Mkuu wa Shule na Mzazi wa Mwanafunzi walinitengenezea zengwe hadi nikafukuzwa kazi

Asante k
Ingependeza tukapata maelezo kutoka upande wa pili.

Kama ni kweli unachokisema basi ile kauli ya "Tenda wema nenda zako" inafanya kazi.

Nilichobaini kuna suala la "MAPENZI" kama sababu kuu.
Inawezekana uliingilia masilahi ya boss wako kwenye mapenzi.

Elewa jambo moja wanawake kiasili ni wasaliti na wanaweza kukuharibia muda wowote na mahali popote.

Tafuta huyo mwanamke mpange vizuri ila sidhani kama atakuelewa na akijua umeshafukuzwa na kazi ndiyo basi tena utaona kila aina ya rangi.

Hao watu 2 ie mama na mtoto ndiyo pekee wataweza kukuokoa na jinamizi hili wakili kabisa walirrubuniwa na mkuu kwa masilahi yake. Je itawezekana?

Wito: usimwamini mwanamke kwa chochote unachokifanya japo hata wanaume wanatabia za kike.
wa ushauri, nitaufanyia kazi mkuu
 
Nimekuelewa vizuri, nchi kubwa sana hii, nilikoanzia kazi ni kijijini sana hakuna zaidi na ni halmashauri hii hii baadae nakahama.
Pia sijaficha chochote kosa langu ni hilo moja tu nililotuhumiwa nalo.

Kuna kurasa amezificha. Ukiona mtu hadi amefikia hate ya kukufukuzisha kazi aisee kuna kitu kikubwa sana kati yetu. Otherwise wangemuamishia vijijini ndani uko kama adhabu.

Okay, ngoja tuone wengine watamshaurije. Ila sio mwisho wa maisha. Mtaani kupo.
 

Attachments

  • Screenshot_20240317-073151~2.png
    Screenshot_20240317-073151~2.png
    55.1 KB · Views: 6
I bet kuna taarifa umezificha,hujaelezea. Huwezi kufukuzwa kazi kirahisi hivyo..kwa story kama hyo
 
Hakuna kesi ya kufukuzwa kazi kwa ushahidi wa kufikirika na mwepesi kama huo hata kama ni kweli ulimtongoza huyo binti. Labda kama ungekuwa umemtafuna kweli, na ukakamatwa na vielelezo/vidhibiti vya kutosha! Mfano ujumbe mfupi kwenye simu, umekutwa naye ndani ya chumba chako na huyo mwanafunzi, umempa ujauzito, nk.

Wewe endelea kupigania haki yako. Ikiwezekana nenda kwa DAS, RAS, nk kutoa malalamiko yako. Na baada ya hapo fanya utaratibu wa kuomba kuhamia shule iliyo kwenye Kata/Tarafa nyingine ndani ya hiyo Halmashauri yako ili kuepukana na hizo changamoto.
Shukran sana kwa mawazo mema
 
Ukweli unajua mwenyewe ila naamini haijasema kweli toka kwenye moyo wako.

Ukisema kweli nitakusaidia.
Kazi ni kwako kusema kweli au kuendelea kuongopa huku ukiwa jobless.
Msaada wa watu ni kitu pekee ninachokihitaji kwa sasa, na natambua ni lazima niwe muwazi. Niliyoyasema yote ni sahihi kiongozi hivyo karibu kwa msaada tafadhari.
 
jiandae kutafuta kingine cha kufanya kupata riziki, watu waliodhamiria kukuweka sehemu mbaya hawatashindwa kuendelea kuhakikisha unakuwa pabaya zaidi na zaidi.

ubaya hurudi kwa ubaya na wakati mwingine ubaya unabaki kimya bila marudio ya ubaya wala wema, unaweza kuwatarajia hao waliokufanyia hayo wakutane na malipo ya ubaya wao lakini ikawa kinyume chake, badala yake wewe ndie unae umia.
maoni yangu achana nao, tafuta kingine cha kufanya hauta aibika .
Umesema vyema kabisa. Hiyoo team yote haitotaka kuonekana hawatoshi, lazima watatak kuthibitsha zaid, udhalimu wao.
Maana kwa System ya sasa, kila mtu hapo anamjua mtue, unaweza kwenda kufatilia rufaa, unaye muandikia rufaa ana ushikaji na hao , unakuta email zako au barua zako zina somwa na unao walalamikia .

Kama una connection fight, zama Wizarani kajiripue, ila kama ndio wale wanyonge, utashangaa kesi inachezeshwa ktk jinai huko, so mahakama za kiraia zitahusishwa..

By the way, kumbuka kuna watu wana ubaya mwingi sana, mtu anaweza kuongea uongo ,akijua matokeo yake ni kukupoteza na anaongea uso mkavu na kiapo juu.
 
Hizi drama zoote zimeanza kisa ulikuwa unajaribu kum satsify mwanamke kwa namna moja au nyingine, na wala sio kwa ubaya nia ilikuwa njema kabisa. Mwanangu punguza shobo na hawa wanawake watakuja kukukost big time, your career is at an edge of a cliff because of a woman, hili likiisha salama redefine the way you deal/treat women sikatai ni mama zetu ila mwanamke pekee anaeweza kukuelewa na kukuthamini mpaka mwisho ni mama yako mzazi tu. Fear women.
 
Kama KunA kitu una pindisha ebu nyoosha tujue jinsi ya kukusaidia. Nawajua walimu walio wapa wanafundi mimba. Na bado Wana dunda kwenye ajira zao...Yani wewe kuhusiwa tu uwe chanzo Cha kufukuzwa tena bila uthibitisho😭😭😭😭

Nyoosha maelezo ndugu yangu...jf ni jukwaa kubwa...!​
 
Nimewka wazi kila kitu, karibu kwa ushaur
Inaonesha wewe mwl ulikuwa karibu na huyo mwanafunzi, kuna shida mahali haiwezekani kila kiongozi awe against wewe

Umesema vyema kabisa. Hiyoo team yote haitotaka kuonekana hawatoshi, lazima watatak kuthibitsha zaid, udhalimu wao.
Maana kwa System ya sasa, kila mtu hapo anamjua mtue, unaweza kwenda kufatilia rufaa, unaye muandikia rufaa ana ushikaji na hao , unakuta email zako au barua zako zina somwa na unao walalamikia .

Kama una connection fight, zama Wizarani kajiripue, ila kama ndio wale wanyonge, utashangaa kesi inachezeshwa ktk jinai huko, so mahakama za kiraia zitahusishwa..

By the way, kumbuka kuna watu wana ubaya mwingi sana, mtu anaweza kuongea uongo ,akijua matokeo yake ni kukupoteza na anaongea uso mkavu na kiapo juu.
shukrani sana kwa maelezo yanayoeleweka mkuu.
 
Nimenyoosha kwa kiwango changu cha juu kabisa kiongozi
Kama KunA kitu una pindisha ebu nyoosha tujue jinsi ya kukusaidia. Nawajua walimu walio wapa wanafundi mimba. Na bado Wana dunda kwenye ajira zao...Yani wewe kuhusiwa tu uwe chanzo Cha kufukuzwa tena bila uthibitisho😭😭😭😭

Nyoosha maelezo ndugu yangu...jf ni jukwaa kubwa...!​
 
Mwalimu Ni mwalimu tu

Just imagine mwalimu anashindwa kuandika kwa Aya
Hiko ni kitu kidogo sana mkuu cha msingi umepata ujumbe. Unadhani hajui kuwa ilipaswa apangilie aya? Unajua alikuwa katika hali gani kimawazi wakati anaandika huu ujumbe? Hakuna Jambo linaloleta frustrations kubwa kama kuzuiliwa kukatiwa njia inayokupatia ridhiki.
Tujifunze kuvaa uhusika wa jambo kabla ya kutoa ushauri
 
Naamini jambo langu lilibadirika baada ya mkuu kujua kuwa jambo lilikuwa linaelekea kwa Katibu tawala mkoa au Baraza la mitihani, lazima alihisi hatakuwa salama kwa uzembe aloufanya. Naamini alinifanyia hivyo kuniziba kauli. Mzazi hakuwa na nguvu kutokana na uelewa mdogo ndo maana mwanae alikosa haki yake ya msingi
Pole. Mwalimu Mkuu angeweza kukuita tu mkazungumza kuwa unachotaka kufanya kitahatarisha ajira yake halafu kwa pamoja mngekuja na hitimisho, hapakupaswa kuwa na vita.

Ila bado hilo la mzazi kushirikiana na mwalimu ambaye ndiye mbaya wake kukusingizia unatembea na mwanae bado halijakaa sawa, aliahidiwa nini? Anyway kila la heri, haki yako ipatikane.
 
Tsc wilaya hawana welding wa kuamua kesi za walimu wengi wana mihemko na kati ya jambo la hovyo ambalo serikali imelifanya ni kuwapa uwezo Tsc wilaya kufukuza kazi walimu, walimu wengi wataumia kupitia huo mfumo.

Hapo mwamba ulichotakiwa kufanya kabla hujakata rufaa ulipaswa uje humu kuomba ushauri huu au kukutana na mwanasheria au expert wa hiyo field ili akusaidie.

Pengine muda huu unaposubiri majibu ya rufaa yako kuna vitu umeshajichanganya wkt wa kujibu rufaa hiyo hivyo ni rahisi tena kuliwa kichwa ktk ngazi ya juu ya rufaa yako simply because pengine ulijibu rufaa hiyo kwa mihemko au jazba kwa vile urihisi umeonewa.

Cha kukushauri zaidi kama utaweza nitafute box, tuma na utetezi wako tuone umejibu nn kulingana na ulivyotuhumiwa ili tuone kama utaweza kujinasua kwenye huo msala unless unaweza kuwa jobless hvhv unajiona.
 
Back
Top Bottom