Makapuku Forum

Nyumba inayodaiwa kuwa ya mkurugenzi wa gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe iliyoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam, imekamatwa kwa ajili ya kupigwa mnada, ili kulipa deni la malimbikizo ya mishahara ya waliokuwa waandishi na wahariri wa gazeti hilo, Sh62.7 milioni.

Nyumba hiyo ya ghorofa moja iliyoko katika kiwanja namba 9, Mtaa wa Feza, barabara ya Chipata, Mikocheni A imekamatwa leo Jumatano, Februari 28, 2024 na dalali wa mahakama, kampuni ya udalali ya MM Auctioneer & Debt Collectors.

Dalali huyo alifika katika nyumba hiyo saa 3:40 na kuegesha gari lake nje ya geti la nyumba hiyo.

Baada ya muda mfupi Dadley, ambaye ni mtoto wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alitoka nje na kumfuata dalali huyo na baada ya kusalimiana, dalali huyo alijitambulisha na jukumu alilokwenda kulitekeleza.
Screenshot_20240228_151320_InstaPro%20.jpg
 
Nyumba inayodaiwa kuwa ya mkurugenzi wa gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe iliyoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam, imekamatwa kwa ajili ya kupigwa mnada, ili kulipa deni la malimbikizo ya mishahara ya waliokuwa waandishi na wahariri wa gazeti hilo, Sh62.7 milioni.

Nyumba hiyo ya ghorofa moja iliyoko katika kiwanja namba 9, Mtaa wa Feza, barabara ya Chipata, Mikocheni A imekamatwa leo Jumatano, Februari 28, 2024 na dalali wa mahakama, kampuni ya udalali ya MM Auctioneer & Debt Collectors.

Dalali huyo alifika katika nyumba hiyo saa 3:40 na kuegesha gari lake nje ya geti la nyumba hiyo.

Baada ya muda mfupi Dadley, ambaye ni mtoto wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alitoka nje na kumfuata dalali huyo na baada ya kusalimiana, dalali huyo alijitambulisha na jukumu alilokwenda kulitekeleza.View attachment 2919178
Eeh jirani imekuaje tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom