- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Mti wa matunda ukiwa unadondosha maua na matunda mapema, ukiupigilia msumari kwenye shina haudondoshi
Uvumi huo ukweli wake ukoje?
Uvumi huo ukweli wake ukoje?
- Tunachokijua
- Kuna wakati miti ya matunda kama miembe, mipapai, miparachichi na mingine, hudondosha maua na matunda wakati yakiwa bado machanga, kitendo ambacho ni hasara kwa wakulima.
Baadhi ya miti hiyo huanza kudondosha matunda muda mfupi baada ya kuanza kuzaa na hii hutokea baada ya maua kujitenga na tunda au maua kudondoka kabla hayaanza kuweka tunda.
Hata hivyo baadhi wa watu wamekuwa wakishauri kuwa hali hiyo ikiupata mti au miti ya matunda, miti hiyo ipigiliwe msumari kwenye shina na hivyo itaufanya mti kughairi zoezi la kupukutisha maua au kudondosha matunda na kuyaaacha matunda yakomae au maua yaweke tunda na kisha tunda kukomaa.
Je, ni kweli Mti wa Matunda ukiwa unadondosha maua mapema au matunda mapema, ukiupigilia msumari kwenye shina unaacha kudondosha?
Baada ya mdau kuuliza swali hili, JamiiCheck ilimtafuta na kuzungumza na Eliud M. Letungaa, Mtaalam wa Kilimo na Afya ya Mifugo na Kilimo cha Kiikolojia (Agroecology) ambaye alieleza kuwa:
Mti wa matunda ukiwa unadondosha maua mapema, ukiupigilia msumari kwenye shina unaacha kudondosha, hii ni nadharia yenye kaukweli ndani yake.
Ukweli wake ni kuwa inapotokea hali hiyo (kupigiliwa msumari) Mti unajichukulia kama unataka kuanza kufa, hivyo unajihami kwa kupunguza uzao kama namna ya kujikinga.
Kwa kupiga msumari unaupa mti tahadhari na unahisi unakaribia kufa, hivyo unaanza kufyonza zaidi virutubisho ardhini na virutubisho zinavyohitajika, hapo unaacha kudondosha matunda, badala ya kuzaa matunda mengi unatoa maua machache kwa sababu unaona bora ujilinde kwanza.
Unaweza piga msumari kwenye miti ya Parachichi, miembe n.k lakini haishauriwi kutumia msumari wa inchi 6 kwa diameter 12 kwa kuwa unaweza kufika mpaka katikati ya mti husika ukasababisha mmea husika kufa.
Hivyo, Kutokana na maelezo ya mtaalamu wa kilimo kuithibitishia JamiiCheck kuwa ni kweli kupigiliwa msumari kwenye shina kwa mti unaodondosha maua au matunda huufanya uache, hivyo tumejiridhisha kuwa suala hilo ni kweli.