Mbunge Nicholaus Ngassa Aeleza Jinsi Jimbo la Igunga Linanufaika na Bajeti ya Wizara ya Kilimo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,030
974
Mbunge Nicholaus Ngassa Aeleza Jinsi Jimbo la Igunga Linanufaika na Bajeti ya Wizara ya Kilimo

Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa Akimpongeza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Mohammed Bashe baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo.

Jimbo la Igunga Linanufaika na Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwenye;
1. Ruzuku ya mbolea na pembejeo za kilimo.
2. Fedha za kufuatilia shughuli za Kilimo vijijini zitakazotolewa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
3. Visima vya wakulima wadogo Isakamaliwa na Igogo (Nanga)
4. Usanifu wa kina na ujenzi wa Bonde la kimkakati la Wembere
5. Usanifu wa kina na ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji wa Bwana la Mwamapuli (Mwanzugi)
6. Usanifu wa kina na Ukarabati wa Skimu ya Igurubi
7. Upembuzi yakinifu wa Skimu ya Makomelo
8. Ujenzi wa Nyumba za Maafisa Ugani Kining'inila na Kinungu

Wana Igunga, Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza Fedha nyingi kwenye Sekta ya Kilimo inayogusa maisha ya Wananchi wa Jimbo la Igunga kwa zaidi ya Asilimia Themanini.

NICHOLAUS GEORGE NGASSA
MBUNGE WA JIMBO LA IGUNGA
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-05-03 at 22.45.39.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-03 at 22.45.39.jpeg
    65 KB · Views: 5
Usanii mtupu, sasa fima Jimboni unakuta hakuna kitu kama hicho, ba umasikini umetamalaki,
 
Back
Top Bottom