Lissu: Zanzibar ni koloni la Tanganyika

Alicho ongea lissu sio ujinga labda kama una tafsiri yako ya ujinga.

Na Tanganyika sio koloni la Zanzibar ukielewa yule anaye ng'ang'aniza muungano na yule anaye pinga ndipo utajua yupi ndio mkoloni halisi.

Alicho ongea Lissu ndio ukweli halisi.
Mkoloni wa wa-Zanzibari ni CCM, kwa sababu hata sisi wa-Tanganyika hatuitaki Zanzibar.
 
Mkoloni wa wa-Zanzivari ni CCM, kwa sababu hata sisi wa-Tanganyika hatuitaki Zanzibar.
Sahihi kabisa.

Lissu alipaswa kueleza hilo; nadhani kapitiwa tu.
CCM wa huku Tanganyika ndio walioshikriwa na wenzao wa Zanzibar wanaoogopa Tanganyika ikijiondoa maslahi ya hao CCM wa visiwani yatafikia kikomo.
 
SANA, MIMI NINA LIBRARY YA CLIP ZAKE......huyu mtu na akili sana tena sana! niliwahi kusema kuwa Lisu unaweza kumlinganisha na Albert Einstein!
HeeeeHeee! Uliwahi kumsikiliza Einstein, mkuu 'Retired'?

Lakini ninakubaliana na wewe kuhusu uwezo wa kujieleza na kutambua mambo alionao Lissu.
 
Sawa sawa kabisa. Sijui Lissu kaingiwa na mtindio wa akili ukubwani?
Koloni litawezaje kuweka mtu wake awe mkuu wa nchi, na hilo koloni lifaidike zaidi kiuchumi kuliko mkoloni mwenyewe.

Lissu ni muhimu achunge sana kauli zake tata za aina hii. Vinginevyo zitaanza kumshushia heshima yake katika jamii.
Yupi ana lazimisha muungano kwa kimabavu kati ya Tanganyika na Zanzibar ?

Nafikiri unafahamu sasa sijui ni nani aliyekosa akili kati ya Lissu na wewe katika hilo
 
Sahihi kabisa.

Lissu alipaswa kueleza hilo; nadhani kapitiwa tu.
CCM wa huku Tanganyika ndio walioshikriwa na wenzao wa Zanzibar wanaoogopa Tanganyika ikijiondoa maslahi ya hao CCM wa visiwani yatafikia kikomo.
Watanganyika kupitia CCM ndio wanao amua hata Rais Zanzibar nani awe na nani asiwe hata kwa kutumia majeshi ya Tanganyika huu ni ukoloni wa wazi wazi
 
Nafikiri unafahamu sasa sijui ni nani aliyekosa akili kati ya Lissu na wewe katika hilo
Tueleze kwanza zako kabla ya kukimbilia kwa Lissu. Naona kwako kichwani ni mtupu kabisa hata kama huwezi kujitetea mwenyewe.
Nimekusoma vibandiko vyako kadhaa kwenye mada hii, sioni chochote cha kunishawishi kuwa kichwani zinakutosha.

Baada ya kusema hayo, ukitaka nikufundishe kidogo ili nawe uweze kusimama na kujenga hoja kuhusu maswala kama haya, anza kushika adabu yako. Umenielewa?
 
Wewe ni mwanamke au mwanaume ?
 
Watanganyika kupitia CCM ndio wanao amua hata Rais Zanzibar nani awe na nani asiwe hata kwa kutumia majeshi ya Tanganyika huu ni ukoloni wa wazi wazi
Sikiliza, usipayuke hovyo hapa. Tulia na ujadili mada na siyo kulazimisha tu unavyotaka wewe.

Haijawahi kutokea nafasi nzuri kama iliyopo sasa hivi, kwa Wazanzibari kujiondoa kwenye muungano bila ya rabsha nyingi.
Huko CCM sasa hivi hakuna mtu yeyote mwenye ushawishi tena wa kung'ang'ania Muungano, kama Mwenyekiti wao na Rais, Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yetu akitaka iwe hivyo.
Na zaidi, huyo huyo Mwenyekiti na Rais, na hata akiwa Makamu wa Rais, amekwisha fanya mengi sana ya kuwaudhi waTanganyika kwa lengo la kulegeza Muungano huo.
Leo hii anachotakiwa kufanya, ni kuitisha tu kura ya maoni ya wananchi, na utaona mwenyewe waTanganyika wanataka nini kwenye muungano huu wa kipuuzi.
 
Back
Top Bottom