apate tendo la ndoa kama kawaida..??
Sijaona ulicho mshauri huyo mjukuu wako.

Au wewe ndiye uliyenyimwa halafu ukaja hapa ukijifanya babu ili tukushauri?


Kuwa wazi kama ndo wewe umenyimwa papuchi tukushauri.
 
Waambie pendaneni, msinyimane 🐒

Chanzo kikubwa cha mchepuko na nyumba ndogo ni kunyimana 🐒

Lakini, miongoni mwa sababu za kukaribisha ndani ya ndoa, maradhi ya fedheha kama vile UTI sugu, gono, kaswende na hata UKIMWI ni kunyimana 🐒

Lakini, pia chanzo cha yatima na watoto wa mitaani, single mothers na single fathers walio hai na afya zao kabisa, ni kunyimana 🐒

Ni vizuri kuketi chini kwa upendo na upole, kubainisha kasoro, tofauti na ukweli wa hali hiyo na hatimaye kusawazishana na kusameheana 🐒

Mpendane, msichokozane! Amani ya bwana iwe ndani yenu. Tendo ni Baraka yake Mungu, amewakirimia katika kushirikiana nae katika kazi ya uumbaji.

Haifai kuchoka, kuwa mvivu au kukataa bila sababu yoyote ya msingi kushiriki kazi ya uumbaji. Kumbuka Mungu yuko katikati yenu katika kazi hiyo, peaneni kwa upendo bila hiyana, msinyimane tafadhali 🐒
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom