KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,592
- 4,624
Leo nimesikia kitu kilichonifurahisha sana kutoka wa waziri wa fedha wakati akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/2024 nalo ni kuja na mpango wa kuanza kukusanya Kodi kwenye matangazo ya biashara mitandaoni.
Sijajua kwa upande wa Serikali ukiachana na kukusanya Kodi kwenye matangazo hayo ni upi lakini kwangu mimi ni Jambo nililokuwa natamani kwa muda mrefu lije kwa sababu nina kisa cha mtu aliyenusurika kutapeliwa simu kupitia tangazo aliloliona mtandaoni.
Pia soma Serikali kuanzisha mfumo wa kidigitali kukusanya kodi kwenye matangazo ya mitandao ya kijamii
Kisa chenyewe ni hiki : Kuna jamaa alikuwa anataka kununua simu.Akaona aingie kwenye mtandao wa Facebook ajaribu kutafuta wauzaji wa simu. Katika kutafuta tafuta akafanikiwa kupata muuzaji ambaye kwa aina ya simu aliyokuwa anahitaji alikuwa anauza kwa Bei nafuu. Muuzaji akamwambia tutakutumia mzigo ukilipia, jamaa akasema nataka nije mlipo nifanye malipo hapo na nikague mzigo. Wakakubaliana kwenda kuona mzigo ili anunue lakini alichoenda kukikuta kule ni kitu tofauti kabisa na kilichotangazwa, mzigo ulitangazwa 'new' lakini akaoneshwa 'used' na umechoka mbaya. Kuwauliza juu ya Jambo hilo walikuwa wanajichekesha tu.
Huo ni mfano mdogo wa matangazo yasiyojali thamani ya Bei, ubora na huduma yanavyovunja Imani ya watanzania kwa matumizi ya teknolojia katika suala zima la digital marketing
Hebu tufikirie mbali zaidi kwa huyu jamaa Kama angekubali kufanyiwa 'delivery' halafu analetewa kitu used tena kimechoka vibaya maumivu ambayo angesikia ,naamini ni makali sana.
Kwa wanaoagiza vitu China kupitia Alibaba au AliExpress watakuwa ni mashahidi wa ubora wa huduma na bidhaa na Kama kuna kasoro basi tunaweza kusema ni digital marketing. Leo hii ni rahisi kuamini ubora wa bidhaa kutoka China ambapo ni mbali sana kuliko kuamini ubora wa bidhaa kutoka Kariakoo. Kwa nini?
Kwa sababu 'digital marketing' ina mapungufu mengi sana kwenye nchi yetu na hii inatokana na udhibiti mdogo uliopo hivyo serikali kuja na mpango kwenye Jambo hili naliunga mkono asilimia zote. Kwa sababu:
Wafanyabiashara wa mikoani wengine wanaona Kariakoo ni Kama Guangzhou yao na wanapoona tangazo la biashara la mtu wa Kariakoo anafurahi kama wengine wanapoona matangazo Alibaba na kwingine hivyo Jambo hili litawasaidia kupata bidhaa bora.
Uwekezaji mpya wa bandari utakaofanywa na DP WORLD utasaidia kulikuza sana eneo la Kariakoo na kufanya Kariakoo kuwa kitovu cha biashara Afrika mashariki na Kati na biashara zikawa zinafanyika online kama zinavyofanyika sasa kutoka China. Matangazo ya hovyo ya biashara yatapunguza imani katika kuelekea huko.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni hakika kwenye Jambo hilo Rais Samia na Waziri Nchembe wapewe maua yao na mimi nawapa yakiwa bado mabichi kabisa.