Jan 28, 2024
48
48
Screenshot_20240405-184828.jpg

Juzi (03.04.2024) tumeshuhudia Mh. Raisi akizindua Tume ya ulinzi wa taarifa binafsi na kusisitiza juu ya ulinzi wa taarifa binafsi kwakufata sheria. Sasa, je ni kwanini Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ni muhimu kwetu watanzania? Leo nitawasanua wadau juu ya umuhimu wa sheria hii mpya nchini Tanzania .

Kwakuanza, sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, maarufu kama PDPA, ilitungwa na kupitishwa Tanzania mwaka 2022 ili kuweka mwongozo wa jinsi taarifa binafsi zinavyopaswa kushughulikiwa. Sheria hii imeanzisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kama mlezi wa taarifa zetu na faragha zetu, Tume hii ina kazi ya kuhakikisha kwamba sheria na kanuni za ulinzi wa taarifa binafsi zinafuatwa kwa umakini na haki.

Lakini wait, nini maana ya taarifa binafsi? Aya ya 14 ya kifungu cha 3 cha PDPA imeeleza maana ya taarifa binafsi, lakini hapa nitaelezea kwa upana wake na kwa urahisi. Taarifa binafsi (Data) ni taarifa zote zinazomuhusu mtu binafsi, hapa namaanisha mimi, wewe ama sisi. Taarifa hizi ni kama vile kabila la mtu, uraia, dini, umri, na hali mbalimbali za maisha yake, kama vile hali ya ndoa, elimu, historia ya matibabu, historia ya uhalifu, na historia ya ajira. Lakini taarifa hizi ni pamoja na maelezo madogo madogo, kama vile nambari za utambulisho, alama, au taarifa maalum, kama vile anwani, alama za vidole, au aina ya damu. Aidha, ikiwa jina la mtu linaonekana kwa mtu mwingine, bado lina considered sehemu ya taarifa zake binafsi, taarifa hizi pia zinajumuisha mawasiliano ya faragha yaliyobadilishana kati ya mtu huyo na mwingine. Inshort, hii ni taarifa yeyote ambayo inaweza kumtambulisha mtu.

Pia PDPA inasisitiza kuhusu umuhimu wa kuhifadhi taarifa binafsi kwa usalama, na kuweka miongozo ya jinsi ya kukusanya, kuchakata, kuhifadhi, na kufichua taarifa hizo. Inataka udhibiti na wachakataji wa data kuchukua hatua stahiki kuzuia ufikiaji, upotevu, au uharibifu usioidhinishwa wa data.

Katika sheria hii, haki za wamiliki wa data zimewekwa wazi, wakiruhusiwa kufikia, kusahihisha, na hata kufuta data zao. PDPA pia inatoa adhabu kali kwa yeyote atakayekiuka kanuni hizi, na inahitaji usajili wa wadhibiti na wachakataji wa data pamoja na uteuzi wa maafisa wa ulinzi wa data.

PDPA ya Tanzania inalenga kulinda faragha na data za watu binafsi. Inaweka malengo yaliyo wazi, ikilinda data dhidi ya uvamizi usiofaa. Inajenga mfumo wa kisheria na kitaasisi kwa ajili ya ulinzi wa data, ikitekeleza hatua za kuzuia ufikiaji haramu wa data na kuweka miongozo mikali ya uhifadhi na utupaji wa data.

Kwa kifupi, PDPA imekuwa ngao imara, ikiunda mazingira salama ya kushughulikia taarifa binafsi nchini Tanzania, na kuhakikisha kwamba faragha na data za watu zinalindwa kwa mujibu wa sheria. Ni muhimu kusoma na kuielewa sheria hii 👉 OAG MIS | Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022, pamoja na kanuni zake au kumtafuta mtaalamu wa maswala haya ili kupata uelewa mpana zaidi​
 
Back
Top Bottom