Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungeni Jijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,030
974

MHE. TIMOTHEO MNZAVA, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungeni Jijini Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mnzava akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwenye maeneo ya Kilimo cha Umwagiliaji, Zao la Chai, na Zao la Mkonge.

"Mwaka 2019/2020 eneo lililokuwa linatumika kwa shughuli za Umwagiliaji ilikuwa ni Hekta 475,052 lakini leo eneo la shughuli za kilimo cha Umwagiliaji limefika Hekta 727,280.66 na kama miradi ikikamilika tutafika hekta 983466 sawa na 86% ya malengo tuliyowekewa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Tume ya Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo mnastahili pongezi kwa kazi kubwa mnayoifanya. Tuongeze eneo linalofaa kwaajili ya Kilimo cha Umwagiliaji. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutoa fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 18 kuendelea mradi wa Bwawa la Mkomazi" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Niwahakikishie wananchi wa Kata za Mkomazi, Mkumbala, Mazinde na Mombo na Waziri wa Kilimo, na niwaondoe wasiwasi mradi wa Bwala la Umwagiliaji la Mkomazi utatekelezwa maana ndiyo dhamira yetu, nia yetu, maisha yetu, uhai wetu na Uchumi wetu. Mkuu wa Mkoa amefika amezungumza na wananchi" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Miradi ya Umwagiliaji inatumia fedha nyingi sana, Wizara wekeni utaratibu wa kufanya Miradi iwe endelevu, wananchi wapewe elimu. Tume ya Umwagiliaji inapewa fedha nyingi na Serikali kutekeleza miradi, tuangalie namna ya kuijengea uwezo Tume na isikae kwa asilimia 100 kusubiri kupewa fedha na Serikali, kuwe na namna ya kuifanya Tume kutengeneza mapato ili mambo yake yaweze kuwa mazuri waendelee kukarabati Skimu za Umwagiliaji" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Mwaka 2023 tulizungumza kuhusu ukarabati wa Skimu za Umwagiliaji za Mombo, Mafuleta, Ukamezangu. Mto wa Kwamkumbo umejaa udongo, maji yanapoteza uelekeo yanaingia kwenye mashamba ya wananchi. Waziri wa Kilimo unapokwenda kukarabati Skimu ya Mombo tuhakikishe tunatengeneza eneo la Kwamkumbo ili wananchi wafanye Kilimo vizuri" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Sina mashaka na Bodi ya Chai, wanajitahidi kufanya kazi nzuri. Nilisoma kwenye Website ya Wizara ya Kilimo ya Taarifa ya tarehe 15 Februari, 2022. Karibu nusu ya wakulima wa Chai tulionao ni Wakulima wadogo. Zao la Chai linakabiliwa na changamoto kuu mbili; kwanza ni Bei (bei ni ndogo inaumiza wakulima wetu) ambayo inachangiwa sana kwenye soko la Dunia. Niwaombe Wizara, Bodi ya Chai taasisi zingine tuweke mkazo kwenye kuongeza ubora kwenye Chai yetu ili ishindane vizuri kwenye masoko" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Wakulima wadogo wa Chai wanategemea viwanda vya wakulima wakubwa ambao wamewekeza kwenye mashamba makubwa. Mohammed Enterprises wamefungua kiwanda wameanza kuchakata Chai ya kwao wenyewe, wanajiandaa kwenda kununua Chai ya wakulima. Serikali ikae na wawekezaji kama hawawezi kuendelea na kazi za uzalishaji tutafute namna ya kuongeza nguvu viwanda wapewe wakulima wadogo" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

Ukienda Kenya, asilimia 75 ya viwanda vinasimamiwa na wakulima wadogo. Tuwape namna wakulima wadogo wawe na viwanda vya kwao na wasitegemee viwanda vya wawekezaji ili wawekezaji wakiyumba mambo yao yasiyumbe na Biashara ya Chai iendelee kuwa nzuri" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Watu wa Mkoa wa Tanga Tunaishukuru na kuipongeza Serikali kwa kufufua na kurejesha zao la Mkonge (Katani) kwenye ramani ya mazao ya nchi yetu. Lakini pia tumeongeza uzalishaji, tulikuwa Tani elfu 36 lakini leo tupo kwenye zaidi ya Tani elfu 56. Lakini kati ya Tani elfu 56, asilimia 70 tunapeleka nje ( Export). Maana yake tunakwenda kuuza ajira za watu wetu na kodi zetu na tunakwenda kuishi kwa kutegemea soko la wenzetu na ikitokea changamoto kama ya COVID19 wakulima wetu wanaingia kwenye matatizo" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Waziri wa Kilimo, ongeza nguvu kuimarisha soko la ndani la Mkonge hasa kwa kuimarisha viwanda. Tanzania bado tuna changamoto ya nyuzi za Plastiki na magunia ya nyuzi. Tanzania mahitaji ya Maguni kwa mwaka ni zaidi ya pisi Milioni 15. Waziri kaa na watu waliopewa viwanda vya kamba na magunia tusiuze ajira za watu wetu na tuhakikishe usalama wa soko la watu wetu kwenye zao la Mkonge" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini
 

Attachments

  • maxresdefaultwertfg.jpg
    maxresdefaultwertfg.jpg
    95.3 KB · Views: 4
  • 1I4A7697mnbgyt.jpeg
    1I4A7697mnbgyt.jpeg
    207.8 KB · Views: 4
Back
Top Bottom