SoC01 Ulaji unaofaa na mitindo bora ya maisha katika kukabiliana na magonjwa sugu yasiyoambukiza

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 13, 2021
6
6
ULAJI UNAOFAA ni kula chakula chenye mchanganyilo wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi matano ya chakula.Chakula hicho kinatakiwa kiwe cha kutosha kukidhi mahitaji ya mwili.

Ulaji unaofaa unatakiwa kuzingatia mahitaji ya mwili kutokana na jinsia,umri,kazi na shughuli zinazofanywa pamoja na hali ya kifiziolojia(kunyonyesha na ujauzito).Mambo ya kuzingatia katika ulaji unaofaa ni:

Kula angalau Milo mitatu kwa siku
Kunywa maji safi na yakutosha kila siku

Kula matunda na mboga mboga kwa wingi kila siku
Kula vyakula vyenye makapi mlo kwa wingi (unga wa dona,vyakula vya jamii ya kunde)
Kuepuka kutumia mafuta ,sukari,na chumvi kwa wingi

Mtindo bora wa maisha ni ule unaozingatia ulaji unaofaa ,kufanya mazoezi ya mwili,kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku na msongo wa mawazo.

**Je ulishaji wa mtoto una uhusiano gani na magonjwa sugu yasiyoambukizwa

Tafiti zimeonyesha kuwa uhusiano kati ya ulishaji wa mtoto na ueezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyoambukiza utotoni,katika ujana na hata anapokuwa mtu mzima.

Tafiti zimeonyesha kuwa;
Unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee chini ya miezi sita huwakinga watoto dhidi ya kuwa na uzito uliozidi na unene uliokithiri wanapokua wadogo na hapo badae .
Ulishaji wa vyakula vya nyongeza vyenye nishati lishe kwa wingi na maziwa mbadala unahusishwa na mtoto kuwa na hatari ya kupata unene ,saratani na shinikizo kubwa la damu ukubwani.


#storyofchange

Ulaji unaofaa ni pamoja na kula chakula mchanganyiko ,cha kutosha na chenye virutubishi vyote kwa uwiaono unaotakiwa.kula matunda angalau Mara mbili kwa siku na kula mboga mboga kwa wingi. Kunywa maji Lita mbiki au zaidi kwa siku.

Ulaji unaofaa ni lazima uzingatie matumizi ya mafuta kwa kiasi kidogo. Mafuta ya nyamama sio mazuri sana kwani yanahusishwa na magonjwa ya moyo, badala yake inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokananyo na mimea.
Matumizi ya sukari na chumvi yawe kiasi.Pia kwa watu wanaokunywa pombe wasinhywe pombe kupita kiasi.

**KULA CHAKULA MCHANGANYIKO
Chakula mchanganyiko hukuwezesha kupata virutubishi vyote vinavyohitajika mwilini kwa mfano vyakula vya wanga vinasaidia kuupa mwili nguvu na moyo,utomwili husaidia kujenga mwili,vitamin na madini hulinda mwili dhidi ya magonjwa. Kila siku jitahidi kula vyakula kutoka katika makundi yafuatayo;
Vyakula vya asili ya nafaka,ndizi za kupika ,viazi na mizizi
Vyakula vya jamii ya kunde na asili ya wanyama
Mboga mboga
Matunda
Sukari, asali, mafuta na mboga zenye mafuta


**KUTOKULA MAFUTA MENGI
Mafuta mengi mwilini hasa yale yenye asili ya wanyama yanaweza kusanabisha ongezeko la magonjwa ya moyo na shinikizo kubwa la damu ,hivyo inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea.
Jinsi ya kupunguza mafuta;
Tumia mafuta kwa kiasi kidogo wakati wa kupika
Epuka kula vyakula vilivyokaangwa kwa mafuta badala yake chemsha ,oka au choma.
Punguza mafuta kwenye nyama iliyonona na ikibidi ondoa ngozi ya kuku kabla ya kupika
Chagua nyama au samaki wasio na mafuta mengi

**KULA MATUNDA NA MBOGA MBOGA KWA WINGI
Vyakula hivi huupatia mwili kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama vile baadhi ya magonjwa ya moyo,saratani na kisukari.
Pika mboga mboga kwa muda mfupi ili kupunguza upotevu wa vitamin na madini
Tumia maji kidogo wakati wa kupika mboga mboga .Maji yanayopikia mboga mboga yaendelee kutumika sio kumwaga
Kula matunda si chini ya mara mbili kwa siku

**VYAKULA VYENYE NYUZINYUZI (FIBRE)
Vyakula vyenye nyuzinyuzi fibre husaidia katika usagaji wa chakula tumboni na pia huweza kupunguza baadhi ya saratani, magonjwa ya moyo na kisukari.
Ili kuongeza fibre:
Kula saladi na matunda mara kwa mara
Kula tunda zima badala ya juisi
Tumia unga usiokobolewa dona ,attack n.k
Kula vyakula vya jamii ya kunde mara kwa mara kwani vina nyuzinyuzi kwa wingi.

**PUNGUZA CHUMVI
Tumia chumvi kidogo wakati wa kupika
Epuka vyakula vyenye chumvi nyingi kama vile bisi,crisps nk
Epuka uongezaji wa chumvi kwenye vyakula kama vile kwenye mihogo ya kuchoma ,maembe na chips na badala yake unaweza kutumia viungo kama ndimu na pilipili kuongeza ladha.

**PUNGUZA SUKARI
Sukari huongeza nishati mwilini hivyo huchangia kuongezeka kwa uzito. Matumizi ya sukari huzalisha bacteria kinywani ambao husababisha karisi(meno kutoboka).
Hivyo inashauriwaKunywa vinywaji ambavyo havina sukari kama vile madafu na juisi ya rozela badala ya soda zenye sukari
Punguza kula vyakula vyenye sukari nyingi kama vile keki,pipi,chocolate nk
Punguza matumizi ya vyakula vilivyoongezwa sukari.

**KUNYWA MAJI KWA WINGI
Inashauriwa kunywa angalau glasi 8 za maji Lita moja na nusu au vimiminika vingine kwa siku.Maji Husain mwili kufanya kazi vizuri

#story of change
 
Nina ongeza tu vyakula vyenye fibre vinasaidia utendaji kazi wa utumbo mkubwa pia vinapunguza uwezekano wa saratani ya utumbo mkubwa ( colorectal cancer).
 
Back
Top Bottom