Shida ya kushika mimba na jinsi unavyoweza kutatua tatizo hilo kwa kutumia lishe

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,172
20,641


1. Tunaendelea kudodosa yaliyomo kwenye kitachu Eating to Conceive by Lisa Olson.
2. Kazi yangu ni kufanya tafiti na kuwasilisha majibu kwa lugha tunayoishi nayo kila siku. Lengo tuelewe, tusikariri! Sitakagi mambo mengi. Tuendelee.

Kanuni ya Pili: Kula Complex Carbohydrate na nafaka kwa wingi!

1. Lisa anasema siku hizi tunaambiwa tusile vyakula vya kobohadreti na nafaka kwa sababu vinaongeza uzito na kusababisha sukari mwilini.
2. Anasema ni kweli lakini usipokula vyakula hivyo hutopata nguvu kwa hiyo hutakiwi kuacha, isipokuwa unatakiwa kula vyakula sahihi
3. Vyakula sahihi ndo complex kabohaidrate na siyo complex kabohaidreti.
4. Simple kabohaidrate ni hatari na hupatikana kwenye unga wa mahindi, ngano, sukari yenyewe, soda etc
5. Complex kabohadreti ndiyo sahihi na inapatikana kwenye mbegu kama mtama, ulezi, maharage, mchele mwitu (brown rice) mbegu za mchicha, quinoa, mboga za majani, matunda fresh nk.
6. Hii ni ile orodha ya mbadala wa ugali, wali na sukari tuliyoiona kwa Dkt. Sebi. Usikoboe.
7. Kwa uelewa zaidi, tembelea mitandaoni na tafuta orodha ya vyakula vyenye complex carbohydrate ule sana ushike mimba. Hapo vipi?
8. Au nenda kwa wataalamu waulize hivyo vyakula wakutajia uzuri siku hizi tuna wataalam kila kona ya nchi, mpaka vijiji wapo, wanaitwa Maafisa Lishe. Hawa ni watu wa maana sana.

Kanuni ya Tatu: Kula Mafuta Sahihi

1. Kuna watu wameacha kula mafuta kwa kuogopa matatizo ya kiafya. Wanakula chukuchuku.
2. Lisa anasema hii ni hatari sana maana mwili unahitaji mafuta.
3. Kumbe solution siyo kuacha kula mafuta badala yake unatakiwa kula mafuta sahihi.
4. Lisa anasema mafuta yameonekana ni hatari kwa sabubu hatuli mafuta sahihi.
5. Yaani kuna watu wanaamini mapishi ni mafuta mengi. Kila kitu kimejaa mafuta. Yaani ukipewa chakula unasisimuka.
6. Anasema unapopata mafuta sahihi basi unasaidia homoni kukaa freshi na viungo vya uzazi kufanya kazi yake ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora kwa viumbe bora.
7. Lisa anataja aina za mafuta, Kiswahili chake sijakipata, ila soma uelewe.

Saturated fats

1. Haya ni mafuta yanayopatikana kwenye wanyama, ukipata zako kuku wa kienyeji safi kabisa unaweza kumla hata bila kuongeza mafuta, yale mafuta yake yale ni safi sana kwa viungo vya uzazi.
2. Kamata kuku wako wa kienyeji, chinja, nyonyoa, pika gonga mpaka mifupa😄.
3. Hata ukila kuku mzima haina neno.Simfuko wako bhana? Maana bei ya kuku wa kienyeji imesimama.
4. Wanyama wote wanaofugwa bila kuchomwa chomwa sindano na kulishwa vidonge kama binadamu hawafai sana katika safari yako ya kutafuta mtoto.

Trans fat*

1. Lisa anasema haya ni mafuta kutoka viwandani, ni hatari sana kwa mtu anayetafuta ujauzito, orodha ya mafuta haya ni ndefu, tunaijua, achana nayo.
2. Haya mafuta yana vitu vingi ndani yake, humo kuna madawa yanawekwa ili mafuta yakae kwa muda mrefu bila kuharibika, yanaweza kukaa hata miaka 10.
3. Hiyo dawa haiwezi kukuacha salama.
4. Haya mafuta utayakuta kwenye chips, mandazi, vitumbua na vyakula kibao vya supermarket, kumbe hata hivyo vyakula kwa mtu anayetafuta ujauzito anatakiwa kauchana navyo anasema Lisa.

Unsaturated fats

1. Haya ni mafuta ya mimea. Yanafaa sana kwa viungo vya uzazi, kula sana uwezavyo.
2. Ni mafuta ya alizeti, mafuta ya olive, mafuta ya parachichi, mafuta ya soya, mafuta ya karanga nk.
3. Gonga sana hayo. Wakati mwingine yanatest mbaya lakini hiyo isikupe shida.
4. Mimi wife alikuwa hapendi mafuta ya alizeti kwamba yana harufu mbaya, tukawa tunagonga korie tu kumbe hatari. Kumbe ni ufundi wa kupika.
5. Siku hizi sisi ni alizeti kwenda mbela au karanga kwa lugha ya mama yangu tunaitwa kitwiro. Ni safi sana.

Essential Fatty Acids

1. Haya ni mafuta ambayo mwili hauwezi kuzalisha badala yake unayategemea kutoka nje.
2. Ni mafuta muhimu sana kwa mwili wa binadamu kwani husaidia moyo kukaa vizuri, kuzuia kansa, uzito na ngozi.
3. Lisa ameyaita Omega 3, Omega 6 na Omega 9.
4. In short wewe unachotakiwa ni kula mafuta ya chia seeds, soya, walnut, tofu, mafuta ya samaki, mafuta ya dagaa, oil,mafuta ya dagaa, mafuta ya alizeti, almonds nk
5. Mfuta haya hutengeneza seli za mwili kukaa freshi.
6. Husaidia kubalansi homoni na hivyo kusaidia mzunguko wa uchavushaji wa mayai ya uzazi kwenda vizuri.
7. Husaidia mayai ya uzazi kuwa bora.
8. Husaidia follicle kutoa mayai ya uzazi kwa wakati. Sasa hiyo follicle imekaa kisayansi zaidi. Nadhani point ya kuondoka nayo ni wewe kugonga hayo mafuta kwa wingi.
9. Kwa maelezo zaidi soma kitabu cha Eating to Conceive by Lisa Olson. Kimeandikwa lugha ya Kizungu.
10. Shukrani sana Bilionea Frank Mamosa kwa kusupport utafiti huu wa lishe ya uzazi. Hata wewe ukipenda unaweza kusupport. Kumbuka mtenda wema haporomoki, akiporomoka anapata pa kuegemea!

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom