Lissu: Zanzibar ni koloni la Tanganyika

Yah kinyume chake ndio ukweli. Sasa nani koloni wa mwenzake kama wao wanaweza kuja bara wakafanay chochote bila kuhitaji kuwa ni kitambulisho. Kama wao wanafaidika na kazi za abra ila mtanganyika labda ukafanye kazi hotelini ila si serikalini. Kama wao hadi wanafikiria twende kwao kwa passport, kama wanaweza kumiliki ardhi. Muda mwingine wanasiasa husema lolote kuwafurahisha walio wengi.

Hata Msumbiji walipokuwa koloni la Wareno, Mzambikano aliruhusiwa kwenda Ureno bila kizuizi chochote. Hakuhitaji kibali wala passport, lakini hiyo haikuifanya Mozambique kutokuwa koloni la Ureno.

Kiuhalisia Tanganyika iliichukua Zanzibar kwa usaidizi wa US, baada ya Kenya kukataa kuichukua Zanzibar. Kiuhalisia Zanzibar ni mali ya Tanganyika. Ni jambo la kawaida mtoto kuwa na uhuru na mali za Baba kuliko baba kuwa na uhuru na vitu vya mtoto. Zanzibar ni mtoto, ndiyo maana anadeka.
 
Kiumbe kinachougusagusa na kuuchokonoa muungano hakitufai, huyu bwege logic yake kubwa ni ku attracts wazanzibar kwenye chama Chao, kwa ku inflict, na kanuni anayoitumia ni hiyo ya kukalia kikoloni, ametoka nje ya malengo mazima ya kanuni za vyama,na nini vyama vinapaswa kufanya!, tulitaraji aje na sera safi za kuunyanyua uchumi wetu, na kujenga taifa imara zaidi, yeye amekuja na sera za kubomoa kabisa taifa letu,
A STUPID POLITICIAN!
 
Utukufu wake ni upi ? Kuua Wazanzibari au ?
Naona chadomo mmekosa pa kushika sasa mmebakia kuuchokonoa muungano, CHADEMA SI CHAMA KINACHOITAKIA MEMA NCHI HII YA TANZANIA!,
Kuna makosa makubwa sana katika sheria za uanzishwaji vyama, ilipaswa suala la muungano kutokuwa ajenda za kujadiliwa hovyo hovyo, na ilistahili liwe chini ya rais na waziri anayelishughulikia na iwe jinai kwa atakaye jihusisha na suala hili.
N. B, LICHUKULIWE NA JMT
 
Kwa hiyo chama tawala zanziba ni kipi? Chairman wa ccm ni mzenj kama anataka muungano wa uvunjwe anaweza maana ni rais na mwenyekiti wa ccm

Kwahiyo unahisi kuwa Chairman wa CCM inakutosheleza kufanya unachotaka? Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar unalindwa na CCM, Tiss na JWTZ. Kwahiyo yeye kama yeye hawezi kuwa na maamuzi bila ya kupata support kutoka kwenye makundi hayo matatu.
 
Kinyume chake? 🐼
Ina alternate kuna msimu Zanzibar huwa koloni la Tanganyika na kuna msimu Tanganyika huwa koloni la Zanzibar. Inategemea nani yupo Madarakani.

Kwa sasa Tanganyika ni koloni la Zanzibar kama ule wakati wa wakina Diria...ila Kipindi cha Mkapa, JK na Magufuli Zanzibar ilikuwa koloni la Tanganyika.

Kwa sasa huwezi kusikia kina Jusa na Othuman wakitaka Zanzibar huyu. Ila subiri nchi achukue Bashungwa. Watapaaza sauti hadi kwenye koo ya kutaka Zanzibar kama alivyokabidhiwa Shamte na Malkia.

Mambo ni zamu kwa zamu. TL afanye ku update hiyo clip yake.
 
Kwahiyo unahisi kuwa Chairman wa CCM inakutosheleza kufanya unachotaka? Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar unalindwa na CCM, Tiss na JWTZ. Kwahiyo yeye kama yeye hawezi kuwa na maamuzi bila ya kupata support kutoka kwenye makundi hayo matatu.
Unampa madaraka ya kupangua na kupanga watakaomuunga mkono. Kama ana uwezo wa kuondoa wapinzani wake kwenye chama na serikali kujihakikishia nafasi ya kugombea tena hata hili analiweza.
 
Unampa madaraka ya kupangua na kupanga watakaomuunga mkono. Kama ana uwezo wa kuondoa wapinzani wake kwenye chama na serikali kujihakikishia nafasi ya kugombea tena hata hili analiweza.

Mpaka akaweza kuwaondoa hao wapinzani ujue anayo support kutoka ndani ya mfumo. kuondoa wapinzani ndani ya chama ni ishu ndogo sana ukilinganisha na ishu ya muungano
 
Back
Top Bottom