MBUNGE BAHATI NDINGO, Mbunge wa Jimbo la Mbarali Akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo ya Shilingi Trilioni 1.2 Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,988
960

MBUNGE BAHATI NDINGO, Mbunge wa Jimbo la Mbarali Akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo ya Shilingi Trilioni 1.2 Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025

"Natoa pongezi za dhati kwa Wizara ya Kilimo kwa kazi kubwa nzuri waliyotufanyia wana Mbarali. Wakati Mhe. Hussein Bashe anasoma Bajeti yenye kurasa 307, neno Mbarali limetamkwa mara 27 na miradi mbalimbali iliyotajwa. Hii inaonyesha Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetutendea haki wana Mbarali " - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Ni kiu ya wana Mbarali kwa Miaka mingi kuona Serikali inatengeneza miundombinu ya umwagiliaji kwenye bonde ili tuwe na kilimo chenye tija. Wana Mbarali tutaandika historia ya Daktari Samia Suluhu Hassan kwa wino wa dhahabu" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2023-2024 Wana Mbarali tulipata miradi 8 ya umwagiliaji ambayo mpaka sasa wakandarasi wapo SITE. Shilingi Bilioni 98.2 zimeshuka Mbarali. Sasa mabwawa 8 wanatafuta Mkandarasi Mshauri ili yaende kuchimbwa Mbarali. Baada ya kukamilika miradi hii tunaamini Mbarali inakwenda kutulia" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Wana Mbarali asilimia 90 ni Wakulima na tulichokuwq tunahitaji ni kuwa na kilimo chenye tija. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameonyesha kuithamini na kuijali Mbarali kwa muda mfupi aliopokea kijiti. Wazee wa Mbarali wamenipigia simu wanasema Dkt. Samia Suluhu Hassan Tunashukuru Sana Sana Sana!" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Waziri Bashe, Mazungumzo na mwekezaji yatakapokamilika Tunaomba mashamba yakagawiwe kwa walengwa wakulima wadogo wa Mbarali, isitokee watu wachache wakajimilikisha maana wametumika kwa muda mrefu sana kama vibarua, leo wakapate Ardhi yao na wafanye shughuli zao" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Ni muhimu Sekta ya Kilimo ifungamanishwe na sekta zingine zinazoingiliana na wakulima, sasa hivi kilio kikubwa cha wakulima ni ushuru, ni lazima Waziri Bashe uwalinde wakulima kwa wivu mkubwa. Ushirikiane na TAMISEMI kutoa muongozo wa namna ya upatikanaji ushuru kwa wakulima" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Kilio cha wakulima Mbarali ni mkulima anatoka shambani kwenda kupeleka mazao yake nyumbani anatakiwa alipe ushuru. Akitoka nyumbani kupeleka Mashineni anadaiwa ushuru, akiwa anataka kuuza anadaiwa ushuru. Hii ni kinyume na Sheria iliyopo ya ushuru. Naibu Waziri wa Kilimo alitoa ufafanuzi Bungeni lakini bado hali inaendelea kuwa mbaya kwasababu wakulima wanatumia gharama kubwa na wasilipishwe kodi mara mbili mbili" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Wakulima wa Mbarali wanakumbwa sana na mikopo ya kausha damu kwasababu taratibu za kupata mikopo kwenye Mabenki bado ni changamoto. Mkulima mdogo hawezi kupata mkopo na akipata mkopo hauwezi kumtosheleza. Hekari moja ya Mpunga mpaka kumaliza kila kitu siyo chini ya Milioni moja mpaka Milioni moja na nusu" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Leo hii Mkulima mwenye Hekari tano akipewa Shilingi Milioni mbili haiwezi kumsaidia. Wakulima wanachofanya wanakwenda kukopa fedha ili wakivuna wapeleke mipunga. Waziri wa Kilimo endelea kuboresha upatikanaji wa fedha kwa maslahi ya wakulima hasa wale ambao hawana dhamana" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Benki, wakulima wanaoweza kupata mikopo ni wale ambao tayari wanazo dhamana na wana uwezo lakini kwa wakulima wadogo bado tuna changamoto. Mbarali mbolea zilifika lakini wakulima walipata shida kuzifikisha mashambani, barabara za Vijijini hazipitiki" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Mbarali kuna Skimu za Umwagiliaji 11 zinaendelea na zipo kwenye mpango wa Serikali na Mkandarasi Mshauri ndiyo mnamtafuta. Naomba zoezi lifanyike haraka ili mwaka ujao wa fedha tuone miradi ipo kwenye bajeti" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-05-05 at 23.40.24(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-05 at 23.40.24(1).jpeg
    93.8 KB · Views: 1
Ndugu mwandishi kulikuwa na haja gani ya kila baada ya Aya kuweka Jina na neno mbunge wa mbalali ikiwa hakuna sehemu umeonesha Kuna mchangiaji mwingine ni yeye tu ameongea? Eti ndugu mwandishi? Au ndugu mwandishi mimi ndio sijui uandishi? Au unasemaje ndugu mwandishi? Ulivyochukia ndivyo ulivyotuboa wasomaji wako ndugu mwandishi.
 
Ndugu mwandishi kulikuwa na haja gani ya kila baada ya Aya kuweka Jina na neno mbunge wa mbalali ikiwa hakuna sehemu umeonesha Kuna mchangiaji mwingine ni yeye tu ameongea? Eti ndugu mwandishi? Au ndugu mwandishi mimi ndio sijui uandishi? Au unasemaje ndugu mwandishi? Ulivyochukia ndivyo ulivyotuboa wasomaji wako ndugu mwandishi.
Nashukuru kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom