Microwave oven vs Airfryer ipi Bora kwa kuchoma nyama, kukaanga chips na kupasha chakula

Kwa io Toyota na utitiri wa magari haifai? Au ni kwa electronics?
Sasa umeshasema magari hiyo ni bidhaa ya aina moja, electronics ni industry pana sana ambayo ndani yake ina bidhaa za aina nyingi, mfano feni na jiko ni bidhaa za aina mbili tofauti kabisa
 
Mkuu coffee maker sio electric kettle...jinsi inafanya kazi tofauti na namna unavyodhani
Screenshot_20240219_212020.jpg

Hapo kwenye cook unaona.
 
Nunua Kenwood original sio yale mafamba ya kichina...

Ukishaona kampuni moja inatengeneza utitiri wa vitu sijui redio, speaker, feni, TV, blender, friji, oven n.k, hiyo si kampuni ya kununua vitu vyake...ndio hao kina Aborder, Mo electronics, Ailyons n.k
Unakuta mtu kajenga nyumba nzuri tu, ingia hapo sebuleni kwake sasa 😂😂 tv ukutani aboder,sijui buffer aboder, king'amuzi continental alooh
 
Unakuta mtu kajenga nyumba nzuri tu, ingia hapo sebuleni kwake sasa 😂😂 tv ukutani aboder,sijui buffer aboder, king'amuzi continental alooh

Wengi hawana uelewa mkuu, huku wengine ikiwa ni masuala ya bajeti, wengine wanahofu ya kuwanunulia wezi, na wengine mambo ya electronics sio vipaumbele, wengine wana hofu na watoto waharibifu...
 
Nunua Kenwood original sio yale mafamba ya kichina...

Ukishaona kampuni moja inatengeneza utitiri wa vitu sijui redio, speaker, feni, TV, blender, friji, oven n.k, hiyo si kampuni ya kununua vitu vyake...ndio hao kina Aborder, Mo electronics, Ailyons n.k
Kwa hiyo vitu vya Samsung na LG sio vya kuviamini?

Amandla...
 
Kuchoma nyama - Airfryer
Kuchoma kuku mzima - Airfryer
Kuoka chips (sio kukaanga) - Airfryer
Kupasha chakula - Microwave oven na hata Airfryer (ingawaje utakuwa unaichosha)

Kifaa cha kufanya kazi hizo zote unataka, nunua jiko lolote iwe la gesi, umeme, mkaa n.k...
Daddy…

Nimependa hitimisho lako

By the way i miss you!
 
Back
Top Bottom