Mkuu wa Shule na Mzazi wa Mwanafunzi walinitengenezea zengwe hadi nikafukuzwa kazi

Duh pole sana...

Ndo maana huwa napenda kuwa peke yangu muda wote sitak mazoea na mtu.
 
Unapofukuzwa kazi na tsc unapaswa kukata rufaa mamlaka ya juu ambayo ni kwa waziri wa Tamisemi .Waziri akishindwa unakata rufaa kwa Raisi wa nchi.Ila huko tsc makao maku ulikokata rufaa hawatakusaidia kitu mkuu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Unapofukuzwa kazi na tsc unapaswa kukata rufaa mamlaka ya juu ambayo ni kwa waziri wa Tamisemi .Waziri akishindwa unakata rufaa kwa Raisi wa nchi.Ila huko tsc makao maku ulikokata rufaa hawatakusaidia kitu mkuu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
asante mkuu, ila maelezo ya barua ya maamuzi mamlaka ya nidhamu baada ya TSC Wilaya ni TSC Makao makuu then kwa Raisi.
 
Naamini na wewe una matatizo ila umeamua kuyaweka matatizo ya mkuu tu hapa. Inaonekana ni mtu unayependa ligi na boss wako, mjuaji flan. Maisha ya aina hiyo yanataka umakini sana Kwan ukiteleza kidogo hutapata Mtu wa kukusaidia. Jifunze kufanya mambo yako, taasisi yoyote utakoyoenda utakuta Kuna mambo ya watu, vitu vya Watu na Watu wa Watu, Jiepushe navyo mkuu , si unaona Hata uliolenga kumsaidia asigongwe Hana Msaada kwenye shida zako Tena amekua sehemu ya kukukandamiza zaid, ungeacha akagongwa ungepungukiwa Nini?

Unapopata shida kubwa, hasa kesi ya kiutumishi pambana uisolve kabla haijaenda hatua ya juu zaid, kadri unavyochelewa Ndio inavyozidi kupiga hatua, namna inavyopiga hatua Ndio inazidi ugumu wa kutatua. Hiyo kesi ilikua inaishia shuleni tu ila ujuaji wako Ndio umekufikisha hapo.

Ushauri nenda CWT watakusaidia, kama ni kuongea na mwajiri Au kupeleka kesi mahakamani na Kama unaweza kamuone DED uongee Naye ana Kwa ana. Hapo hujafukuzwa Bado, umepigwa tu DP. Unapoweza kujishusha Ili kumaliza shida, jishushe ila sio Kwa kubaki kesi kimaandishi,Naamini Kwa uwezo wa Mungu yataisha.
We jamaa una busara sana aisee nimekuelewa hapo kuwa Kila sehemu ya kazi Kuna MAMBO YA WATU,VITU VYA WATU,WATU WA WATU mi kazini kwangu huwa tunadeal na shida za watu unaona Kuna mwingine hastahili kabisa ila unaambiwe umsaidie hivyohivyo na yeye apitishwe mi huwa sibishani Nampitisha tu.

Kuna siku tulikaa kikao nikashauri muongozo tuliotumiwa na ofisi ya waziri mkuu tuuzingatie weeh! Mkurugenzi aliwaka akasema mi sipo kwenye ile nafasi yake ndio maana ntajifanya mjuaji kama nataka niende akaniachie ofisi yake nilikuwa mkimya kama nimemwagiwa maji.

Tangu ile siku mi kwenye kikao kazi yangu kujifanya naandikaandika tu kwenye laptop na kupiga makofi na kunyoosha mkono wakiuliza anayeunga mkono.
Kikubwa nalipwa mshahara na posho zangu zile za lazima(hata baadhi ya posho zisizo za lazima sifuatilii sanaaa).
Kazi yenyewe nimeipata kwa shida hii GPA ya chini nkiikosa ntateseka sana
 
Back
Top Bottom