Stories of Change - 2023 Competition
Oct 26, 2016
1
1
Unamkumbuka Mwanafalaki na Mwanahisabati aliyekuwepo zaidi ya miaka elfu mbili na mia mbili iliyopita katika kisiwa cha Sisilia ambacho leo tunaita Italia. Mtaalamu ,huyu alikuwa anaitwa Archmedes mtoto wa Phidias ambaye pia alikuwa Mwanafalaki. Katika kipindi cha uhai wake kabla ya kuja kuuliwa, aligundua kanuni ya kuelea ambayo mpaka leo wanafunzi wa Fizikia wanaisoma shuleni. Kanuni hii aligundua wakati yupo bafuni alipoingia kwenye maji,akaona maji yanakuja juu na hapo akakumbuka ile kazi aliyopewa na mfalme wa Sisilia wa wakati huo (Mfalme Hiero wa pili),alipewa kazi ya kugundua kuwa kama taji la mfalme lina dhahabu tupu au limechanganywa na shaba. Na kama limechanganywa ni kwa kiasi gani.? Mfalme alimtilia shaka mtengeneza taji kuwa amechanganya dhahabu na shaba. Archemedes baada ya kuona maji yanapanda juu alivyoingia,akatoka nje uchi na kukimbia mitaani huku akisema "HEUREKA,HEUREKA" yenye maana ya "Nimegundua nimegundua."

Archmedes alisema: “Uzito wa kitu kinachozamishwa chote au sehemu yake ndani ya maji ni sawa na uzito wa maji yaliyomwagika baada ya kitu hicho kuzamishwa."

Ukichunguza kwa wakati huu lugha ya Kiswahili inakua na kuenea nje ya mipaka yake . Lakini tukiwa kama wahusika wa lugha, tunaweza tukaipeleka mbali zaidi ya hapa lugha ya Kiswahili. Katika kanuni ya Archmedes inatufundisha kuwa maji ambayo yapo katika chombo fulani na baadaye kikaingizwa kitu katika maji aidha chote au nusu ya hicho kitu kwa maana ya kuzamishwa nusu basi kuna maji ambayo yatamwagika au yale maji ambayo yatakuja juu. Jibu ni kuwa uzito wa maji yaliyomwagika ni sawa na uzito wa kile kitu na kama siyo sawa basi itatofautiana kwa kiasi kidogo.Sasa tufanye chombo kilichowekwa maji ni dunia au bara, pia tufanye maji ni mafanikio na pia kitu kinachowekwa katika maji ni Lugha, na yale maji yanayomwagika ndiyo kipimo cha lugha ile jinsi ilivyofanikiwa. Kwa mfano tukiwatazama Wakorea, wao tunagundua walishaweka lugha yao muda katika chombo na kuthibitisha hili tazama tu Watanzania walivyokuwa wanafahamu maneno ya Kikorea Oppah (Kaka au Mchumba wa Mwanamke) Kumowo (Asante), muda mwingine wameiga hadi baadhi ya utembeaji au wameiga mavazi ambayo wanavaa Wakorea katika sinema zao. Lakini hii ni kwa sababu wameweka lugha yao katika dunia au bara katika chombo chenye maji na wanahitaji wafanikiwe. Jiulize wameiweka Lugha yao kwenye maji kwa mtindo upi, na hapo utagundua Sinema ndiyo mbinu pekee kubwa wameitumia katika kuendeleza lugha yao, lakini kama nilivyosema awali watu wanaishi Kikorea lakini hili si kosa ila tu Wakorea wanatumia nafasi vizuri. Na kama watanzania wengi wapenzi wa sinema wangeambiwa wachague nchi ya kutembelea wangechagua Korea. Kwa hali hiyo Utalii katika nchi kama hiyo ni rahisi kukua.

Na sisi Waswahili pia tunaweza tukaipeleka mbali lugha yetu. Najua kuwa na sisi tushaiweka lugha yetu katika chombo, maji yaliyomwagika ni mengi kwa mtazamo wetu au ukilinganisha na tulikotoka lakini nina imani tunaweza kufanya vizuri zaidi ya hapa. Ningetamani siku moja kusoma mahali kuwa watu kutoka nje wanajifunza kiswahili au misamiati ya Kiswahili kupitia Sinema zetu kwa kiasi kikubwa.Au wanaiga Utamaduni wetu kwani lugha na utamaduni ni vitu ambavyo haviwezi vikatengana. Kwani wakorea na mataifa mengine wamewezaje na sisi tushindwe, ni kujipanga. Kuna wengine wanazani sababu kubwa ni Teknolojia yetu ya Sinema ni ndogo, inaweza ikawa kweli kwa aina ya sinema ambazo wanazungumzia, kama unazungumzia Sinema za maroboti kwa nini tusione tupo nyuma katika kila kitu ? maana tunafanya filamu ambazo si rafiki katika mazingira yetu, kwa nini tusihitaji hiyo teknolojia inayozungumziwa? lakini tujiulize Kwenye tamaduni zetu kuna teknolojia.? kwa nini tusifanye kitu ambacho tuna uwezo lakini kwenye ubora wa hali ya juu. Nimetolea mfano Sinema lakini najua vipo vingi sana. Serikali pamoja na wadau wanahitajika katika kuyafanya mambo ambayo yanakuza na kueneza Kiswahili ndani na nje ya nchi.

Hongera kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuruhusu mtaala kuangaliwa upya na sasa rasimu ishatoka ambayo ikipita tutapiga hatua kubwa sana ya kimaendeleo katika sekta zote kwani inaeleza kuwa Kiswahili ndiyo lugha ya mawasiliano na ya kufundishia na mbinu hii wenzetu walishatumia katika masuala mbalimbali yanayohusu matumizi ya lugha mfano China wanatumia Kichina, Japan wanatumia Kijapani, kwa hiyo hii itazidi kuzalisha wataalamu ambao watatumia Kiswahili katika masuala mbalimbali na maendeleo yatakuja kwa watu wote maana darasani uelewa utazidi kukua na tutakuza wataalamu wa ndani.

Lakini pia bila kusahau wasanii wote ambao wakitumia lugha yetu nzuri ya Kiswahili wataweza kushawishi wasiojua Kiswahili kutaka kujifunza lugha ya Kiswahili, Hongera pia kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongofleva. Ali Saleh Kiba, Nasibu Abdul, Ambwene Yesaya (AY), Rajab Abdulkahali Ibrahim (Harmonize) na wengineo.

Kama Chombo kilichotiwa Maji ni Dunia, najua Lugha tumeiweka ndani, kuna maji ambayo yamemwagika ndiyo ishara ya kufanikiwa...lakini ni vizuri tukahakikisha tunaiweka zaidi au kuzamisha zaidi ...ili maji ambayo ni mafanikio yawe mengi... katika Kanuni ya ‘Archmedes’ naiona vizuri lugha yetu nzuri ya Kiswahili...
 
Back
Top Bottom